Pinda akerwa na ‘ujeuri’ wa Barrick

Pinda akerwa na ‘ujeuri’ wa Barrick

Ukiweka viongozi wote toka ngazi ya kijiji mpaka
ngazi ya KIKWETE hakuna KIONGOZI mchovu NA mlafi kama PINDA,
pinda angekuwa muadilifu kiasi cha kubusu pete za maaskofu leo hii angekuwa ameshakabidhi barua ya kujiudhuru kwa kikwete ili kikombe hicho cha wizi wa mali za umma na kunyanyasa wananchi kimuepuke
LAKINI yeye ndiye kinara wa uongo mpaka bungeni, kisa kazawadiwa uwaziri na mwanaume mwenzie,
Yawezekana yeye binafsi haendi lakini anaendeshwa na mama TUNU ila maisha ya familia yaendele vizuri,
ndio maana inafikia hatua kwa ujinga huu huu analia mpaka mbele za waandishi wa habari kwa sababu nafsi ina msuta
 
hatuna viongozi kwa style hii maana yeye ni kiongozi analalamika je, wachini yake itakuwaje?
 
Matatizo makubwa ya uwekezaji katika nchi hii yanatokana na sera na sheria mama kuhusu uwekezaji za mwaka (1990, 1996 na 1997). Mapungufu haya yamekuzwa na viongozi na watunga sera na mikakati wetu kwa kuwekea madhanio pasi kuwa na ushahidi wa kutosha. Ukiangalia hata bajeti zetu, zinatawaliwa na generic assumptions on economic spill overs, trickle downs na other linkages baina ya uwekezaji kama huu katika madini, jamii husika na mfumo mzima wa uchumi Tanzania bila hata ya kuzingatia kwamba hivi vitu vipo au kuwa na mkakati husika wa kuhakikisha kunakuwa na hivi vitu.

Mheshimiwa Pinda alikuwa anafurahisha baraza tu. Ingependeza siku Pinda awakutanishe pamoja hawa "wawekezaji" na wahanga wa uwekezaji huo.
 
huyu mzee kweli amePinda Jairo alimshindwa...Barrick ndo ataiweza? atarudi tu aseme ingekuwa ni uwezo wake angewafukuza nchini....
 
Mbia mkubwa wa Barrick [Canada and Autralia] ni familia ya George Bush, pia kuna matajiri wakubwa ambao ni wakurugenzi kama Lord Carrington etc.Barrick wamerubuni viongozi wa nchi nyingi dunian na wana uwezo wa kumuweka au kumtoa kiongozi wa nchi kama yetu endapo atatofautiana nao kimsimamo,PM anajifaragaua,jioni akionana na Deo Mwanyika akachukua bahasha yake ndio mwisho wa story.
 
uyu pinda nae upuuzi mtupu,anaboa na matamko yake ya "kukerwa" ebu anyamaze
waziri gani butu hivi?agggrrr asitukere hapa
 
hii nchi itakapofanya mapinduzi tu,ndio tutaweza kuachana na huu ukoloni wa wazungu
yani tunataifisha rasilimali zote zilizouzwa na ccm kwa misaada ya kipuuzi sana isiyo saidia mwanainchi wa chini kbs
 
Kwanza alitakiwa awasikilize wananchi halafu awaite asiende kwao waje awaagize anayotaka baada ya kuwasikiliza wanachi, kisha kutoa taarifa kwa nchi na kufuatilia utekelezajin wa aliyo waagiza.Period, sasa yeye anasema ameomba akutane nao ajifunze chanzo cha migogoro Shame on you PM!
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameoneshwa kukerwa na jeuri inayooneshwa na uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara (Nyamongo) unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold uliopoTarime katika kuwasaidia wananchi wanaozunguka mgodi huo.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Mara baada ya kuwasili hapa, Pinda alisema pamoja na kuzungumza na uongozi wa mgodi huo, atazungumza pia na wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

Alisema matatizo na migogoro baina ya uongozi wa mgodi huo na wananchi ni moja ya sababu zilizomfanya kuomba kukutana na uongozi wa Mgodi wa Nyamongo wakati wa ziara
yake mkoani hapa.

“Hili suala la madini lina changamoto kubwa, ndio maana niliomba mwenyewe niende Nyamongo nizungumze na uongozi na wananchi, Serikali itoe tamko kuhusiana na suala hili maana haiwezekani mwekezaji anakuja na jeuri, mgodi upo katikati ya watu, yeye hataki kushirikiana nao na kila anapoelezwa anasingizia uwekezaji.

“Hatuna maana kwamba wawekezaji wawawezeshe wananchi kuwa matajiri, lakini kuna ile misaada ya kijamii ambayo ni lazima wasaidie.

Unakuta mgodi una umeme mwingi unaowatosha na kubakia wa ziada au maji, lakini mwekezaji hataki hata kuwapa kidogo wananchi wa jirani huku ni kutafuta uadui wa bila sababu,” alisema Pinda.

Alisema atakapofika katika Mgodi wa Nyamongo atafanya mazungumzo na uongozi wa mgodi na wananchi wa jirani ili kujifunza kiini cha migogoro inayotokea mara kwa mara kati ya wananchi na mgodi ili kupata ufumbuzi.

Alisema Serikali haitavumilia tena kupokea wawekezaji ambao baada ya kuwasili nchini na kuwekeza wanaanza kutoa kauli za kijeuri dhidi ya Serikali kwa kisingizio kwamba wao ni wawekezaji wanaotafuta faida.

“Hatuwezi kukubali eti kwa vile wanawajibika kwa Wizara ya Nishati na Madini, basi watu wengine wasiwaguse au kuhoji juu ya suala lolote, ni lazima faida wanayoipata isaidie kupunguza matatizo ya kimsingi kwa wananchi wa jirani,” alisema.
Uamuzi gani ametoa!!?? au kama kawaida AMELIA. kweli magamba mmechoka.
 
Hizo porojo za pinda zisizo na utekelezaji tumeshazizoea.Hawa wanahadaa wananchi akizunguka analipiwa ticket ya kwenda na kurudi ulaya na hao wawekezaji anakunja mkia.Mungu ibariki tz

Mwenzake alinunuliwa suti na wawekezaji. sijui yeye sasa anataka kaunda suti au yale mashati yake ya design ya maua maua/mawinguwingu?? Maana hawezi kupata same privilege kama za mwenye kaya.

 
Mwenzake alinunuliwa suti na wawekezaji. sijui yeye sasa anataka kaunda suti au yale mashati yake ya design ya maua maua/mawinguwingu?? Maana hawezi kupata same privilege kama za mwenye kaya.


yeye kaisha nunuliwa ni huo uwaziri mkuu, kapewa kwa masharti ya kutumika kama hivi
 
Back
Top Bottom