Pinda ampokea Mwenyekiti wa Bavicha aliyetimkia CCM na wanachama 233

View attachment 1050798


Mizengo Pinda ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, amewapokea wanachama wapya wa upinzani 233 akiwemo mwenyekiti wa vijana (Bavicha) Mkoa wa Manyara, Frank Oleleshwa na aliyekuwa Katibu wa Chadema wilayani Simanjiro.

Wamepatiwa kadi za CCM na Pinda katika ziara yake ya siku nane Mkoa wa Manyara.

Akizungumza leo kwa niaba ya wanachama wenzake, Oleleshwa amesema sababu za kuhamia CCM zipo nyingi ila yale aliyokuwa anapigania alipokuwa Chadema yanafanyika CCM.

"CCM imeonyesha utashi mkubwa wa uzalendo katika kuongoza nchi hivyo tumeamua kuhamia huku ili kuunga mkono juhudi hizo," amesema Oleleshwa.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi kadi wanachama hao wapya wa sehemu mbalimbali wilayani Simanjiro, Pinda aliwapongeza kwa kujiunga na CCM.

Pinda amesema hivi sasa Rais Magufuli anafanya kazi kubwa ya kufanikisha maendeleo hivyo Watanzania wanapaswa kumuunga mkono.
Hawa viongozi wastaafu wa nchi hii wanastahili kushitakiwa kwa kulihujumu taifa.
Maana kwa vinywa vyao wanashuhudia kuwa hawakuliongoza taifa hili kimaadili na weledi Bali kuliharibu na kulihujumu, na sasa magufuli anatengeneza waliyoyaharibu wao.
KATIKA MAMBO YOTE,MAGUFULI NAMPONGEZA KWA HAYA
1, HAKUNA MTANZANIA ANAYEINUA KINYWA KUDAI KATIBA MPYA
2,HAKUNA KIONGOZI MSTAAFU ANAYEFURUKUTA KUKOSOA HATA KWA SIRI
3, HAKUNA MSOMI WA BACHELOR'S, DOCTORATE WALA PROPHESOR. WOTE KUUNGA JUHUDI TU. RUBBISH.
4, HAKUNA NKAPA,MWINYI WALA JAKAYA,WOTE WAMESHIKWA NA KIHARUSI
Bashite kwa mganga ulikompeleka msukuma huyu ni KIBOKO!Hakuna duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
siasa anaruhusiwa kufanya mbunge tu wa chadema tena jimboni mwake na mwana CCM yeyote popote.
 
Back
Top Bottom