Pinda amelidanganya bunge! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda amelidanganya bunge!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dmalale, Feb 13, 2011.

 1. d

  dmalale Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  NI KWELI WAZIRI MKUU AMELIDANGANYA BUNGE

  Deusdedit Jovin

  FEBRUARI 10 mwaka huu, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari, kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Jambo hili lilitokea baada ya Mbunge wa Arusha, Godbless Lema (CHADEMA), kuomba apewe mwongozo wa spika “kuhusu utaratibu” aliohisi unakiukwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, wakati akitoa maelezo kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha Januari 5, mwaka huu.

  Pinda alizungumzia vurugu hizo za Arusha wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua serikali ina msimamo gani kuhusu mauaji ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi wakati wa vurugu hizo.

  Akijibu swali la Mbowe, Pinda alilieleza Bunge kwamba chanzo asilia cha vurugu hizo ni uamuzi wa madiwani wa CHADEMA kutokubali kushindwa katika uchaguzi wa umeya mjini Arusha, wakati “utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa”, kwa maana kwamba “Meya wa Arusha yupo kihalali.”

  Kufuatia kauli hiyo na zingine zinazofanana nayo, Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika “kuhusu utaratibu” wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na mbunge wa kawaida endapo kiongozi mkubwa wa nchi kama Waziri Mkuu amelidanganya Bunge.

  Baada ya kuombwa mwongozo huo, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, Spika Makinda alisema: “Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; waziri mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya?”

  Kisha, Spika alimpa siku tatu Lema ili awasilishe kwa maandishi utetezi wake wa kuthibitisha kwamba waziri mkuu alisema “uongo” bungeni siku hiyo.

  Katika muktadha huu, tunakusudia kufanya mambo mawili. Kwanza ni kuonyesha kwamba ni kweli kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema uongo bungeni ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

  Na pili tunataka kuonyesha kwamba, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema.

  Waziri Mkuu alisema uongo: Meya wa Arusha si halali

  Kwa lengo la kuonyesha kwamba Waziri Mkuu alisema uongo bungeni, inatosha kutoa ushahidi utakaokanusha usemi ufuatao kama ulivyotolewa naye bungeni: Kwamba, “Utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa”, kwa maana kwamba “Meya wa Arusha yupo kihalali.”

  Hapa inatosha kabisa kuonyesha kwamba miongoni mwa wajumbe waliompigia kura ya ndiyo “Meya wa Arusha”, yupo angalau mjumbe mmoja ambaye hakuwa na haki ya kisheria ya kuingia na kupiga kura hiyo. Na huyo si mwingine, bali ni Mary Pius Chatanda, ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Mkoa wa Tanga. Utetezi unafuata.

  Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya “Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) ” (Local Governments (Urban Authorities) Act) ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda atakuwa ni mjumbe mwenye sifa ya kisheria ya kupiga kura katika vikao vya Manispaa ya Arusha kama atatimiza sifa mojawapo kati ya sifa tano zifuatazo:

  Kwanza, lazima awe ni miongoni mwa madiwani ambao ni “wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(a)). Chatanda hakuwa miongoni mwa madiwani ambao ni “wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha]”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa meya wa Arusha.

  Pili, lazima awe ni “mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana” (Tazama ibara ya 19(2)(b)). Chatanda hakuwa “mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

  Tatu, lazima awe ni “Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana” na kwa mpigo awe “ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(c)). Chatanda hakuwa “Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

  Nne, lazima awe ni “Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais” na kwa mpigo awe “ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(d)). Chatanda hakuwa “Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

  Na tano, lazima awe ni miongoni mwa “wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI ambaye katika uteuzi wake [amezingatia] makundi maalumu kama vile watu wenye ujuzi maalum, watu waliotelekezwa na watu walio katika mazingira magumu.” (Tazama ibara ya 19(2)(e)). Chatanda hakuwa miongoni mwa “wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

  Hivyo basi, Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya “Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji)” ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda hakuwa na sifa yoyote ya kisheria ya kuingia katika kikao cha Manispaa ya Arusha na kupiga kura kama alivyofanya. Baraka za chama chake haziwezi na hazipaswi kubatilisha sheria za nchi.

  Tena tusifananishe uwepo wa Mary Pius Chatanda na uwepo wa Rebecca Mngodo katika kikao kilichofanya uchaguzi wa Meya wa Arusha. Kufanya hivyo ni kufananisha maembe na machungwa. Mngodo ni mbunge viti maalumu aliyepatikana kupitia mkoa wa Arusha kupitia CHADEMA. Na hatimaye alipangiwa kazi na chama chake kufanyia kazi katika Mkoa wa Arusha. Kwa hiyo alikuwa na sifa zote za kisheria za kuwemo katika kikao kile.

  Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema

  Na sasa, tuone ni kwa nini Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema. Kabla ya spika kumnyima mwongozo “kuhusu utaratibu” wa kikanuni, spika alipaswa kufanya tafakari kadhaa kuhusu Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi yetu.

  Kwanza, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(1) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni msimamizi mkuu wa shughuli zote za siku hadi siku zinazofanywa na vyombo vya dola katika Jamhuri nzima. Pili, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(2) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni “Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni”.

  Tatu, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 62(2) na 66(1) za Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni mjumbe halali katika vikao vya bunge kupitia kofia yake kama mbunge wa kuchaguliwa.

  Nne, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Waziri Mkuu (Mizengo Pinda), kama ilivyo kwa Mbunge mwingine yeyote, anapokuwa akisema bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha tu.

  Tano, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(3) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema) anaweza kusimama mahali pake na kuomba mwongozo “kuhusu utaratibu” uliokiukwa bungeni; na kwamba baada ya kuruhusiwa na Spika, anaaweza kudai kwamba, Mbunge aliyekuwa anasema kabla yake (kama vile Mizengo Pinda) ametoa maelezo ya uwongo kuhusu jambo au suala alilokuwa analisema bungeni.

  Sita, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(4) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge anayeomba mwongozo “kuhusu utaratibu” uliokiukwa bungeni (kama vile Godbless Lema alivyofanywa), atakuwa na wajibu wa kutoa na kuthibitisha ukweli kuhusu jambo au suala hilo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge.

  Saba, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(5) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika au Mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema), baada ya kutoa maelezo mafupi ya ushahidi unaotilia mashaka ya dhahiri kuhusu ukweli wa kauli juu ya jambo ambalo mbunge mwingine (kama vile Mizengo Pinda) amelisema Bungeni, anaweza kumdai Mbunge huyo (Mizengo Pinda), ambaye kauli yake inatiliwa shaka, atoe uthibitisho wa ukweli wa kauli yake na kama atashindwa kufanya hivyo, afute maelezo yake hayo.

  Nane, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(6) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha ukweli wa kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda), atawajibika kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, papo hapo au katika muda atakaopewa na Spika kwa ajili ya kufanya hivyo.

  Tisa, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(7) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda) atashindwa kufanya hivyo, anaweza kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake hayo, papo hapo au katika muda atakaokuwa amepewa na Spika kwa ajili ya kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake.

  Na kumi, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(8) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, Mbunge aliyetakiwa kutoa uthibitisho wa ukweli wa kauli yake aliyoitoa bungeni (Mizengo Pinda) atakataa au atashindwa kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, na kama atakataa kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake, basi Spika atamwadhibu kwa kumsimamisha Mbunge huyo (Mizengo Pinda) asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano.

  Hivyo ndivyo Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) zinavyosomeka. Na huu ndio mwongozo aliopaswa kuutoa Spika Makinda. Lakini, baada ya kuombwa mwongozo husika, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, akaona kwamba ombi hilo ni utovu wa “adabu” wa “hali ya juu”. Kwa maneno yake mwenyewe, Spika alisema, “Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; Waziri Mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya?” Kwa hakika, lazima hapa tukubaliane kwamba spika alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Aliombe radhi Bunge na taifa kwa ujumla.

  Simu: 0758341483/0684175182
  Email: deus.jovin@gmail.com
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Ish! Mbona unamwaga kuku kwa mchele kidogo. Haraka ya nini mbona kesho haiko mbali. Mbona habari yote imeshakuwa void kwa mwandishi kunakiri vipengele vya Sheria ambavyo havipo kwenye Sheria aliyoitaja kwani Sheria ya Serikali za Mitaa haina Ibara bali ina Vifungu.
   
 3. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama Lema atakuwa amenukuu neno ibara badala ya kifungu itakuwa imekula kwake!! kutotumia maneno sahihi katika hayo mawili kulikisababisha chama cha walimu kushindwa kesi yake dhidi ya Serikali waliokuwa wanaiomba mahakama iwaruhusu kuandamana.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  MAMA SPIKA ANNA MAKINDA, BUNGENI KUHESHIMIWE TU 'NGUVU YA HOJA'
  KWA WASHIRIKI WOTE; UMRI, VYEO NA USOMI TUKASUBIRIANE MITAANI


  Bungeni ndiko pekee mahala ambapo hata nyau tu huthubutu kumtazama moja kwa moja mfalme usoni huku mchezo ukichezwa kwa maneno mdomoni, akili kichwani na maspika wakiwa ni refasrii na washika bendera.

  Nasema bungeni ndiko mahala ambapo mchezaji wa kulipwa au kepteni kwenye timu asipokaa vizuri hulambwa chenga mara kibao na wachezaji chipukizi; wengine ambao hata majina bado hawa. Ndio!! Bunge ndio uwanja wa siasa penye mazungumzo ya kistaarabu tu (vijembe, kejeli, na mizengwe mahala pake sokoni) huku kukiw ni kwamba kinachotafutwa kwa kiasi kikubwa ni kushawishiana mwelekeo wa mambo, kuridhishana UKWELI ULIPO, na kutatwa matatizo ya jamii iliowatumeni mahala pale.

  Hivyo, hali iliojitokeza kati ya viongozi wetu Waziri Mkuu na Mbunge wa Sumbawanga na mwenzake Mbunge wa Arusha, Gdbless Lema, majuzi bungeni Dodoma, lina mengi mazuri ya kutufundisha kadri bunge letu linavyoendelea kuseheni viongozi vijana na wasomi, kuliko kuishia tu kwenye kutuhumiana UTOVU WA LABDA NIDHAMU na hata wengine kuonekana kule kwamba kila kitiririkacho toka vinywani mwao siku zote kibakia na kuendelea kuwa ni UKWELI NA UKWELI MTUPU!!!

  Tusisahau pia kwamba siku zote watu tumezingirwa na minada ya kila aina katika maisha tunayoishi. Wakati mnada wa wafanyabiashara wa mitumba ni Mchikichini kwa Makamba Dar, mnada wa nyama ni Vigunguti, Simu za Wizi pale makutano ya barabara za Independence na Makungnya, ya wambeya vijiweni, na mnada wa silaha haramu toka Rwanda ni pale Kijitonyama Breakpoint, kwao wao wanasiasa mnada wao wa kuuza na au kutetea mawazo chini ya misingi inayoeleweka ni bungeni.

  Mpaka hapo kwaza nitangulize po ngezi zangu kwa wabunge wa CHADEMA kwa namna ya pekee wanavyochangia kuweka VIWANGO VYA KIMATAIFA KATIKA UENDESHWAJI WA BUNGE LA VYAMA VINGI ambyo kwa bahati mbaya hayakuzoeleka katika nchi yetu ambayo imekwepo chini ya mfumo wa chama kimoja. Pia, kwa namna ya pekee nimpongeze Mhe Godbless Lema kwa utetezi w nguvu anaouleta bungeni dhidi ya madai ya Waziri Mkuu. Wadadisi wa mambo wanahofia kwamba endapo kutabainika kwamba Mhe Pinda alitoa majibu rahisi kwa maswali magumu basi ofisi ya spika itamchukulia hatua gani?? Jamani wabunge wa CHADEMA mko deepu saaana!! Duu, kwa mtaji wa utetezi huo sasa hapa ni patamu mnoooooooo!! Na sasa tunasubiri kweli kweli mwenendo mzima baada ya hapa tuone inavyokwenda.

  Kweli sasa bunge letu si kama enzi zao Marehemu Amran Mayagila,Komanya, Joseph Rwegasira au Fredrick Msuya ambako mbunge kazi yake ilikua ni kuingia pale mjengoni na kuanza kuchapa usingizi waka mjadala ukiendelea huku akitajwa tu jina na spika wa wakati huo, Marehemu Chifu Adam Safi kumuuliza maoni yake juu ya mjadala unaoendelea, mara utasikia mtu mzima kaibuka ndotoni na udenda ukichuruzika, na kusilibia tu jibu lolote lile kama vile 'MHESHIMIWA SPIKA NAUNGA MKONO HOJA ASILIMIA KWA MIA KAMA ILIVYOSEMWA NA MVUNGUMZAJI ALIYETANGULIA'.

  Sasa hivi kweli karibu kila mbuge, hasa wale wa upinzani ni watu ambao ni wadadisi wakubwa na wa kudadavua kweli kila nukta n kituo azungumzapo mtu bungeni na hada huku majukwaani mitaani. Ni watu ambao ni wafuatiliaji wakubwa wa mambo, WENYE NIDHAMU KUBWA KWA 'NGUVU YA HOJA' ILA WATOVU WAKUBWA WA NIDHAMU KWA 'HOJA ZA NGUVU'; hata kama hoja za aina hiyo zinashilishwa mbunge mwenye umri mkubwa kuliko Mrehemu mpendwawetu Mzee Abdalla Fundikira, mwenye usomi zaidi ya Maprofesa Sarungi, Mwakyusa au Mwandosya, au mwenye cheo kikubwa cnini kama Mhe Rostam Aziz - kinachoheshimiwa ni nguvu ya hoja tu!!

  Je mnaonaje bungeni tukazingatia zaidi heshima, adabu na unyenyeke mkubwa kwa NGUVU ZA HOJA PEKE YAKE (kwa maslahi ya wale waliotutuma bungeni kuwatetea) kama wajumbe rasmi bungeni, halafu baadaye sana tu kukaanza kuzingatia heshima, adabu na unyenyekevu mkubwa kwa umri wa mtu, elimu yake au cheo pindi tukishatoka nje ya bunge??

  Hili ni muhimu sana na lazima liwe hivyo mheshimiwa spika kwa sabu ilikuondoa hatari ya waheshimiwa wabunge kubaguana kiumri, kiusomi, na au ki-vyeo kule mjengoni, ni bora tutambue ya kwamba wangiapo ndani ya bunge la ni kazi moja tu - UWAKILISHI WA WATU WAKE WITHOUT FEAR OF FAVOUR - hivyo dira yake kuu ya kutolea heshima, adabu na unyenyekevu ni NGUVU YA HOJA TUU, ili ubunge wake kama li-taasisi linalotegemewa na wengi sana nje ya bunge liweze kufanya kazi bila vikwazo vingi. Hapo ndipo taasisi za Uwaziri Mkuu na Ubunge wa Jimbo la Arusha au nyingine yoyote itaweza kufanya kazi kwa umurua wake stahiki.

  Lakini pindi Ndugu Godbless Lema au Mr Sugu, Halima Mdee au David Kafulila anapokutana Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda aka 'Mtoto wa Mkulima' mwenzangu na mimi hapa basi hapo yale yoote heshima, adabu na unyenyekevu ZIWE MBEEELE KAMA TAI kama ilivyo ada katika jamii yetu ya ki-Tanzania, wazee kutambulika kwa kuwa wametuzaa, kisomo huingatiwa kwakuwa hutuwezesha vizuri zaidi kumudu mazingira yetu tunamoishi na vyeo vithaminiwe hasa wenye dhamana hizo wanapovitumia vizuri zaidi na kwa haki kwetu sote.

  Mwisho, heshima, adabu na unyenyekevu zote kwa pamoja ni tamu sana ilioje kwa wanaozipata kila leo na hasa pale ambapo zote hupatikana kwa hiari zaidi!!!
   
Loading...