Pinda ajitosa sakata la gesi...

Pinda ajitosa sakata la gesi...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

JUMATATU, JANUARI 14, 2013 04:54 NA ELIZABETH HOMBO, DAR ES SALAAM


​
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amejitosa katika sakata la gesi iliyoko Mikoa ya Lindi na Mtwara na kusema kwamba gesi itawanufaisha Watanzania wote. Amesema kwamba, kujengwa kwa bomba la gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam, itakuwa ni faida kwa Watanzania wote kwa sababu umeme utakaozalishwa na gesi hiyo utasambazwa mikoa yote nchini.

Pinda alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi alipokuwa akizindua duka jipya la vifaa vya nyumbani liitwalo Beko kutoka nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa Pinda, Jiji la Dar es Salaam linachangia asilimia 80 ya pato la taifa na kwamba umeme wa uhakika unapokosekana, mapato mengi hupotea kwa kuwa shughuli za uzalishaji husimama.

"Katika suala la umeme wa uhakika tunaona suluhu pekee ni gesi ambayo sasa imepatikana Mtwara. Nawaomba watu waelewe kwamba, ujenzi wa bomba hili ni kwa faida ya wote kwa sababu tunafahamu rasilimali zinazopatikana nchini ni za Watanzania wote, hivyo wasijali wataelewa tu na tunategemea ifikapo mwaka 2015 tatizo la umeme litakuwa limekwisha.

"Tutajenga bomba hilo la gesi hapa Dar es Salaam kwa sababu ndilo jiji linalochangia uchumi wa taifa kwa zaidi ya asilimia 80, hivyo utakapokamilika tutasambaza mikoa yote nchini na kila mmoja atafaidika," alisema Waziri Mkuu Pinda.

Kauli hiyo ya Pinda imekuja huku akionyesha kuungana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyesema hivi karibuni, kwamba gesi hiyo siyo ya wananchi wa Mtwara na Lindi bali ni ya Watanzania wote.

Alisema kwamba, pamoja na kwamba baadhi ya wakazi wa mikoa hiyo hawataki gesi isafirishwe kwenda Dar es Salaam, uwepo wa gesi hiyo kutasaidia katika uendeshaji wa kiwanda kipya cha saruji kitakachojengwa mkoani Mtwara.

Pamoja na hayo, alisema wanaopinga gesi hiyo isisafirishwe kwenda Dar es Salaam hawatendi haki kwa kuwa gesi hiyo yote iliyoko ukanda wa Bahari ya Hindi, haiko Mtwara na Lindi kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

Wakati hao wakisema hayo, hivi karibuni wananchi wa Mtwara waliandamana kupinga gesi hiyo isisafirishwe kwenda Dar es Salaam kwa kuwa hawaoni sababu ya kufanya hivyo.

Wakati huo huo, katika mazungumzo yake juzi, Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara nchini kuwa wabunifu kama wafanyabiashara wa nchi nyingine ili nao waweze kuwekeza nchi za nje.

"Leo tumezindua duka hili la vifaa vya nyumbani kama televisheni, friji, feni na vingine vingi ambavyo vinatoka nchi ya Uturuki na hii ni moja ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaoanzia mwaka 2011/2012- 2015/2016.

"Kampuni hii ya Beko Granding ni moja ya kampuni kubwa za Kituruki za uzalishaji vifaa vya nyumbani vya kielektroniki na sehemu ya kampuni kubwa za Kituruki yenye umaarufu mkubwa duniani,'' alisema Pinda.

Naye Mwenyekiti wa Modern Holdings, wasambazaji pekee Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki wa bidhaa za Beko Granding, Anselm Minja, alisema ufunguzi wa maduka hayo ya vifaa vya Beko kutoka Uturuki itakuwa mwendelezo wa ufunguzi wa maduka mengine kwa kuwa Machi mwaka huu, maduka mengine yatafunguliwa Arusha, Mbeya, Mwanza na Dodoma.

 
Well Wananchi wa MTWARA hawajasema kuwa GASI ni yao tuuu... Wao hawataki hilo BOMBA kwenda DAR...
Serikali isipindishe MATAKWA ya WANANCHI wa MTWARA; hapo ndipo UNAJUA VIONGOZI wa sasa wa CCM hawana LEADERSHIP SKILLS... Ni kuparang'anyia UMBEA na UNAFSI...
 
Hana jipya,ajibu hoja za wananchi wa Mtwara!
 
Well Wananchi wa MTWARA hawajasema kuwa GASI ni yao tuuu... Wao hawataki hilo BOMBA kwenda DAR...
Serikali isipindishe MATAKWA ya WANANCHI wa MTWARA; hapo ndipo UNAJUA VIONGOZI wa sasa wa CCM hawana LEADERSHIP SKILLS... Ni kuparang'anyia UMBEA na UNAFSI...
Hivi hiyo haiwezi kuwafaidisha Watanzania wote kwa kuanzia na kutokea Mtwara mpaka walazimishe kufikisha Dar tu?

Majitu mengine bwana Ntwara Tandika Nchale Mafichadi ya Gechi yenu....Sura mbaya na akili mbayaaaaaaaaaa!!!!
 
Jamani hivi hapo ndiyo umefikia MWISHO wa kufikiri wa SERIKALI NZIMA ya CCM. Nani kasema wananchi wa Mtwara wanasema gesi ni yao peke yao. Wananchi wa Mtwara wanachotaka ni kuona mitambo ya ku-process gas inajengwa hapo Mtwara, mtambo wa kuzalisha umeme kwa gas unajengwa Mtwara na baadaye kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

In short wananchi wa Mtwara wanataka kufahamu watafaidikaje na rasilimali ya ges iliyopatikana katika mkoa wao. Hawajasema gas ya Mtwara ni yao peke yao. Kweli serikali nzima imeshindwa kutoa jibu la swali hilo imebaki na huu ubabaishaji kwamba rasilimali ni za Watanzania wote. Those are political rhetorics of STONE AGE.
 
jamani nmakonde chi mutu, tukikachilika tatandika nchale voohe
 
Kwani wakizalisha na kutengeneza kiwanda kule na kisha kuunganisha umeme unaozalishwa kule kwenye grid kuna tofauti gani jaman?
Kutokutokea kwa mtu wa serikalini kupinga hii kitu kunaonyesha ni jinsi gani serikali inavyowahadaa watu kwenye hili suala. Yaani inshort wamejipanga.
 
pinda lile la mauaji ya albino lilimshinda hili ataweza?hili gumu litampinda.
 
naona wanaendeleza sarakasi za maneno tuh,
mwishowe mbivu na mbichi itapatikana tuh.
 
huyu Pinda ni ******* sana huyu yaani waziri mkuu mzima unaenda kuzindua duka na diwani na meya watafanya nini? jamaa mbona wanakaba sana hawa?

eti kufungua maduka ni mpango wa maendeleo wa miaka mitano? hivi hajui hapo anaendelea kuongeza trade deficit? mm nirifikir angeshawishi hao jamaa waje wawekeze hata kakiwanda ka kuassemble tv tu


Sijui Watanzania tulimkosea nini Mungu.......... hakuna kiongozi anyeweza kuzungumza Bongo mpaka ukasema "Yes, now we have a leader" .................. kila mtu ni kupiga bah blah tu. Imagine mpaka mMaprof. ambao tena walikuwa na madaraka makubwa kama akina Tibaijuka, huy wa sasa Muhongo...... hawawezi hata kutupa kitu kipya watz. Nafikiri hata huyo Mahiga anayesifiwa humu kila siku kama atarudi na kuingia kwenye siasa kwa kupitia CCM ................ itakuwa same story!!
 
napata tabu sana ninapomsikia rais jk anasema kuwa wananchi wa mtwara wajiandae kufaidika na gesi how??

Faida moja kubwa inayoweza kupatikana na uzalishaji wa gesi ni ajira ajira ajira ajira. ndiyo kitu pekee kinachoweza
kubadilisha maisha ya watu wakaona hali imebadilika.

ukijenga shule nzuri wataweza kulipia ada za watoto wao
ukijenga hospital wataweza kulipia hospitali na kununua dawa.
uijenga barabara wataweza kununua gari ya kupita kwy barabara hizo.

Bila ajira hayo yote hapo hayatawezekana na gesi itapita kama yalivyopita madini huko mwanza na watu wakaachwa na
mashimo makubwa lakini hakuna faida faida iliyopatikana.
 
viongozi wa serikali hawataki kubadilika hata kama ukweli wanaujua!!!!!wanakera kwakweli ina maana umeme ukizalishwa mtwara hauwezi kuwafikia watanzania wote??inaelekea kwa viongozi wa serikali vitu ili viwafikie wananchi ni lazima vifike dar es salaam!!!kwa hali hii hamuwathamini wananchi wenu hata kidogo na mnadhani kila mnachokiamua ni sahihi..........duh!ni aina gani ya uongozi ambao mnatuonesha wananchi???acheni kuwa static nyie lazima mubadilike na siku ambayo watanzania watasema baaaaaaaaaaaaaaaaasi naomba muwe hai ili mushuhudie nini kitatokea ianakera sana kuona wasomi tunatumia elimu zetu kuyanyanyasa mawazo na maoni ya wananchi alafu tunajinyenyekeza kipindi cha kuomba kura na kuhitaji ata kuwa karibu nao "mungu tazama raia wako"

 
Kaptura aliyovalishwa Pinda haimtoshi,inawezekana inambana au inampwaya. Kwahiyo anataka kutuambia kuwa mitambo ya kufua umeme ikijengwa Mtwara na kisha umeme ukasafirishwa kwenda huko Dar haitakuwa na manufaa kwa watanzania? Na siyo kweli kuwa watu wa Mtwara wanakataza gesi isiende Dar. ACHA KUPOTOSHA UKWELI.
 
Waziri Mkuu anazindua duka la 'kisasa' la vifaa vya nyumbani????? Haki ya Mungu Tanzania kuna kitu tumemkosea Mungu, si bure. Waziri Mkuu anazindua duka la vifaa vya ndani????? Sikubaliani na udhaifu huu. Hii ni rushwa. Tunapaswa kuelezwa alipewa seti ngapi? Je, zawadi wanazopewa ambazo zinazidi thamani ya Sh 50,000 wanaziwasilisha kwenye Tume ya Maadili kama sheria inavyoagiza?

Manyerere Jackton
Dar es Salaam
 
Waziri Mkuu anazindua duka la 'kisasa' la vifaa vya nyumbani????? Haki ya Mungu Tanzania kuna kitu tumemkosea Mungu, si bure. Waziri Mkuu anazindua duka la vifaa vya ndani????? Sikubaliani na udhaifu huu. Hii ni rushwa. Tunapaswa kuelezwa alipewa seti ngapi? Je, zawadi wanazopewa ambazo zinazidi thamani ya Sh 50,000 wanaziwasilisha kwenye Tume ya Maadili kama sheria inavyoagiza?

Manyerere Jackton
Dar es Salaam

Mimi namalizia duka langu la chupi na sidiria, mkuu wa kaya ndo atakuja kulizindua.
 
Kila mtu anataka kuonekana kwenye TV. Biashara ya kuuza sura! Hopeless bunch of the so called leaders!
Kaptura aliyovalishwa Pinda haimtoshi,inawezekana inambana au inampwaya. Kwahiyo anataka kutuambia kuwa mitambo ya kufua umeme ikijengwa Mtwara na kisha umeme ukasafirishwa kwenda huko Dar haitakuwa na manufaa kwa watanzania? Na siyo kweli kuwa watu wa Mtwara wanakataza gesi isiende Dar. ACHA KUPOTOSHA UKWELI.
 
Anashindana na Raisi Kikwete - alikuwa Nzega juzijuzi, hana kazi ya kufanya Ofisini, anajimuvuzisha!
Waziri Mkuu anazindua duka la 'kisasa' la vifaa vya nyumbani????? Haki ya Mungu Tanzania kuna kitu tumemkosea Mungu, si bure. Waziri Mkuu anazindua duka la vifaa vya ndani????? Sikubaliani na udhaifu huu. Hii ni rushwa. Tunapaswa kuelezwa alipewa seti ngapi? Je, zawadi wanazopewa ambazo zinazidi thamani ya Sh 50,000 wanaziwasilisha kwenye Tume ya Maadili kama sheria inavyoagiza?

Manyerere Jackton
Dar es Salaam
 
Total empty, they don't have any idea to create number of people gainfully
for the employment, especially Mtwara/Lindi regions. Where are living in
poorish life, this deep south of Tanzania,why not became a Central Natural
Gas Processing Plant and (Turbine) Gas Electricity Power Plant.
These matters remain in doubt. Because when you say Development, others
are in the Deal program.
 
Dar inachangia 80% ya mapato kwa kuwa imewezeshwa kufanya hivyo.
Hata mtwara wanataka kuchangia pato la taifa vile vile.
Nadhani ruzuku kubwa itaenda dar badala ya mtwara tukitumia mantiki hii ya kina Pinda.
 
Back
Top Bottom