Pinda hafikirii kumrithi Kikwete

Pinda hafikirii kumrithi Kikwete

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema hana mawazo ya kuwania urais kwa kuwa ni kazi kubwa, ngumu, na yenye lawama.

Waziri Mkuu ametoa msimamo huo jana mjini Tabora, baada ya mshairi Ramadhan Katwila ‘ Mv Liemba’, kusoma shairi akimwomba Mungu kumjaalia awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza ngwe yake mwaka 2015.

Pinda amesema hana hamu ya kuwa Rais, kwa sababu ni kazi ngumu tofauti na watu wanavyofikiri.

“Baba wa Taifa (Mwalimu Nyerere) alisema Ikulu si mahali pa kukimbilia, msifikiri kauli ile ni ya uongo.“Urais ni kazi ngumu. Hata hii kazi ya uwaziri mkuu ni ngumu sana, sema kwa vile tu ni lazima mzigo mzito akabidhiwe ‘Mnyamwezi’.

“Ni kazi ambayo kila mtu anakutupia lawama hata ambazo hustahili. Utasikia mwingine anasema kwanza liangalie lilivyo, kila siku utaandamwa na magazeti na kila mara utajikuta kwenye ‘The Komedi’,” alisema Waziri Mkuu.

Hata hivyo, alisema atakuwa tayari kumuunga mkono mtu yeyote atakayejitokeza kuwania urais baada ya kipindi cha Rais Kikwete kumalizika.

Awali Mwenyekiti mstaafu wa CCM wa Mkoa wa Tabora, Juma Nkumba, alimwomba Mungu ampe rehema Rais Kikwete aweze kumteua tena Pinda kuwa Waziri Mkuu mara baada ya kushinda uchaguzi mkuu ujao.

Jana Waziri Mkuu alikagua bwawa na lambo la Imalamihayo ambalo linatumika kama kuogesha mifugo ya wafugaji wa eneo hilo.

Akihutubia wafugaji hao, Pinda aliwataka wapunguze idadi ya mifugo ili kufuga kisasa na kuongeza tija na faida.

Alisema wilaya ya Tabora ina ng’ombe 54,000 ambao ni wengi kulingana na eneo hilo na hivyo kuathiri malisho ya mifugo hao hatua ambayo inawafanya kukosa afya inayotakiwa.

Baadaye Waziri Mkuu alifungua sekondari ya Nkumba ambayo ni kwa ajili ya wakazi wa kata ya Uyui na ambayo inakabiliwa na uchache wa walimu, ukosefu wa maabara, umeme na maji.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga, aliwachangia wafugaji wa Imalamihayo Sh 100,000 na kutangaza kujenga kisima cha maji shuleni Nkumba, hatua ambayo wananchi katika jimbo hilo walisema angeifanya mapema bila kusubiri ujio wa Waziri Mkuu.
 
Hao wananchi walisema muda gani madai yao hayo au ni wewe tu umeamua kuwa msemaji wao ndg? maana nipo katika msafara wa waziri mkuu toka akanyage Tabora na katika shule ya Nkumba nilikuwepo sasa hayo wewe umeyatoa wapi?
 
Hao wananchi walisema muda gani madai yao hayo au ni wewe tu umeamua kuwa msemaji wao ndg? maana nipo katika msafara wa waziri mkuu toka akanyage Tabora na katika shule ya Nkumba nilikuwepo sasa hayo wewe umeyatoa wapi?

Kilimasera jibu shutuma hizo?
 
kumbe umetoa kwenye gazeti siyo? basi hayo siyo, nipo kwenye msafara na kesho tuna majumuisho ya ziara ya waziri mkuu mkoa wa tabora katika chuo cha utumishi wa UMMA uhazili saa tatu asubuhi! kama kuna ambacho ungependa kujua niulize, au umesahau wakati tunakaribia kupokea taarifa ya serikali juu ya sakata la richmond kuna magazeti yaliandika fulani kufukuzwa, fulani kuvuliwa uanachama nk mambo ambayo yamekuja thibitika baadae si kweli? so some times inabidi uwe makini na magazeti yetu ya bongo hasa katika kipindi hili tuelekeapo kwenye uchaguzi mkuu
 
hata kama angetaka wasingempa....usiniulize nani?

jibu ni mtandao wa RA, JK na EL...hao ndiyo wenye ccm yao na wenye kuamua hatima ya kisiasa....ni vigumu kukubali lakini ndiyo ukweli..
 
hata ningekuwa mimi ndo PINDA!.....siwezi kufikiria urais wakati uwaziri mkuu unanishinda
 
hata ningekuwa mimi ndo PINDA!.....siwezi kufikiria urais wakati uwaziri mkuu unanishinda

tehe tehe ina maana ukuu umemshinda??mbona naona kama anajitahidi sana!tatizo yupo ndani ya kapo lililooza!
 
Back
Top Bottom