PreGE2025 Pigo kwa ACT - Wazalendo, Katibu Wilaya ya Tunduru, Diwani wa Mchoteka watimkia CCM wakati wa mkutano wa Nchimbi

PreGE2025 Pigo kwa ACT - Wazalendo, Katibu Wilaya ya Tunduru, Diwani wa Mchoteka watimkia CCM wakati wa mkutano wa Nchimbi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Diwani wa Mchoteka kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Seif Dauda pamoja na Katibu wa Wilaya ya Tunduru, Said Mponda na baadhi ya wanachama wa chama hicho, wamejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) Jumatano, Aprili 2, 2025.

Tukio hilo limetokea katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mlingoti, Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma.

Pia soma: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Dk. Nchimbi ameanza ziara ya siku tano mkoani Ruvuma kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025.

Baada ya kuwapokea, Dk. Nchimbi aliwapongeza kwa uamuzi wao wa kujiunga na chama kinachowatetea.

Akizungumza kwa ufupi, Mponda alisema: "Nilikuwa CUF, nikahama kwenda ACT-Wazalendo, na tulipambana mwaka 2020 tukapata diwani wa Mchoteka. Lakini kutokana na yanayoendelea CCM, mimi na wenzangu tumeamua kujiunga na CCM."

Naye Dauda alisema kuwa uamuzi wa kujiunga na CCM umetokana na juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwemo kumpendekeza na kumteua Dk. Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa urais.

 
Back
Top Bottom