Pinda hawezi kukwepa kung'olewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda hawezi kukwepa kung'olewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Acha Uvivu, Apr 20, 2012.

 1. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Zimefika saini 73, hizo zimezidi hata zile 70 zilizotarajiwa. Hongeza Zitto na Filkunjombe.
  PINDA lazima atang'oka.
  Kwanza wabunge wote wa CCM walio upande wa Lowassa, akiwemo yeye pia watapiga kura ya kufanikisha mchakato, ili aibu ya kujiudhuru isiishie kwake, na ili kumtikisa rais aliyemchafua kwa sera ya kuvuana magamba.
  Pili, kauli ya Filkunjombe baada ya kuhojiwa na BBC akisema kitendo cha kusaini si yeye pekee bali ni pamoja na wananchi wa Ludewa waliomtuma. Hapa kawashitaki wabunge wengine wa CCM kwa wananchi wao waliowatuma, kwamba nao itawalizimu kuiunga mkono hoja kama ishara kuwa wanawaheshimu wapiga kura wao kama alivyofanya yeye. Lasivyo safari zao za kisiasa zatakuwa hatarini na kutupa nafasi laini CDM kuchukua majimbo ya wabunge wanafiki wa CCM.
  Tatu, Ushauri wa Zitto kwenye twitter kuwa wananchi wawashauri wabunge wao kwa ujumbe mfupi au kuwapigia simu itawapa wakati mgumu wabunge wengine wa CCM na watalazimika kushiriki kumuondoa waziri mkuu (PINDA). Nami naongezea kuwaasa kuwa tuwatafute hao wabunge wetu. Tunakaribia kufanikiwa msife moyo. Kwa wale ambao wabunge wao pia ni mawaziri kama mimi, Mhe. Mwandosya wasitishike kuwataka wapige kura ya ndio. Pinda atang'olewa tu.
  Nne, hoja itawasilishwa wakati wa bunge la bajeti baada ya kanuni inayotaka siku 14 hoja iwe imefika kwa ofisi ya spika kabla ya kupiga kura ya maoni. Sasa bunge hilo ndo hatari maana litaamsha hasira kwa wabunge wetu wote kupinga madudu ya Mkulo. Bajeti ya nchi masikini kama Tanzania kuandaliwa Marekani! Jamani inaumiza sana, maradhi, chakula na posho vyote hivyo gharama kubwa sana kwa nchi masikini kama Tanzania. Mkulo kweli sio mwaminifu. Na Pinda lazima atang'oka lasivyo hao mawaziri wajiuzuru mapema kumnusuru. Hongera Zitto Kabwe na Filkunjombe na wabunge wengine wote mnaojali.
   
 2. s

  sugi JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  ngoja nimsms mbunge wetu maana kakaa kiboyaboya tu,anaonekana hatopiga kura
   
Loading...