Pigo Serikali za Mitaa

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,072
20,451
ASILIMIA kumi ambayo serikali za mitaa huwa wanaidai hasa maeneo ya mijini baada ya wahusika kuwa wameuziana nyumba au kiwanja. Nikasema wazi kabisa bila kungata meno kuwa hiyo pesa iitwayo asilimia kumi au pesa nyingine yoyote mtu atakayolipa serikali za mitaa eti kwakuwa amenunua au ameuza eneo lake ni rushwa. Na leo nakumbusha na kusisitiza tena kuwa Watanzana wajue ukitoa pesa ile umetoa rushwa na huyo kiongozi wa serikali za mitaa uliyempa amepokea rushwa kwakuwa malipo hayo hayatambuliwi na hayaainishwi na sheria yoyote. Lazima ifike hatua haya mambo yaeleweke. Pia nimetahadharisha mara nyingi kuhusu umakini unaponunua kiwanja/nyumba na kueleza baadhi ya mambo ambayo ukiyafanya utakuwa umefanya manunuzi salama na utakuwa umeepuka migogoro na hata mgogoro ukitokea wewe hautapoteza.

Uhalali kisheria wa serikali za mitaa kusimamia mikataba.

( a ) KISHERIA HAIRUHUSIWI SERIKALI ZA MITAA KUSIMAMIA MAUZO YA NYUMBA/KIWANJA.

Kwanza nataka nieleweke wazi kuwa nazungumzia sana ununuzi wa nyumba /viwanja kwa kuona huruma jinsi watu wanavyopoteza umiliki wa maeneo yao waliyonunua kwa kuamini wameyanunua kihalali kumbe kuna nukta walizokosea katika taratibu za kimanunuzi na sasa zinawagharimu. Ninayosema hapo yanatokea karibia kila siku mahakamani. Watu wanalia lakini mda huo huna wa kumlilia.Nianze hivi kisheria Wakili ndio mtu ambaye anaruhusiwa kusimamia mkataba . Wakili ana vyeo vitatu, kwanza ni wakili, pili mthibitishaji wa umma ( notary public) tatu ni afisa wa viapo. Uwakili nao ni cheo katika vyeo alivyonavyo wakili. Vyeo viwili yaani uwakili na uthibitishaji wa umma ndivyo humpa mamlaka ya kusimamia mikataba. Hapa naongelea nyumba/viwanja lakini kimsingi vyeo hivi si tu humpa mamlaka ya kusimamia mikataba ya viwanja/nyumba lakini pia mikataba yote. Hakuna katka nchi hii sheria yoyote ambayo imemruhusu kiongozi wa serikali za mitaa kusimamia mkataba, uwe wa nyumba, mkopo au wowote ule hata wa mauzo ya baiskeli. Kama hakuna sheria hiyo maana yake ni kuwa kusimamia mikataba si kazi yao. Kwa maana hii hii narudia kusema na kusistiza kuwa hairuhusiwi serikali za mitaa kusimamia mauzo ya nyumba/kiwanja.

( b ) MKATABA WANGU WA MANUNUZI YA NYUMBA/KIWANJA UMESIMAMIWA NA SERIKALI ZA MITAA JE UNA HADHI GANI?.

Kama ndani kwako una mkataba wa manunuzi ya nyumba/kiwanja ambao ulisimamiwa na serikali za mitaa basi ujue kuwa mkataba huo hadhi yake ni sawa na umesimamiwa na jirani yako , ndugu yako au mtu mwingine yeyote unayemuamini ambaye amekusaidia kukamilisha mkataba. Tuache kuishi kwa mazoea hii ndiyo hali halisi kisheria. Mkataba wa mauzo ya nyumba/viwanja au mkataba mwingine wowote uliofanyika serikali za mitaa ni sawa na mkataba uliofanyika nyumbani kwako. Hiyo ndio hadhi au nafasi ya mkataba wa aina hiyo kisheria. Kiongozi yeyote wa serikali za mitaa anaweza kuwa shahidi yako ukiamua kumuita lakini lazima ujue kuwa ushahidi wake katika mkataba wako kisheria ni sawa na ushahidi wa mtu mwingine yeyote. Hakuna eti kwakuwa huyu au hawa ni serikali za mitaa kwahiyo wakionekana katika mkataba wangu ndio utakuwa na uzito na wenye kuaminika zaidi, hapana. Hawa kama utaamua kuwashirikisha maana hata kuwashirikisha nayo ni hiari yako wanaweza kuwa mashahidi sawa na shahidi ndugu yako au jamaa yako mwingine yeyote . Anayeufanya mkataba kuwa na uzito mbele ya macho ya sheria ni wakili na huyu ndiye aliyepewa kazi hii. Kwa hiyo wanunuzi wa viwanja/nyumba jihadharini kwakuwa serikali za mitaa kisheria hilo si jukumu lao. Wanayo majukumu yao lakini hili si miongoni mwa hayo. Watu wasifanyiwe utapeli serikali haisimamii mikataba ya watu binafsi. Kama serikali kuu haiwezi kusimamia mkataba kati Bakhresa na Mohammed enterprise hata serikali za mitaa hawezi kusimamia mkataba kati yangu na wewe. Nawatahadharisha zaidi wanunuzi kwakuwa upande wa ununuzi ndio upande wa kupoteza linapotokea tatizo.

( c ) USHAURI KWA WANUNUZI WA NYUMBA/VIWANJA.

Kama unataka kununua nyumba/kiwanja na unataka mkataba wako wa manunuzi uwe na nguvu na hadhi ya usimamizi wa kisheria basi epuka kuwatumia serikali za mitaa kufanya jambo hili. Serikali za mitaa wanajua vyema kuwa kusimamia mikataba ya kuuza na kunuua si katika majukumu yao isipokuwa kwakuwa hapa ndipo penye hela kuliko hata hizo posho zao wanazopewa na serikali kuu basi hawako tayari kulisema hili kwa mtu yeyote. Hili utakuja kulijua vyema ukishapata mgogoro wakati wao hawapo tena wameshaondoka na chao. Mikataba ya serikali za mitaa haina hadhi na wanasheria wanaichallenge sana mahakamani wakati wa migogoro kiasi cha kuonekana kama vile pengine hukufanya mkataba kabisa. Migogoro ya nyumba na viwanja ni mingi mno lakini wewe unaweza kuiepuka migogoro hiyo ikiwa utazingatia ushauri wa kitaalam na utaepuka kukurupuka unapotaka kununua kiwanja/nyumba. Leo nilitaka nikuhadharishe na hilo ndugu mpendwa.

MKATABA WOWOTE WA MANUNUZI KWA SASA LAZMA UPEWE NA RISITI YA EFD, NENDA KWA WAKILI, WACHANA NA KUGONGA MUHURI KWA HAKIMU, MDANDISHI WA UMMA, MTENDAJI WA MTAA/KIJIJI, NA WANASHERIA WA SERIKALI/SOLICITOR.

KUNATABIA YA WANASHERIA WA SERIKALI HASA MANISAPA NA MIJI KUANDIKA NA KUGONGESHA MIHURI YA SERIKALI KWA MASLAHI YAO BINAFSI, TAKUKURU WAWAKAMATE KWA MATUMIZI MABAYA YA MALI ZA UMMA.

HUWEZI TUMIA WINO, RIM NA KALAMU YA SERIKALI KWA KUJIINGIZIA KIPATO BINAFSI, MSISUBIRI MPAKA MAGUFULI AJE KUFUKUNYUA HUKO, WACHENI.

MAWAKILI WA MANISPAA, STATE ATTORNEYS NA LEGAL OFFICERS KWENYE mashirika ya umma, mfano pale TPA./BANDARI dar kuna mawakili wanamiliki law firms zao, wanashinda mitaani kwenye kesi binafsi huku za shirika zikiozea huko mahakamani, Mtukufu jpm, naomba utumie TISS,PCCB, haichukui siku moja na sisi wanyonge tutakutajia.

Mawakili wa serikali ndio wanatumika kuwaanddalia rufaa majambazi, ndio wanawaambia kitu cha kuzungumza mahakamani,
MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959
 
saf kabisa, natamani huu ujumbe ningeupata niusevu kweny email yangu,
 
Hata mwandishi uma kumbe naye hana uhalali? mbona hapa Arusha Ngarenaro jamaa anapiga ile mbaya?
 
Mwisho wa bandiko lako umeonyesha wivu wa dhati kwa wengine wanaojipatia extra income kutokana na fani zao. So inawezekana umesukumwa na wivu huo kuleta huu uzi kwa kisingizio cha kutoa elimu
 
Je 5000/- ya kublashi kiatu kwa matrafiki ambayo Jiwe aliipitisha yenyewe itakuwaje. Na pia hao viongozi wa mitaa hawana mshahara hio ndio posho ya uongozi wao
 
Suala la ARDHI kwa ujumla ni BOMU NA NI JANGA LA KITAIFA. Hakuna sheria ya ARDHI iliyo imara na inawafaa wananchi, ukizingatia mazingira ya wananchi hasa wa vijijini.

Hizi sheria zinafaa mijini (takriban 40% ya watanzania)tu ambako kuna wanasheria n.k, huku asilimia 60 ya Watanzania hata siku moja sheria hizi hazitawafaa kwa vile wahusika hawawezi kufika huko wakaangalia mauziano ya ARDHI kati ya eneo langu na mhitaji.

Nitakupa mfano mwepesi katika wizara ya AFYA unaolingana na huu wa wizara ya ARDHI: Fikiria wizara ya AFYA ipitishe sheria kuwa mja mzito kuzalia nyumbani ni marufuku, wajawazito wote wakajifungulie zahanati au hospitali. Halafu huko waliko zahanati wala hospitali hakuna. Sheria hii itakuwa mfu.

Kimsingi matatizo tulioachiwa na Nyerere kuhusu sheria za ARDHI , ndio zinazotutesha mpaka leo. Kila serikali toka Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hta sasa hivi wanaogopa kufanya marekebisho yenye tija kwa wananchi. Beuracracy ya kisheria imejaa katika wizara hii.

Japo waziri wa ARDHI alikanusha juu ya uhalali wa wenye viti wa mitaa kuandika mikataba ya mauziano YA ARDHI, lakini hilo lipo kwa siku nyingi na yeye analifahamu. Alichotakiwa kufanya ni kuliomba Bunge liunde sheria ya kuhalalisha suala hilo, kwa vile sehemu ya watendaji wa serikali walio karibu na wananchi.

Kifanyike nini?
  • SERIKALI ZA VIJIJI ZINGEPEWA NGUVU KISHERIA JUU YA MAUZIANO YA NYUMBA/ARDHI IKISHIRIKIANA NA WIZARA YA ARDHI.
  • AU VIJIJI VIWE NA WATAALAM WA ARDHI WATAKAO SHUGHULIKIA MASWALA YA MAUZIANO YA NYUMBA/ARDHI (Hili litakuwa na gharama kubwa, long term pengine.)
  • AU VIJIJI VIMILIKISHWE ARDHI YA KIJIJI.
 
Umeongea point ya msingi sana ila huko kwingine umeingiza majungu mzee baba....
Pia jua kwamba wakili si kila kitu...
Yes umeuziwa kihalali then mara eneo ni bondeni, ni la shule, manispaa, barabara.... au utapel etc.. na wauzaji washasepa. ...
Mgogoro wa ardhi unaenda had miaka hadi 10 ..... noma sana
 
Naam, wakili anajua la kufanya, akikusimamia manunuzi, atafanya offical search, site visitation, kujua migogoro, ama kesi zilizopo mahakamani kuhusiana na ardhi, kujua kama kuna waridhi kwenye ardhi husika na mengine mengi
 
Suala la ARDHI kwa ujumla ni BOMU NA NI JANGA LA KITAIFA. Hakuna sheria ya ARDHI iliyo imara na inawafaa wananchi, ukizingatia mazingira ya wananchi hasa wa vijijini.

Hizi sheria zinafaa mijini (takriban 40% ya watanzania)tu ambako kuna wanasheria n.k, huku asilimia 60 ya Watanzania hata siku moja sheria hizi hazitawafaa kwa vile wahusika hawawezi kufika huko wakaangalia mauziano ya ARDHI kati ya eneo langu na mhitaji.

Nitakupa mfano mwepesi katika wizara ya AFYA unaolingana na huu wa wizara ya ARDHI: Fikiria wizara ya AFYA ipitishe sheria kuwa mja mzito kuzalia nyumbani ni marufuku, wajawazito wote wakajifungulie zahanati au hospitali. Halafu huko waliko zahanati wala hospitali hakuna. Sheria hii itakuwa mfu.

Kimsingi matatizo tulioachiwa na Nyerere kuhusu sheria za ARDHI , ndio zinazotutesha mpaka leo. Kila serikali toka Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hta sasa hivi wanaogopa kufanya marekebisho yenye tija kwa wananchi. Beuracracy ya kisheria imejaa katika wizara hii.

Japo waziri wa ARDHI alikanusha juu ya uhalali wa wenye viti wa mitaa kuandika mikataba ya mauziano YA ARDHI, lakini hilo lipo kwa siku nyingi na yeye analifahamu. Alichotakiwa kufanya ni kuliomba Bunge liunde sheria ya kuhalalisha suala hilo, kwa vile sehemu ya watendaji wa serikali walio karibu na wananchi.

Kifanyike nini?
  • SERIKALI ZA VIJIJI ZINGEPEWA NGUVU KISHERIA JUU YA MAUZIANO YA NYUMBA/ARDHI IKISHIRIKIANA NA WIZARA YA ARDHI.
  • AU VIJIJI VIWE NA WATAALAM WA ARDHI WATAKAO SHUGHULIKIA MASWALA YA MAUZIANO YA NYUMBA/ARDHI (Hili litakuwa na gharama kubwa, long term pengine.)
  • AU VIJIJI VIMILIKISHWE ARDHI YA KIJIJI.
yani waunde sheria kuhalalisha mauzo yafanyike kwa wenyeviti?
ur not serious comrade.

Hawapaswi wala si majukumu yao, kuna sheria ya makamishana wa viapo, ambayo mawakili ni makamishana wa viapo NOTARIES PUBLIC AND COMMISIIONER FOR OATHS, sasa
 
Umeishi vijijini? Hivi kuna mawakili wangapi huko vijijini? Tafuta solution mbadala!
 
Back
Top Bottom