Pigo: Kampuni ya Erolink Limited yafika kiama Vodacom wafanyakazi kupunguzwa

gasto genaro

JF-Expert Member
Oct 15, 2014
780
554
Wakuu,

Kampuni inayokiongoza kitengo cha huduma kwa wateja Vodacom, mkataba wake una malizika mwisho wa mwezi huu wa tano 2017.

Kiama hiki kinakuja pale ambapo watanzania wengi haswa vijana walipo na uhitaji mkubwa wa ajira, huku serikali yao pendwa ikiwa imezuia ajira kwa takribani mwaka na nusu.

Ikumbukwe kuwa, erolink ni kampuni iliyoajiri vijana zaidi ya 1000 nchini. Kwa vodacom pekee, erolink ina wafanyakazi zaidi ya 500.

Kuondoka kwa erolink vodacom, ni pigo kwa baadhi ya wafanyakazi maana ni lazima redundancy ifanyike.

448b062b29c64742d25344817eeec46c.jpg



Updates!

Nimepata habari kuwa, ajira za wafanyakazi wote waliokua Chini ya erolink zitakua safe maana mwajiri mpya atawatumia wafanyakazi hao hao. Kwaiyo msiwe na hofu wafanyakazi mliokua chini ya Erolink.
 
natamani kusikia anayewareplace labda atakuwa na utu kidogo erolink wanalalamikiwaga sana
 
Kaondoka kwa erolink sio mwisho wa Vodacom kutoa huduma kwa wateja bali hapo kitakachofanyika haohao wahudumu watapewa mkataba na kampuni itakayokuwa imepewatenda kama ilivyokuwa erolink

ni mawazo yangu lakini
 
duuuh!! Duniani hakukaliki mbinguni hakuendeki hadi 2020 tutakuwa kama korea ya kaskazini
 
Serikali inahusika vipi na mkataba wa Vodacom na Erolink, hata hivyo wakiondolewa Erolink kuna kampuni nyingine itapewa ulaji na kuna watu wataajiriwa pia.
 
Back
Top Bottom