Pinda awatemea cheche wezi


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
639,488
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 639,488 280

Pinda awatemea cheche wezi

Imeandikwa na Jasmini Shamwepu, Dodoma; Tarehe: 16th December 2010 @ 07:01

WATUMISHI wanaofanya kazi kwa malengo ya kuiba fedha za umma wametakiwa kujiengua kwenye utumishi na kutafuta kazi nyingine kwa kuwa Serikali haipo tayari kuwavumilia watu wa namna hiyo.

Aidha, watumishi katika Serikali za Mitaa watakaobainika kuwa wanafuja mali za umma wataachishwa kazi na kufunguliwa kesi.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa kauli hiyo jana alipohutubia katika Mahafali ya Pili ya Chuo cha Serikali za Mitaa kilichopo Hombolo mjini Dodoma.

Aidha, amewataka wakuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na viongozi mbalimbali kupitia ngazi ya Serikali za Mitaa kuhakikisha wanapata kozi maalumu kupitia Chuo cha Serikali za Mtaa.

Pinda alisema watumishi waliopo katika Serikali za Mitaa wengi wanafanya kazi kwa mazoea na ndiyo maana wamekuwa wakitumia fedha za umma kwa nanufaa yao binafsi badala ya kujali maslahi ya taifa.

Alisema ili watumishi wa Serikali za Mitaa wafanye kazi zao vizuri na zenye tija ni lazima wakapata elimu ya kutosha kupitia katika chuo hicho kwa maana viongozi wengi wa Serikali za Mitaa wanaingizwa kazini kwa kuteuliwa hivyo hawajui wajibu wao.

Alisema, nchi nyingi duniani zilizoendelea hufanya vizuri kutokana na watumishi wa Serikali za Mitaa kupitia katika vyuo husika na siyo kufanya kazi kwa mazoea ambayo husababisha hasara kwa taifa.

Kwa upande, Kaimu Mkuu wa Chuo, Dk. Robert Kisusu alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa ajira kwa wahitimu pamoja na uchache wa watumishi ambao ni walimu.

Dk. Kisusu alisema mbali na hilo bado kuna uhaba wa chumba cha maktaba, ukosefu wa jengo la watumishi kwa maana ofisi pamoja na mabweni ya kutosha katika kuwalaza wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho.

Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho, Ramadhani Khalifa alisema pamoja na jitihada za Serikali kuboresha masomo katika chuo hicho, lakini bado halmashauri nyingi hazijaweza kuwapeleka watendaji kupata masomo ya uendeshaji wa shughuli za halmashauri.

Alisema Tanzania ina halmashauri tatu tu zilizoonesha kuwapatia elimu watumishi katika chuo hicho na kuzitaja kuwa ni Kigoma, Kondoa na Babati.
 

Forum statistics

Threads 1,239,125
Members 476,369
Posts 29,343,429