Truth guy.
JF-Expert Member
- Oct 30, 2013
- 396
- 196
Nilitafuta sehemu yenye kichaka nikijificha,ule mwanga mkali wa gari ulizidi kukaribia mahali nilipokuwepo,niliomba sana ili wasiweze kuniona,maana sikujua lile gari lilikuwa ni la watu gani,dakika 3 baadae niliweza kushuhudia lile gari likipita karibu yangu kabisa,pikipiki nilikuwa nimeilaza kwenye majani,na kwa rangi yake nyeusi haikuwa rahisi kuonekana na taa za lile gari,mapigo ya moyo yalienda mbio sana mara lile gari lilipofika karibu yangu kabisa,likiwa umbali wa mita kama 20 tu kutoka ktk kichaka nilichokuwa nimejificha,"Mungu wangu,mkojo ulipenya kwenye nguo yangu ya ndani,"nikapata mshtuko usio wa kawaida,ambao tangu nikiwa ktk sekeseke hilo la kuokoa roho yangu sikuwahi kuupata,sikia tu mtu akusimulie,usiombe yakupate,lile gari,lilikuwa ni gari la kijeshi,lilikuwa kubwa mfano wa fuso,ndani yake niliona wanajeshi wengi wakiwa na silaha nzito za kivita,nilibahatika kumuona vyema mmoja wao akiwa na bunduki yenye mkanda wa risasi,na begani kwake paliandikwa 'RWANDA' katikati ya bendera iliyo..........