Pinda ajitosa sakata la gesi...

Pinda ajitosa sakata la gesi...


JUMATATU, JANUARI 14, 2013 04:54 NA ELIZABETH HOMBO, DAR ES SALAAM

“Leo tumezindua duka hili la vifaa vya nyumbani kama televisheni, friji, feni na vingine vingi ambavyo vinatoka nchi ya Uturuki na hii ni moja ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaoanzia mwaka 2011/2012- 2015/2016.

“Kampuni hii ya Beko Granding ni moja ya kampuni kubwa za Kituruki za uzalishaji vifaa vya nyumbani vya kielektroniki na sehemu ya kampuni kubwa za Kituruki yenye umaarufu mkubwa duniani,’’ alisema Pinda.


Kuifanya Tanzania soko la Uturuki ni mpango wa maendeleo wa CCM !!!??
Na sisi tunauza nini huko ?
 
QUOTE=Mzee wa Kwembe-Kati;5452119]Waziri Mkuu anazindua duka la 'kisasa' la vifaa vya nyumbani????? Haki ya Mungu Tanzania kuna kitu tumemkosea Mungu, si bure. Waziri Mkuu anazindua duka la vifaa vya ndani????? Sikubaliani na udhaifu huu. Hii ni rushwa. Tunapaswa kuelezwa alipewa seti ngapi? Je, zawadi wanazopewa ambazo zinazidi thamani ya Sh 50,000 wanaziwasilisha kwenye Tume ya Maadili kama sheria inavyoagiza?

Manyerere Jackton
Dar es Salaam[/QUOTE]Kwakweli imefika kipindi viongozi wa ngazi za juu wawe makini na mialiko maana mingine haileti taswira nzuri kwa jamii.
 
Hivi huyu is alienda Korea kwa fadhila za wabrazil wa Pertro.as ? Alienda yeye na Mkewe nanina wasiwasi lazima atakuwa anakaunti Uswiss.
 
kuna siri gani hapa kati mbona wanang'ang'ania 2 ges kwenda dar mbona hawa 2ambii gesi ikienda dar faida zake ni hizi na ikizalisha umeme mtwara bila kufika dar taifa litapata asara kiasi hichi au ndiyo yale ya 10% mchina ameshatoa ndiyo maana wana mumunya maneno yote wamekaririshana hakuna mwenye hoja mpya.
 

JUMATATU, JANUARI 14, 2013 04:54 NA ELIZABETH HOMBO, DAR ES SALAAM


​
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amejitosa katika sakata la gesi iliyoko Mikoa ya Lindi na Mtwara na kusema kwamba gesi itawanufaisha Watanzania wote. Amesema kwamba, kujengwa kwa bomba la gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam, itakuwa ni faida kwa Watanzania wote kwa sababu umeme utakaozalishwa na gesi hiyo utasambazwa mikoa yote nchini.

Pinda alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi alipokuwa akizindua duka jipya la vifaa vya nyumbani liitwalo Beko kutoka nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa Pinda, Jiji la Dar es Salaam linachangia asilimia 80 ya pato la taifa na kwamba umeme wa uhakika unapokosekana, mapato mengi hupotea kwa kuwa shughuli za uzalishaji husimama.

"Katika suala la umeme wa uhakika tunaona suluhu pekee ni gesi ambayo sasa imepatikana Mtwara. Nawaomba watu waelewe kwamba, ujenzi wa bomba hili ni kwa faida ya wote kwa sababu tunafahamu rasilimali zinazopatikana nchini ni za Watanzania wote, hivyo wasijali wataelewa tu na tunategemea ifikapo mwaka 2015 tatizo la umeme litakuwa limekwisha.

"Tutajenga bomba hilo la gesi hapa Dar es Salaam kwa sababu ndilo jiji linalochangia uchumi wa taifa kwa zaidi ya asilimia 80, hivyo utakapokamilika tutasambaza mikoa yote nchini na kila mmoja atafaidika," alisema Waziri Mkuu Pinda.

Kauli hiyo ya Pinda imekuja huku akionyesha kuungana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyesema hivi karibuni, kwamba gesi hiyo siyo ya wananchi wa Mtwara na Lindi bali ni ya Watanzania wote.

Alisema kwamba, pamoja na kwamba baadhi ya wakazi wa mikoa hiyo hawataki gesi isafirishwe kwenda Dar es Salaam, uwepo wa gesi hiyo kutasaidia katika uendeshaji wa kiwanda kipya cha saruji kitakachojengwa mkoani Mtwara.

Pamoja na hayo, alisema wanaopinga gesi hiyo isisafirishwe kwenda Dar es Salaam hawatendi haki kwa kuwa gesi hiyo yote iliyoko ukanda wa Bahari ya Hindi, haiko Mtwara na Lindi kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

Wakati hao wakisema hayo, hivi karibuni wananchi wa Mtwara waliandamana kupinga gesi hiyo isisafirishwe kwenda Dar es Salaam kwa kuwa hawaoni sababu ya kufanya hivyo.

Wakati huo huo, katika mazungumzo yake juzi, Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara nchini kuwa wabunifu kama wafanyabiashara wa nchi nyingine ili nao waweze kuwekeza nchi za nje.

"Leo tumezindua duka hili la vifaa vya nyumbani kama televisheni, friji, feni na vingine vingi ambavyo vinatoka nchi ya Uturuki na hii ni moja ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaoanzia mwaka 2011/2012- 2015/2016.

"Kampuni hii ya Beko Granding ni moja ya kampuni kubwa za Kituruki za uzalishaji vifaa vya nyumbani vya kielektroniki na sehemu ya kampuni kubwa za Kituruki yenye umaarufu mkubwa duniani,'' alisema Pinda.

Naye Mwenyekiti wa Modern Holdings, wasambazaji pekee Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki wa bidhaa za Beko Granding, Anselm Minja, alisema ufunguzi wa maduka hayo ya vifaa vya Beko kutoka Uturuki itakuwa mwendelezo wa ufunguzi wa maduka mengine kwa kuwa Machi mwaka huu, maduka mengine yatafunguliwa Arusha, Mbeya, Mwanza na Dodoma.

kwa nini maneno hayo wanaongea wakiwa Dar, wakienda kuyaongelea Mtwara waakikishe wanakuwa chini ya polisi wa kutosha vinginevyo, nchale
 
Jamani hivi hapo ndiyo umefikia MWISHO wa kufikiri wa SERIKALI NZIMA ya CCM. Nani kasema wananchi wa Mtwara wanasema gesi ni yao peke yao. Wananchi wa Mtwara wanachotaka ni kuona mitambo ya ku-process gas inajengwa hapo Mtwara, mtambo wa kuzalisha umeme kwa gas unajengwa Mtwara na baadaye kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

In short wananchi wa Mtwara wanataka kufahamu watafaidikaje na rasilimali ya ges iliyopatikana katika mkoa wao. Hawajasema gas ya Mtwara ni yao peke yao. Kweli serikali nzima imeshindwa kutoa jibu la swali hilo imebaki na huu ubabaishaji kwamba rasilimali ni za Watanzania wote. Those are political rhetorics of STONE AGE.

Hawa watu wameamua kwa makusudi kuyapinda madai ya wana wa KUSINI , ili watimize lengo lao la kupiga hela kwenye huo mradi na si vinginevyo. NI DILI TU YA PESA NDO INAWATOA MAPOVU WOTE HATA WANASHINDWA KUTOA MAJBU MUAFAKA KWA MADAI YA WANA KUSINI.

Kama moja ya lengo la kuipeleka gesi hiyo Dar ni kuzalisha umeme kwa nini hiyo mitmbo isijengwe hukohuko inakopatikana gesi?
 
Kweli nimeamini vongozi wetu wanajulikana bei zao na hata sio wa ghali.Eeeeh!amezindua duka la vifaa vya nyumbani?Sasa nani atumie hizo fridge,microwave,blander nk?Umeme U-wapi kwenye hizi nyumba zetu za mbavu za mbwa???
 
Viongozi wa serikali hawaelewi mipaka ya nchi hata mikoa yetu ndiomaana issue ya Malawi haiishi!!Serikali itueleze hii gesi kama haipo mtwara iko mkoa gani au nchi gani?maana inaonekana wanataka kutwambi haipo Tanzania bali eneo lisilo na mwenyewe baharini (no mansland)

JUMATATU, JANUARI 14, 2013 04:54 NA ELIZABETH HOMBO, DAR ES SALAAM


​
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amejitosa katika sakata la gesi iliyoko Mikoa ya Lindi na Mtwara na kusema kwamba gesi itawanufaisha Watanzania wote. Amesema kwamba, kujengwa kwa bomba la gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam, itakuwa ni faida kwa Watanzania wote kwa sababu umeme utakaozalishwa na gesi hiyo utasambazwa mikoa yote nchini.

Pinda alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi alipokuwa akizindua duka jipya la vifaa vya nyumbani liitwalo Beko kutoka nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa Pinda, Jiji la Dar es Salaam linachangia asilimia 80 ya pato la taifa na kwamba umeme wa uhakika unapokosekana, mapato mengi hupotea kwa kuwa shughuli za uzalishaji husimama.

“Katika suala la umeme wa uhakika tunaona suluhu pekee ni gesi ambayo sasa imepatikana Mtwara. Nawaomba watu waelewe kwamba, ujenzi wa bomba hili ni kwa faida ya wote kwa sababu tunafahamu rasilimali zinazopatikana nchini ni za Watanzania wote, hivyo wasijali wataelewa tu na tunategemea ifikapo mwaka 2015 tatizo la umeme litakuwa limekwisha.

“Tutajenga bomba hilo la gesi hapa Dar es Salaam kwa sababu ndilo jiji linalochangia uchumi wa taifa kwa zaidi ya asilimia 80, hivyo utakapokamilika tutasambaza mikoa yote nchini na kila mmoja atafaidika,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Kauli hiyo ya Pinda imekuja huku akionyesha kuungana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyesema hivi karibuni, kwamba gesi hiyo siyo ya wananchi wa Mtwara na Lindi bali ni ya Watanzania wote.

Alisema kwamba, pamoja na kwamba baadhi ya wakazi wa mikoa hiyo hawataki gesi isafirishwe kwenda Dar es Salaam, uwepo wa gesi hiyo kutasaidia katika uendeshaji wa kiwanda kipya cha saruji kitakachojengwa mkoani Mtwara.

Pamoja na hayo, alisema wanaopinga gesi hiyo isisafirishwe kwenda Dar es Salaam hawatendi haki kwa kuwa gesi hiyo yote iliyoko ukanda wa Bahari ya Hindi, haiko Mtwara na Lindi kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

Wakati hao wakisema hayo, hivi karibuni wananchi wa Mtwara waliandamana kupinga gesi hiyo isisafirishwe kwenda Dar es Salaam kwa kuwa hawaoni sababu ya kufanya hivyo.

Wakati huo huo, katika mazungumzo yake juzi, Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara nchini kuwa wabunifu kama wafanyabiashara wa nchi nyingine ili nao waweze kuwekeza nchi za nje.

“Leo tumezindua duka hili la vifaa vya nyumbani kama televisheni, friji, feni na vingine vingi ambavyo vinatoka nchi ya Uturuki na hii ni moja ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaoanzia mwaka 2011/2012- 2015/2016.

“Kampuni hii ya Beko Granding ni moja ya kampuni kubwa za Kituruki za uzalishaji vifaa vya nyumbani vya kielektroniki na sehemu ya kampuni kubwa za Kituruki yenye umaarufu mkubwa duniani,’’ alisema Pinda.

Naye Mwenyekiti wa Modern Holdings, wasambazaji pekee Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki wa bidhaa za Beko Granding, Anselm Minja, alisema ufunguzi wa maduka hayo ya vifaa vya Beko kutoka Uturuki itakuwa mwendelezo wa ufunguzi wa maduka mengine kwa kuwa Machi mwaka huu, maduka mengine yatafunguliwa Arusha, Mbeya, Mwanza na Dodoma.

 
Huyu Pinda kwa muda amekuwa mstari wa mbele kuinua Katavi, leo anazungumza masuala ya mtwara, "Nyani haoni--------"
 
Back
Top Bottom