Piga Kura ya Lissu kufunguliwa Mashtaka mapya..

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,613
12,270
Nikiwa kama mtanzania mwenye mapenzi mema na taifa langu, ningependa watanzania wenzangu na wanajamii forum tupige kura kwa matamshi yalio tolewa na Lissu kuwa Serikali ya Magufuli ni ya hovyo, serikali ya kidikteta, serikal inaongoza na fikra za mtu mmoja, serikali inayopaswa kupingwa na kila mwananchi" mwisho wakumnuku.

Kitendo cha Lissu kuiita serikali ya Mh Magufuli ya hovyo kinatafsiriwa kama kejeli, dharau na uvunjifu mkubwa wakatiba kama ilivyoainishwa kwenye ibara 18 juu ya uhuru wakutoa maoni.

Ni lazima sote tujiulize serikali ya hovyo ni nani? Na je serikali ni akina nani? Ukipata majibu yake utagunduwa Lissu amewatusi wa Tz pamoja na vyombo vyote vya ulinzi akiamini hakuna wakumfanya kitu.

Jambo ambalo mimi kama mtanzania nalikataa. Ikiwa serikali híi ni ya hovyo atuonye uhovyo wake na sababu ya tafsiri yake kuwa hii ni serikali ya hovyo.
Serikali hii ni ya kidikteta.

Nadhani wote tunajuwa serikali za kidkteta zipoje na hili la yeye kupelekwa mahakaman kujibu shutuma za uchochezi ni suala lipo wazi kwenye uhuru wa kutoa maoni sasa uhuru una mipaka yake sasa ikiwa kupelekwa kwake mahakamani anatafasiri ni udikteta.

Tungependa kujua kura tulipiga mwaka jana zilikuwa ni za ndio au hapana? Ama zilikuwa kura za vyama vingi? Akisha tufafanulia ndipo atutafsirie maana ya serikali ya Mh Magufuli kuita ya kidikteta alimanisha nini?

Serikali hii haina budi kupingwa na kila mtanzania. Hapa Lissu alimanisha nini? Wananchi waandamane kupinga serikali híi walioichaguwa wenyewe ama watu waingie msituni wapigane vita au alimanisha nini? Na kwanini aseme lugha ya kichochezi?

Mwisho labda ni seme this time taifa letu tumepata kiongozi mwenye nia ya dhati kuleta maendeleo na kama upinzani wanahisi hawana cha kusema au kukosoa bora kukaa kimya ili kuleta hali ya amani na umoja wa taifa hili nilazima Lissu na wanachadema wajue tunalipenda taifa letu, amani yetu na viöngozi wetu kuliko propaganda zao zakuganga njaa huko mtaani.

Tupo watu kulitetea taifa letu kwa gharama yoyote na huu mchezo watu kama Lissu wanaufanya this time haukubaliki maana mara baada ya Oct 2015 inajulikana kwa sura na matendo hamkukubaliana na matokeo ila mkanuwia kufanya haya mnayafanya sasa.

Ila ni bora watanzania zaidi ya milioni arobaini na kitu kuliko kundi dogo la wasaka tonge msio na shukurani kuendelea kulisumbua taifa.

Ajenda iliopo mbele yetu ni moja tu kulijenga taifa letu kwa nguvu zetu zote na akili zetu zote watu aina ya Lissu tuwafungie vioo tuwaambie hayo wanayafanya sasa mwisho ilikuwa mwaka jana.

Hatudanganyiki na aina ya vyama visivyokuwa popo wala ndege.

Mwisho.
 
Hivi ndugu zangu watanzania, mimi napenda kujifunza kutoka kwa wanasheria wetu:
Hivi unaweza kushtaki wazo? Nina maana, maoni, mawazo na kauli inashtakika?
Tunaanzia wapi kuanza kufukuzana na maoni/mawazo/kauli? To put it more clearly, can we prosecute a thought?

Mbona taifa tunataka kuliondoa kwenye agenda ya maendeleo na kulipeleka kusiko?
Tundu kasema, nawe sema, na yule aseme. Kasema serikali ni ya ovyo, je wazo na maoni hayo yana dhambi gani ya kupelekwa mahakamani? Atakayempeleka mahakamani ndiye wa ovyo. Anayeshabikia tumpeleke mahakamani ndiye wa ovyo. Si ajabu hata mimi ninayechangia hapa ndiye wa ovyo. Ngoja niachie hapa nisiendelee kuanika u-ovyo wangu.
 
Ila kwa nini akipelekwa mahakamani anashinda kesi. Jibu ni kuwa inaonyesha hajafanya kosa.

Kama anashinda kesi kwa nini apelekwe kwa kesi isiyo na kosa Hata hapo nje ya mahakama kasema kauli nzito.

Nisaidieni mtu ambaye haingii kwenye kikao cha baraza la Mawaziri anatoa wapi jeuri ya kusema maamuzi ni ya Rais tu?
 
Kujadili kuzuri. Mwisho wa yote itajulikana.someni ala za nyakati..Ufunuo 13:11-15 mtapata majibu.Uhuru uliopo.hautakuwepo. tena linakuja hakutakuwa na Uhuru wa dhamiri.muda utasema.
 
Nikiwa kama mtanzania mwenye mapenzi mema na taifa langu, ningependa watanzania wenzangu na wanajamii forum tupige kura kwa matamshi yalio tolewa na Lissu kuwa Serikali ya Magufuli ni ya hovyo, serikali ya kidikteta, serikal inaongoza na fikra za mtu mmoja, serikali inayopaswa kupingwa na kila mwananchi" mwisho wakumnuku.
Kitendo cha Lissu kuiita serikali ya Mh Magufuli ya hovyo kinatafsiriwa kama kejeli, dharau na uvunjifu mkubwa wakatiba kama ilivyo ainishwa kwenye ibara 18 juu ya uhuru wakutoa maoni. Nilazima sote tujiulize serikali ya hovyo ni nani? Na je serikali ni akina nani? Ukipata majibu yake utagunduwa Lissu amewatusi wa Tz pamoja na vyombo vyote vya ulinzi akiamini hakuna wakumfanya kitu. Jambo ambalo mimi kama mtanzania nalikataa. Ikiwa serikali híi ni ya hovyo atuonye uhovyo wake na sababu ya tafsiri yake kuwa hii niserikali ya hovyo.
Serikali hii ni ya kidikteta. Nadhani wote tunajuwa serikali za kidkteta zipoje na hili la yeye kupelekwa mahakaman kujibu shutuma za uchochezi ni swala lipo wazi kwenye uhuru wakutoa maoni sasa uhuru unamipaka yake sasa ikiwa kupelekwa kwake mahakamani anatafasiri ni udikteta tungependa kujuwa kura tulipiga mwaka jana zilikuwa ni za ndio au hapana? Ama zilikuwa kura za vyama vingi? Akisha tufafanulia ndipo atutafasirie maana ya serikali ya Mh Magufuli kuita ya kidikteta alimanisha nini?
Serikali hii haina budi kupingwa na kila mtanzania. Hapa Lissu alimanisha nini? Wananchi waandamane kupinga serikali híi walio ichaguwa wenyewe ama watu waingie msituni wapigane vita au alimanisha nini? Na kwanini aseme lugha yakichochezi?
Mwisho labda ni seme this time taifa letu tumepata kiongozi mwenye nia ya dhati kuleta maendeleo na kama upinzani wanahisi hawana chakusema au kukosoa bora kukaa kimya ili kuleta hali ya amani na umoja wa taifa hili nilazima Lissu na wanachadema wajuwe tunalipenda taifa letu, amani yetu na viöngozi wetu kuliko propaganda zao zakuganga njaa huko mtaani. Tupo watu kulitetea taifa letu kwa gharama yeyote na huu mchezo watu kama Lissu wanaufanya ths tm haukubaliki maana mara baada ya Oct 2015 inajulikana kwa sura na matendo hamkukubaliana na matokeo ila mkanuwia kufanya haya mnayafanya sasa. Ila ni bora watanzania zaid ya milion arobain na kitu kuliko kundi dogo la wasaka tonge msio nashukurani kuendelea kulisumbua taifa. Ajenda iliopo mbele yetu ni moja tu kulijenga taifa letu kwa nguvu zetu zote na akili zetu zote watu aina ya Lissu tuwafungie vioo tuwaambie hayo wanayafanya sasa mwisho ilikuwa mwaka jana. Hatudanganyiki na aina ya vyama visivyokuwa popo wala ndege. Mwisho.
Well said. Tunatumaini DPP atayafanyia kazi maoni yako. Hivi ndivyo jukwaa la great thinkers linavyopaswa kuwa. Hawa wa porojo na uanaharakati Jf ni vyema sasa mkaanzisha jukwaa lao. Ukitoa mchango au uzi usioendana na great thinker uhahamishiwa automatically kwenye.jukwaa la porojo & harakati za kisiasa. Hii itasaidia sana hata kwa watawala wa serikali yetu. Si kwamba porojo na uharakati wa siasa hauna umuhimu - laa haswa ila zinapaswa kutenganishwa.
 
Bwege, malofa, wabunge viti maalu lazima uwe baby, umesahau. Viweke hapo pia. Naibu spuka anamwambia mheshimiwa toa ubwege hapa ni safi kanisa. Neno hilo likitumiwa upande mwingine ni balaaa. Kunya anye kuku akinya bata .........
Toka lini watu wanapiga kura mtu afunguliwe mshtaka. Kwa sheria ipi.
 
Back
Top Bottom