Pigo chadema: Lema avuliwa ubunge arusha mjini, jaji amzuia kugombea miaka mitano, vilio mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pigo chadema: Lema avuliwa ubunge arusha mjini, jaji amzuia kugombea miaka mitano, vilio mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 6, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Thursday, 05 April 2012 10:56[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]

  Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema

  LEMA AVULIWA UBUNGE ARUSHA MJINI, JAJI AMZUIA KUGOMBEA MIAKA MITANO, VILIO MAHAKAMANI

  Waandishi Wetu, Arusha

  MAKAHAMA Kuu Kanda ya Arusha, imetengua matokeo ya ubunge yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema, Godbless Lema baada ya kuridhika kuwa alitumia lugha ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi huo wa mwaka 2010, Dk Batilda Burian.

  Lema ni mbunge wa nne nchini kuvuliwa ubunge na mahakama katika kipindi cha miaka 16 iliyopita kutokana na kasoro zilizojitokeza katika mchakato wa uchaguzi.

  Akisoma hukumu yake jana iliyochukua zaidi ya saa nzima, Jaji Gabriel
  Rwakibarila alimtia hatiani Lema kwa makosa mawili kati ya manne
  aliyokuwa akikabiliwa nayo, huku akitupa mawili kwa kukosa ushahidi.

  Ndani ya ukumbi wa mahakama uliojaa wanachama, wafuasi na wapenzi wa Chadema, Jaji Rwakibarila alimvua ubunge Lema baada ya kuridhika na ushahidi kuwa alitumia maneno ya kashfa na ubaguzi wa jinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Burian.

  Jaji Rwakibarila katika hukumu yake hiyo, pia alimwamuru Lema kulipa gharama za kesi hiyo na kwamba ana haki ya kukata rufaa ikiwa hajaridhika na hukumu hiyo.

  Uamuzi wa Jaji huyo ni kama umetia doa shamrashamra za Chadema ambazo zilikuwa zikiendelea baada ya chama hicho kushinda kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, kupitia kwa mgombea wake, Joshua Nassari.

  Makosa ya Lema
  Lema alitiwa hatiani kwa kudaiwa kusema kuwa Dk Burian hakustahili kuchaguliwa kuwa mbunge kwa sababu mila na desturi za makabila ya Waarusha (Wamaasai na Wachaga), mwanamke hawezi kuongoza wazee.

  Sababu ya pili aliyotumia Jaji kutengua ubunge wa Lema kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Dk Burian kuwa ni mwanamke asiye mwaminifu, aliyezaa nje ya ndoa na alikuwa na mimba nyingine na bwana huyo aliyezaa naye ambaye siyo mumewe.

  Jaji Rwakibarila alitupilia mbali madai mawili ya kutumia lugha na maneno yenye mwelekeo wa ubaguzi wa kidini na ubaguzi wa makazi.

  Kuhusu ubaguzi wa kidini alikataa madai ya walalamikaji Mussa Mkanga,
  Agness Mollel na Happy Kivuyo kuwa kauli ya Lema kuwataka wapiga kura wa Arusha kujihadhari na wanaovaa vitambaa na hijabu wasije kujikuta wanachagua Al Qaida kuwa haihusiani na dini ya Kiislamu.

  "Mwanamke kuvaa kitambaa kichwani haina uhusiano wowote na dini ya
  Kiislam wala Al Qaida kwani ni dhahiri wanawake wengi ambao baadhi yao
  siyo Waislam wanavaa vitambaa. Kwanza ni heshima kwa wanawake kuvaa vilemba hivyo madai haya nayatupilia mbali," alisema Jaji Rwakibarila katika hukumu yake.

  Kuhusu tofauti ya ukaazi kati ya Lema na Dk Burian aliyedaiwa kuolewa
  na kuishi Zanzibar, Jaji huyo alisema hoja hiyo isingeharibu wala kwenda
  kinyume na maadili ya kampeni kwani kisheria Mtanzania ana haki ya
  kuishi upande wowote wa Jamhuri ya Muungano, yaani Bara na Visiwani.

  Katika shauri hilo namba 13/2010, wadai waliowakilishwa mahakamani na Mawakili Alute Mughwai na Modest Akida, waliomba mahakama kutengua matokeo yaliyompa ushindi Lema kwa madai kuwa alitumia lugha na kauli za matusi, kashfa na udhalilishaji dhidi ya Dk Burian wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.

  Jaji Rwakibarila alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 14 wa
  upande wa wadai na wanne wa upande wa utetezi, aliridhika kuwa Lema alitamka maneno ya kibaguzi, kijinsia na kashfa dhidi ya Dk Burian katika mikutano yake minane ya kampeni kati ya mikutano zaidi ya 60 aliyofanya.

  Kabla ya kuanza kusikilizwa mbele ya Jaji Rwakibarila, shauri hilo
  lilikuwa mbele ya Jaji Aloyce Mujulizi aliyejitoa baada ya Lema kueleza kutokuwa na imani naye kutokana na wabunge wa Chadema kuwahi kuituhumu kampuni yake ya uwakili ya IMMA aliyokuwa akifanyia kazi
  kabla ya kuteuliwa kuhusika na ufisadi wa akaunti ya EPA katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

  Jaji Rwakibarila alianza kusikiliza shauri hilo mfululizo kuanzia mapema Februari kutokana na kutakiwa kulimazika kabla ya Mei 3, mwaka huu kutokana na mahitaji ya kisheria inayoelekeza kesi za uchaguzi zisikilizwe na kuamuliwa ndani ya mwaka mmoja tangu kufunguliwa.

  Licha ya kuibuka washindi kwa uamuzi wa Jaji jana, wadai katika shauri
  hilo pamoja na mawakili wao walionekana kupigwa bumbuwazi mahakamani bila kuamini kilichotokea hadi watu walipoanza kuondoka baada ya Jaji kutoka ndipo waliposimama na kuanza kukumbatiana na kupongezana.

  Baada ya mwaka mmoja kukamilika Novemba, mwaka jana, Msajili wa Mahakama Kuu, Herbert George aliandika barua kwa Waziri mwenye dhamana ya sheria ambaye aliongeza kipindi cha ziada cha miezi sita
  kinachomalizika Mei 3, mwaka huu.


  Mkanganyiko kwenye hukumu

  Jaji Rwakibarila kwa upande mwingine anadaiwa kujichanganya katika vifungu vya sheria alivyotumia katika uamuzi wake.

  Akitoa uamuzi wake jana, Jaji huyo alisema Lema alithibitika kutenda kosa la kutumia maneno yasiyostahili kwenye kampeni zake za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

  Kwa kauli ya kisheria, Jaji alisema Lema anatiwa hatiani kwa kosa la
  ‘Illegal Campaign' kwa kutoa kauli za kumbagua kijinsia Dk Burian
  akitumia tofauti yao ya kimaumbile ya yeye kuwa mwanamme na mwenzake mwanamke aliposema mila na desturi za Waarusha na Wachaga haziruhusu mwanamke kuongoza wanaume.

  Alisema hata kauli ya Lema kuwa Dk Burian siyo mwanamke mwaminifu
  aliyezaa nje na kupata mimba nje ya ndoa ilikuwa ya kashfa dhidi ya
  mgombea huyo wa CCM na kutafsiri kosa hilo kama ‘Illegal Campaign'
  aliyosema inatosha kutengua matokeo ya uchaguzi.

  Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, makosa yote mawili yanaangukia
  kwenye kifungu cha 108, kifungu kidogo cha pili aya ‘A' ambayo
  humruhusu aliyevuliwa ubunge kugombea kwenye uchaguzi mdogo
  utakaoitishwa.

  Lakini katika majumuisho ya hukumu yake, Jaji Rwakibarila alitumia
  kifungu cha 114 cha sheria ya uchaguzi inayozungumzia "Illegal
  Practice" ambayo yanaangukia kwenye makosa yanayohusiana na vitendo vya rushwa kwa wapiga kura, watendaji wa Serikali na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  Wakili wa Lema, Method Kimomogoro alithibitisha utata huo na kusema atafuatilia kujua iwapo Jaji Rwakibarila alijichanga katika kutaja vifungu hivyo vyenye maana na adhabu tofauti kisheria.

  "Anayehukumiwa kwa makosa yanayoangukia kwenye kifungu cha 108 (II) (A) kama ilivyotokea kwa mteja wangu (Lema) anaruhusiwa kugombea kwenye uchaguzi, lakini kwa mshangao wakati akihitimisha hukumu yake jaji alitaja kifungu cha 114 ambacho ni kinyume na makosa aliyokutwa nayo Lema," alidai Wakili Kimomogoro.

  Bila kutaka kuingia kwa undani katika suala hilo hadi atakapopata
  nakala ya hukumu hiyo, Kimomogoro alidai hadi jana jioni alikuwa
  hajapata maelekezo yoyote kutoka kwa mteja wake kuhusu hatua za
  kuchukua dhidi ya uamuzi huo.

  Kimomogoro alieleza kuwa iwapo hukumu hiyoitaachwa kubakia kwenye kifungu hicho cha 114 ina maana mteja wake Lema hataruhusiwa kugombea ubunge kwa kipindi kisichopungua miaka mitano, jambo ambalo siyo haki kwa sababu hakushtakiwa wala kukutwa na hatia ya kujihusisha na rushwa wakati wa kampeni.

  Kwa upande wake, wakili wa wadai Alute Mughwai aliyekuwa akisaidianana Modest Akida alieleza kuridhishwa na uamuzi huo ingawa aliahidi kuwasiliana na wateja wake kuangalia uwezekano wa kukatia rufaa hoja mbili za ubaguzi kimakaazi na kidini zilizotupwa na mahakama.

  Happy Kivuyo aliyekuwa mdai wa tatu katika shauri hilo nambo 13/2010
  alieleza kufurahishwa na hukumu hiyo aliyodai imewatendea haki wote
  waliochukizwa na matusi, kashfa na udhalilishaji uliofanywa na Lema
  dhidi ya Dk Burian.


  Kauli ya Mbowe
  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amevitaka vyombo vyenye Mamlaka ya Maamuzi nchini, ikiwepo Mahakama kusoma alama za nyakati kabla ya kutoa uamuzi ambao unaweza kusababisha nchi kuingia katika machafuko.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Chadema Mkoa wa Arusha, eneo la Ngarenaro, kuhusu hukumu ya Jaji Rwakibarila, Mbowe alisema ni hatari pale watu wanapoanza kutilia shaka vyombo vya uamuzi kama Mahakama Kuu.

  "Sitaki kuingilia uamuzi ya mahakama, lakini ni kweli kuwa uamuzi wa hukumu hii ulivuja hata kabla ya kusomwa, tulipewa taarifa za ubunge wa Lema kutenguliwa, sasa hili ni jambo la hatari kama tutaendelea kuvujisha uamuzi wa kisheria, nchi inaweza kuingia kwenye machafuko pale watawala wanapoingilia vyombo vya kisheria,"alisema Mbowe.

  Alisema Serikali na vyombo vingine vyenye Mamlaka, ni lazima wajue kuwa, enzi za kuwaburuza watu zimepitwa na wakati.

  "Mahakama zisifikiri zinaweza kufanya kila ambacho zinataka bila kuzingatia, sheria, taratibu na matakwa ya umma, mimi sitaki tukife huko,"alisema Mbowe.

  Alisema katika kesi hiyo ya Lema, wanaamini uamuzi ya mahakama umeingiliwa na chombo kingine jambo ambalo ni hatari katika utawala wa Sheria.

  Kukata rufani
  Kuhusu Chadema kuukatia rufaa uamuzi wa Lema kuvuliwa ubunge, Mbowe alisema bado wanasubiri nakala ya hukumu ya kesi hiyo na wanafanya majadiliano kupitia mawakili wa chama hicho na viongozi wengine na kisha watatoa uamuzi ambao utatangazwa kesho Jumamosi kwenye mkutano wa hadhara.

  Mbowe alisema, ingawa wananchi wengi wa Arusha wanataka kurejewa haraka kwa uchaguzi, lakini, hawafahamu kama Mbunge wao Lema, kulingana na hukumu hiyo ataruhusiwi kugombea tena.

  "Kabla ya kufikia uamuzi wowote tumeona ni busara kwanza, tukae kwani Lema ambaye wanamtaka kwa hukumu hii ni lazima tukate rufani,"alisema Mbowe.

  Hata hivyo, aliwaomba wananchi wa Arusha, kutulia kwa sasa na kutofanya vurugu zozote ili kuthibitisha Chadema sio chama cha vurugu na ni chama cha wanademokrasia wa kweli.

  Alisema katika mkutano wa Jumamosi, watatoa tamko la pamoja kama watakata rufani au watatoa nafasi kwa wanachama wengine wa Chadema kujitokeza kumrithi Lema.

  Kabla ya kukutana na waandishi wa habari, Mbowe alizungumza na mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha nje ya Uwanja wa ofisi za Chadema, ambao pia aliwataka kutulia wakati chama hicho kinatafakari uamuzi wa kuchukua.

  Chaguzi zilizowahi kutenguliwa
  Mwaka 1996 aliyekuwa mbunge wa Temeke, Ramadhani Ali Kihiyo alivuliwa ubunge baada ya Mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kughushi cheti na nafasi yake ilichukuliwa na Augustine Mrema, wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi.

  Vivyo hivyo Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba ilitengua ubunge wa aliyekuwa mbunge wa Biharamulo Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Tanzania Labour (TLP), Phares Kabuye.

  Kabuye aliyefariki dunia kwa ajali ya gari akiwa njiani kuelekea jijini Dar es Salaam, alivuliwa ubunge baada ya mahakama kuthibitisha kuwa katika mchakato wa uchaguzi mwaka 2005, alimdhalilisha mgombea mwenzake, Anatoly Choya.

  Desemba 28, 2007 Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kupitia kwa Jaji Josephat Mchome ilitengua matokeo ya aliyekuwa mbunge wa Mwibara Charles Kajege kutokana na kutiwa hatia kwa rushwa.

  Kesi ya kupinga matokeo ya hayo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia TLP, Mtamwega Mgaywa, (TLP) aliyeshindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2005.

  Hata hivyo, Septemba 25, 2009, Mahakama ya Rufaa chini ya majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania wakati huo, Agustino Ramadhani, January Msofe na Jaji Mbaruku, walimrejeshea Kajege ubunge kutokana na rufaa aliyokata dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu.

  Habari hii imeandaliwa na Mussa Juma, Arusha, Peter Saramba, Moses Mashalla
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mmm, amezuiliwa kugombea?
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwahiyo, kafungiwa kwa Miaka Mitano hawezi kugombea - ni lazima akate rufaa na pia ni Miaka 16 tangu Mbunge halali atenguliwe Ubunge Nchini

  Huyu Hakimu kwanini anaulizia Elimu ya Lema? hajui kama angekuwa wakati wa Nyerere angeulizia juu ya Elimu ya Mbunge angetupwa Jela? sababu wabunge wengi wakati ule hawakumaliza shule au hawakuenda shule; kitu kinachotakiwa ni hekima ya kwaongoza wananchi.

  Hii labda ni trick; sababu kama Chadema ingekuwa na hilo Jimbo la Arusha pamoja na Arumeru ina Maana ongezeko la idadi ya wananchi kuchagua CHADEMA kwahiyo Idadi ya Wapinzani kuiwakilisha East African Parliament haitakuwa mtu mmoja itakuwa watu 2 au 3 na kuharibu hesabu zote za CCM ya kuwa na wawakilishi 8 Mmeona hapo?
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Read between lines!
  Hajazuiwa kugombea kwa miaka mitano,bali
  "kutokana na utata wa kisheria wa vifungu vilivyo nukuliwa" review zaid inahtajika!
  Ndio maana makamanda Mbowe na Slaa wameweka kiporo ili kutazama utata huo kwa kutumia wanasheria wao waliobobea na baadaye kuibuka na tamko kesho.
  MY TAKE:
  1:Mtoa thread arudi hapa na maelezo yanayo jitosheleza kueleza utata huo wa kisheria.
  2:Mtoa mada a edit title ya thread yake kama atashndwa kufanya namba 1 hapo juu.
  3:Namba 2 hapo juu itakapo fanyika,Mods wa move hii thread maana tayari itakuwa inafanana na breaking news iliyo kuwa sticked humu.
  Naomba kuwasilisha.
   
 5. john tongo

  john tongo JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Aluta continue
   
 6. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Towards which direction?
   
 7. Pipiro

  Pipiro JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 307
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mimi nina imani huyu Jaji hajakosea hata mara moja.. Sio bahati mbaya kunukuu vifungu tofauti bali ni makusudi mazima. Hapo mpango mzima ulikuwa waje na kifungu cha hukumu ambacho kitamzuia Lema kugombea tena lakini kwa bahati mbaya makosa yaliyomtia hatiani hayahusiani na rushwa ambayo yangemfanya asigombee tena kwa miaka 5.

  Wamejaribu kumtia hatiani wameweza kwa makosa yaliyotajwa, lakini wameshindwa kumtia kwenye makosa yatakayompiga ban ya kutoshiriki siasa na uchaguzi kwa miaka 5. Sasa akaamua kuiweka kimtego. Usishangae hapo ndio watakapojumlisha kuwa makosa ya Lema yanahusishwa na rushwa na hapo ndipo wanapopataka kwani Chadema watakata rufaa na ndio lengo lao litatimia kwani itachukua miaka miwili kuja kuisha na mwaka wa mwisho utakuwa mwaka wa kujiandaa na kampeni za 2015.

  Hapo sasa ndipo CCM wanategemea wananchi kuanza kuigeuka CDM kusema kuwa muda mwingi viongozi wao na wabunge wanautumia kwenye kesi na mahakamani huku kwa nyuma CCM inakuja kusilibia kuhusu suala hilo la CDM kushughulika na maandamano na kesi hawana muda wa kushughulikia kero zao kama walivyoahidi.

  Naamini haitakuwa hivi...
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  The way the cookie crumbles....

  Politics is a dirty game..
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu EliahKamwela,
  Unajua hukumu hii imewekwa kimtego na ndipo Judge aliyetoa hukumu anajiweka kwenye spotlight na ndipo watu wanapoanza ku-question kwamba je hukumu hii haina mkono wa serikali?

  Ukisoma hiyo habari, ni wazi kwamba Lema amekuwa convicted kwa makosa fulani ya kutumia lugha isiyo sahihi na hukumu yake ni kutengua Ubunge. I guess hukumu kama hiyo iliwahi kutokea miaka ya nyuma zama za Lepilal ole Moloimet alipogombea Ubunge Jimbo la Monduli. Kuna mtu aliitwa "layoni" kwa kuwa alitahiriwa hospitalini na kwamba wamasai wasikubali kuongozwa na layoni. Pia kulikuwa na shitaka jingine la kuhutubia kwa kimasai. Sikumbuki vyema hukumu yake ilikwendaje, but kama kuna wana sheria wenye kumbukumbu wanaweza kutuwekea hapa hiyo kesi na hukumu yake.

  Tatizo ninaloliona hapa na ndipo mtego ulipo, ni kwamba Lema amekuwa convicted kwa kutumia lugha ya udhalilishaji lakini kifungu kilichotumika kutengua ubunge wake kinahusiana na mgombea kujihusisha na rushwa, of which rushwa haikuwemo kwenye mashitaka.

  Judge ametumia kifungo hicho kimtego, kwamba automatically Lema hawezi kuruhusiwa kugombea tena kwa kipindi cha miaka 5 na Judge kwa ujanja, hakutamka explicitly kwamba Lema amefungiwa. Bali ni jukumu la Mwanasheria wake kutambua kwamba matokeo ya ubunge yakitenguliwa kwa kifungu hicho, humaanisha kwamba Mbunge kapoteza ubunge na pia hawezi kugombea kwa miaka 5.

  Kinachosubiriwa na CCM/Serikali ni kuona kwamba je Lema atakata rufaa au atakubali ili atumie hukumu ya wananchi? Kama CHADEMA watamteua agombee then CCM itaweka pingamizi kwamba ubunge wake ulitenguliwa kwa kwa kifungu hiki, hawatasema kwamba alikuwa convicted kwa makosa haya. Maana wakitaja makosa, hayaendani na hukumu. So, watasema mbunge akitenguliwa ubunge wake kwa kifungu hiki maana yake ni kwamba haruhusiwi kugombea Ubunge kwa miaka 5. Hapo pingamizi la CCM litapeta na CHADEMA watatupwa nje na hivyo CCM itakuwa haina mpinzani mwenye nguvu na hivyo kushinda kirahisi.

  Njia ya kukwepa hilo ni CHADEMA wakubali kuteua mgombea mwingine badala ya Lema au Lema akishapokea hukumu na ikawa imekaa mkao ambao ni wa kimtego, wakate rufaa ili mahakama ya rufani ipitie hukumu hiyo na kuondoa huo utata wa kuwa convicted kwa makosa fulani lakini ruling inatumia kifungu tofauti. Kama CHADEMA wakienda kwa njia hiyo, then labda mahakama ya rufani inaweza kuchelewa kusikiliza hiyo rufaa kwa mwaka mzima of which inazidi kuongeza chuki kwa wananchi na hivyo wananchi kuichukia zaidi CCM kwa kuwa tayari kuna kata hazina madiwani na serikali + tume ya uchaguzi wako kimya tu.

  Kama hukumu itakuwa imekaa kimtego, hiyo ni kete nzuri sana kwa CHADEMA kwamba wananchi oneni jinsi haki zenu zinavyokandamizwa na vyombo vya kutoa haki. Haya yote yanafanyika ili kudumaza demokrasia na kuhakikisha kwamba CCM inashinda. Kwa hiyo mahakama itakuwa imejiingiza kwenye aibu kubwa sana. Hayo yasemwe kabla kesi ya rufani haijafunguliwa, na once ikishafunguliwa wasubiri hukumu ya mahakama ya rufani.
   
 10. K

  Keil JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Pipiro,

  Nakubaliana na hoja zako za mtego, na kuna post nimeandika ambayo ina mtazamo kama wa kwako. Ndio maana kwenye hukumu, Judge hakuweka wazi swala la adhabu ya kufungiwa miaka 5 kwa kuwa anajua angejiweka kwenye spotlight na huo ni mwanya kwa CCM kuweka pingamizi just in case Lema akiamua kugombea bila kukata rufaa.

  Hoja kwamba CCM watawageuzia CHADEMA kibao, sidhani kama inaweza kuwa na mashiko kwa watu wenye uelewa. Wananchi siku hizi na haswa wa mijini wamefunguka sana na wanajua kila kitu kinachoendelea kwenye politics za maeneo yao. Hapo CCM haiwezi kukwepa. Mimi naona hii hukumu ni nzuri sana na inaweza kuwa ni mtaji kwa CHADEMA.

  Mahakama ya Rufani nayo itajiweka kwenye spotlight kwa kuchelewa kutoa hukumu na pia kama Mahakama ya Rufani itabadilisha vifungu vilivyotumika kutenguaa Ubunge wa Lema, itakuwa ni mtaji kwa CHADEMA kwamba Judge mzima anam-convict mtu kwa makosa ya kifungu fulani halafu anamkuhumu kwa kutumia kifungu ambacho hakihusiani na makosa hayo? Hivi kweli hapo Judge atajitetea vipi? Watu wakisema alihongwa na mafisadi atakana? Maana kosa alilofanya kwenye hukumu yake, hata mwanafunzi wa sheria ngazi ya cheti hawezi kuyafanya, unless awe under influence ya ufisadi (rushwa).
   
Loading...