Pinda atamani watenda maovu wasingekuwapo

P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
40,013
Likes
8,850
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
40,013 8,850 280
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema ‘kama Watanzania wote wangekuwa wacha Mungu na watenda wema, mafisadi na watenda maovu ndani ya Taifa wasingekuwapo, hivyo akawaomba viongozi wa dini nchini kuendelea kuliombea Taifa ili liondokane na hali hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka matajiri na wenye uwezo nchini pamoja na wenye fikra potofu dhidi ya walemavu, kuiona jamii ya watu hao kama binadamu wenzao hivyo wawe na moyo wa kuwasaidia na kuacha vitendo mbalimbali vikiwemo vya kuwadharau pamoja na mauaji dhidi yao.

Alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati wa tafrija ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kwa ajili ya watu wenye ulemavu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Waziri Mkuu alisema dunia kwa wale wote ambao wanaoamini, imetokana na baraka za Mungu ambapo ametofautisha maumbile mbalimbali ya binadamu kwa binadamu, wanyama kwa wanyama, matajiri na masikini ila jambo ambalo lipo sawa kwa wote ni kifo, na kushangaa kuona binadamu wengine hawana utu kwa kuwachinja wenzao kama vile kuku au mnyama mwingine yoyote.

“Jambo pekee ambalo hajatutofautisha ni kifo, hakuna cha tajiri wala masikini, sasa wakati mwingine huwa najiuliza kwa nini hawa wenzangu huwa wanataka kuwanyanyasa binadamu wenzao walioumbwa na Mungu, sisi tuliojaliwa ndiyo tulipaswa kuwa wepesi wa kuwasaidia, lakini inashangaza kuona kuwa hatuko hivyo,” alisema.

Alisema wapo watu waliojaliwa utajiri mkubwa, lakini cha kushangaza badala ya kujitolea kwa watu wenye matatizo wao wameendelea kujineemesha wao, ambapo aliwataka watu hao kufika mahali na kuwajali walemavu.

Waziri Mkuu alisema katika mwaka uliopita pekee zaidi ya matukio 48 ya mauaji ya albino yalitokea na mpaka ilifikia mahali akipigiwa simu na Mkuu wa Mkoa yeyote katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza au Kagera, alikuwa akiogopa akifikiri kwamba ni simu inayotaka kumpa taarifa ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Aidha, Pinda alisema kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kumalizia sheria kwa ajili kuwalinda walemavu ambapo hivi karibuni itapelekwa bungeni ambapo ikikamilika, itawatetea katika mambo mbalimbali japo alisema siyo kila kitu kitatekelezwa ndani ya sheria hiyo.

Kwa upande wake, Mengi alisema Watanzania wanapaswa kuonesha moyo wa huruma na upendo, kwa kuwajali wenye matatizo mbalimbali. Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu (SHIVYAWATA), Abdulrahman Lugowe, aliiomba serikali kuwasaidia kuwapa elimu bure katika ngazi zote ili wakabiliane na ugumu wa maisha na iharakishe rasimu ya sheria inayowalinda ili wapate haki zao na kusaidia kupewa mikopo ili kufanya biashara.
 
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
94
Points
0
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 94 0

- Mungu angependa Pinda atumie nafasi yake kiuongozi kuwasafisha hao watenda maovu, bdala ya kulalamika kama vile sisi wananchi wa kawaida, wakati yeye ni Waziri Mkuu wa jamhuri!

es!
 
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
476
Likes
3
Points
35
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
476 3 35
- Mungu angependa Pinda atumie nafasi yake kiuongozi kuwasafisha hao watenda maovu, bdala ya kulalamika kama vile sisi wananchi wa kawaida, wakati yeye ni Waziri Mkuu wa jamhuri!

es!
Ni kweli kabisa mkuu, huyu jamaa amezidi kulalamika tuuu, no actions. Hivi ni kweli tumuamini yeye ni msafi kama malaika?mie ameshaanza kuniboa hasa kwa statement zake za kujikosha!
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Tatizo lake Pinda hadi leo hajui kama yeye ni PM au haamini kwamba yeye ni mtendaji mkuu wa serikali anafikiri labda kuna mtendaji mwingine simply ni kama hajui wajibu wake alikuwa anafaa sana kama angekuwa kambi ya upinzani ajiunge na kina Mrema kuilalamikia serikali.
 
Forum statistics

Threads 1,250,857
Members 481,494
Posts 29,748,185