Pichani Shule zetu - Usafi chooni inashindikana?

Pichani Shule zetu - Usafi chooni inashindikana?

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
IMG_8122.jpg


Choo cha shule ya msingi Lipangala, huko sehemu mojawapo ya Ludewa. Nashangaa hata kusafisha eneo linalozunguka choo ni:
  • Mbunge achangie?
  • Serikali ipangie bajeti?
  • Wazazi wachangie?
  • Walimu wahimizwe?
  • Kaka Mkuu na Dada Mkuu wa shule hawana akili timamu?
  • Elimu ya maisha na kujitegemea mashuleni imesitishwa?
​Kama mambo hayo hayahitajiki kwa nini kusiwe na taratibu za wanafunzi kufanya usafi wa mazingira yao? Nahofia hapa ipo siku nyoka atakanyagwa mkia kisha kumng'ata mguu mwanafunzi.
 
na usishangae kwamba wanafunzi huenda vichakani hicho huwa hakitumiki.....yani kazi kweli kila kitu ni serikali hadi usafi wa choo jamani hii sasa imezidi
 
Amavubi, hakuna zamu siku hizi? Zamanitulikuwa na zamu za za wanafunzi wakati wa likizo
 
Mkoloni ni bora kuliko mzalendo! Mkoloni alijenga shule za msingi bora na kuhakikisha vyoo vyake ni bomba sana. Leo hii pesa zote za kuimalisha shule zinakwenda kuimalisha chama! lakini mbunge wa hiyo wilaya na gari la mkopo, na dereva wake analipwa mshahara na serikani! malezi ya chama chashika hatamu hayo. Kujali kuimalisha chama kuliko imalisha elimu!
 
Katika maisha ya vijijini changamoto ni nyingi sana.
 
Amavubi, hakuna zamu siku hizi? Zamanitulikuwa na zamu za za wanafunzi wakati wa likizo

Umenikumbusha, tulikuwa na zamu kipindi cha likizo kwenda shuleni kutunza mazingira ya shule, kwani hakukuonekana tofauti ya usafi mazingira ya shule kipindi cha likizo na wakati wa kawaida wa mihula ya shule.
 
na usishangae kwamba wanafunzi huenda vichakani hicho huwa hakitumiki.....yani kazi kweli kila kitu ni serikali hadi usafi wa choo jamani hii sasa imezidi

Nilikoukokotoa uzi huu maudhui ya habari ni kwamba wanafunzi hujisaidia vichakani, we una jicho la mbali kuona mazingira. Sitashangaa kando ya choo hiki majani yamesitawi sana tokana na mbolea itokayo kwa watoto wanaojisaidia huko porini.
 
Mmmmh!
Hiki nacho ni CHOO au kiota cha ndege yule anaeletaga mvua!
 
Umenikumbusha, tulikuwa na zamu kipindi cha likizo kwenda shuleni kutunza mazingira ya shule, kwani hakukuonekana tofauti ya usafi mazingira ya shule kipindi cha likizo na wakati wa kawaida wa mihula ya shule.

sure,ukitaka kusafiri inakupasa uombe ruhusa mapeeema
 
Hivi wanachojenga ni matundu ya choo au choo?shule kama hizi muhimu kuwa na jembe!mtu akitaka kujisaidia anapewa jembe anaingia porini. Full rutuba
 
Hivi wanachojenga ni matundu ya choo au choo?shule kama hizi muhimu kuwa na jembe!mtu akitaka kujisaidia anapewa jembe anaingia porini. Full rutuba

Usiturejeshe kwanye uchafuzi wa mazingira mdau, kipindupindu hakiatuacha salama mfua za vuli zikifumua kifusi cha wale wadudu.
 
Choo cha shule ya msingi Lipangala, huko sehemu mojawapo ya Ludewa. Nashangaa hata kusafisha eneo linalozunguka choo ni:
  • Mbunge achangie?
  • Serikali ipangie bajeti?
  • Wazazi wachangie?
  • Walimu wahimizwe?
  • Kaka Mkuu na Dada Mkuu wa shule hawana akili timamu?
  • Elimu ya maisha na kujitegemea mashuleni imesitishwa?
Kwenye hiyo list yako, umesahau jambo moja kubwa na muhimu: TUNAHITAJI FEDHA ZA WAFADHILI/WAHISANI, HASA WA ULAYA. KUFANYA USAFI NI GHARAMA SANA ATI!!
 
Kwa kweli Mi hili linanishangaza sana na unawakuta Wananchi wa hapo bado wanaipigia ccm kura mpaka sasa. Ngoj wadau waje.


CC; Kwa Crashwise.
 
Last edited by a moderator:
Kwenye hiyo list yako, umesahau jambo moja kubwa na muhimu: TUNAHITAJI FEDHA ZA WAFADHILI/WAHISANI, HASA WA ULAYA. KUFANYA USAFI NI GHARAMA SANA ATI!!

Ee Bwana, umenivunja mbavu, hii inachekesha. Hata nyengo za kufyekea majani hazipo? Labda watasema shule haina zile tengo za kufyekea majani.

Wengi bado tungali na utumwa kila kitu lazima kifanikishwe toka ulaya.
 
Back
Top Bottom