Pinda hajawahi kuhiji kaburi la Baba wa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda hajawahi kuhiji kaburi la Baba wa Taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jul 25, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Familia ya Nyerere imesema tangu Mizengo Pinda achaguliwe kuwa waziri mkuu hajawahi kuitembelea familia hiyo wala kuzuru kaburi la hayati Baba wa Taifa. Akiwakaribisha madiwani wa manispaa ya Sumbawanga waliotembelea familia hiyo Butiama jana mtoto wa familia hiyo Magige Nyerere amesema viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wote wa NEC wamewahi kuzuru kaburi na kuitembelea familia hiyo isipokuwa yeye, amewaomba madiwani hao kufikisha ujumbe kwake kuwa kitendo hicho kinaweza kutafsiriwa kama ni kuisusia au kuibagua familia hiyo.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Kwani Nyerere kawa mtume ?
   
 3. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kaazi kwelikweli...
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Labda mila za kwao zinakataza kutembelea makaburi ya wafu. Hawa si ndio wale wataalamu wa kuruka na nyungo?
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..kwa uelewa wangu Pinda na mkewe walimtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake msasani.

  ..Magige Nyerere aelewe jukumu la kwanza la Waziri Mkuu Pinda ni kushughulikia matatizo ya wa-Tanzania. masuala ya kuzuru makaburi ya viongozi waliopita ni ziada na wakati mwingine nje ya majukumu ya waziri mkuu.

  ..sina uhakika kama Pinda ametembelea makaburi ya mashujaa wa vita vya Kagera kule Bunazi Kagera, au makaburi ya mashujaa wa vita vya Msumbiji kule Naliendele Mtwara, au makaburi ya mashujaa wengine kama Edward Sokoine, Wilbard Kleruu, Sethi Benjamin,...

  ..kwa kauli hii nadhani Magige ameteleza.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tata,
  Magige na Madaraka are 2 different individuals. Madaraka is the quiet one.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Mwamba Jasusi,

  ..na mimi nimeteleza hapo.

  ..aliyetoa kauli hii ni Magige. nimerekebisha kule kwenye post yangu ya awali.

  ..kwa mtizamo wangu Magige hakupaswa kulalamikia suala la Pinda kutotembelea Butiama.

  NB:

  ..aliyewatabiria CDM ushindi ni huyu au mwingine??
   
 8. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Lazima washangae kwa nini Pinda hajatembelea kaburi la baba wa wakatoliki Tanzania na yeye ni mkatoliki safi
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ni huyo huyo Magige.
   
Loading...