Pinda kamsusa Majaliwa?

Pinda kamsusa Majaliwa?

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,461
Si jambo la kawaida kabisa, kuona Waziri Mkuu mstaafu, akisusa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa anayeziba nafasi yake; lakini leo mizengo pinda na familia yake hawakuonekana kabisa Ikulu ya Chamwino. Je, ni hasira za kuukosa urais?
 
Usihukumu kabla ya kumsikiliza kwanza au kujua sababu. Pengine kuna genuine reason ya yeye kutohudhuria event hiyo
 
Si jambo la kawaida kabisa, kuona Waziri Mkuu mstaafu, akisusa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa anayeziba nafasi yake; lakini leo mizengo pinda na familia yake hawakuonekana kabisa Ikulu ya Chamwino. Je, ni hasira za kuukosa urais?

Kwann usimulize pinda mwenyewe
 
Mwacheni mzee wa watu apumzike jamani!
 
Si jambo la kawaida kabisa, kuona Waziri Mkuu mstaafu, akisusa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa anayeziba nafasi yake; lakini leo mizengo pinda na familia yake hawakuonekana kabisa Ikulu ya Chamwino. Je, ni hasira za kuukosa urais?
Ni aibu mwandishi wa habari kuleta uchonganishi na uchochezi usio wa msingi! Hivi ni lazima mizengo atokee pale na hata kama hayupo ndio sababu ya kusema amesusa? acha uchochezi

Hivi unajua umefanya uhalifu wa kimtandao na ni haki yako kupandishwa kizimbani?
 
Nadhani ingekuwa vizuri zaidi kama angefanya juhudi zaidi kufahamu sababu za Pinda kutokuhudhuria.

Kwa nini unadhani kama anaweza kususa wakati muda wake kama waziri mkuu umemalizika?

Inawezekana amepata udhuru kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wake.
 
.
Manyerere anatafuta matangazo ya kipeperushi chake
 
Leo nimeamini kuna mtu huwa anatumia ID yako au ni shemeji nini? leo hakuwepo umeingia mwenyewe engine room ndio umetoka na utumbo huu?
 
Pinda hawezi kwenda kwenye shughuli yeyote ya magufuli anajua ni raisi wa kupachikwa mbona uwanjani kuapishwa magufuli hakuepo hamkuuliza hawezi kubariki wizi wa kura
 
Ungemuuliza kwanza ujue sababu.halafu Manyerere kwny thread zingine tumia fake ID,pumba ukilinganisha na status yako

Halafu MTU kama huyu aandikie lile gazeti lao kisha tulifanye rejea?
Haki ya nani mtu alete habari kisha a quote Jamhuri eti ndio chanzo! Nitapeleka maombi kwa mods apewe ban hata ya masaa
 
Angekuja mngesema gharama kubwa zimetumika kumleta
 
Labda uwaombe Moderator waifute kukuondolea aibu lasivyo umetenda kosa.
 
Last edited by a moderator:
Manyerere Jackton nadhani ID yako imevamiwa. Hivi ni wewe nilikuwa nakuona jana Azam tv ukiwa na Dr Gideon Shoo mkijadiliana kuhusu PM Majaliwa,mkiongozwa na B.Muhuza au majina yamefanana? Huu uzi si wa kaliba yako mkuu. Sumaye na EL mbona huwaulizii? Acha uchonganishi.
 
Last edited by a moderator:
Wewe mleta mada ni lazima utakuwa umeonya mvinyo
kama wa vijana wa UKAWA (wote tuna ujua) kwani hii sio bure kabisa.....
 
Si jambo la kawaida kabisa, kuona Waziri Mkuu mstaafu, akisusa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa anayeziba nafasi yake; lakini leo mizengo pinda na familia yake hawakuonekana kabisa Ikulu ya Chamwino. Je, ni hasira za kuukosa urais?

wakikuita siku wanakabihiana kukabidhiana ofisi, njo na conclusion
 
Si jambo la kawaida kabisa, kuona Waziri Mkuu mstaafu, akisusa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa anayeziba nafasi yake; lakini leo mizengo pinda na familia yake hawakuonekana kabisa Ikulu ya Chamwino. Je, ni hasira za kuukosa urais?

Sasa kama hakualikwa ajipeleke! Aibu!!!
 
Back
Top Bottom