Pinda abeba changamoto, Engusero Sekondari

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
450
225
Pinda abeba changamoto, Engusero Sekondari

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Mhe Mizengo Kayanza Peter Pinda na Waziri Mkuu mstaafu amesema, changamoto zinazowakabili wanafunzi shule ya Sekondari Engusero Wilayani Kiteto Mkoani Manyara atazitatua.

Kwa suala la maji wanafunzi hao wanakunywa maji ambayo sio safi na salama, kwa kuchota kwenye visima vya asili ambayo pia ni machache na pia yana chumvi nyingi.

Shule ya Sekondari ya Engusero ina jumla ya wanafunzi 1050, ambao ni kidato cha kwanza mpaka sita na kwamba uhaba huo wa maji safi na salama shuleni unachangia kushuka kwa kiwango cha elimu.

Akiwasilisha lalamiko hilo Diwani wa Kata ya Engusero, Solomoni Mbulunyuku alisema pamoja na jitihada za Serikali bado adha hiyo ni kubwa, huku Norascko Mtewele (mwanafunzi) wa kidato cha sita akisema baadhi ya wanafunzi wanakata tamaa kuendelea na masomo.

Mhe Pinda aliwahakikishia wanafunzi hao kuwa nafasi yake aliyonayo atashawishi uongozi wa serikali shule hiyo kupata maji safi na salama

Pia alizindua bweni lililojengwa na Halmashauri la wasichana lililopewa jina SAMIA SULUHU HASSANI, lenye uwezo wa wanafunzi 84 la thamani ya mil 86.4

Mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom