Picha: Ziara ya Zitto Kabwe kanda ya Magharibi,jimbo la Igalula

Picha: Ziara ya Zitto Kabwe kanda ya Magharibi,jimbo la Igalula

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
THURSDAY, OCTOBER 10, 2013










​
Siku ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo la Igalula, wilaya ya Uyui. Tumekutana na wananchi katika vijiji vya Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa.


Tumezungumza kuhusu changamoto ya usafiri wa Reli, wafugaji kunyanyaswa na watendaji wa kata na askari kwa kunyanganywa mifugo, zao la Tumbaku, maji safi na salama na suala la jumla la Katiba na mchakato wa kuandika katiba.

Kimsingi shughuli za kiuchumi za wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na mifugo. Hata hivyo ukosefu wa miundombinu unafanya wananchi wasipate thamani ya mazao yao na jasho la kazi zao.

Nilipofika Kijiji cha Loya nimeona eneo kubwa lina miti ya mihama. Wananchi wanatumia tu mihama wakati wa njaa na mara nyingi matunda haya yanaharibika tu. Lazima matunda haya yana matumizi yake ya kiviwanda maana ‘kernel' yake ina mafuta.

Na hili ni swali aliloacha Mh Zitto Kabwe... Nani anajua matumizi ya Mihama?
MICHUZI
 
Simply Presenting - points!!!... Ingekuwa CCM hapo aaah Ungeona Mashati Mapya ya Kijani; Khanga Mpya na Tumbo zimejaa...
 
Hongera mh.Zitto sambaza elimu hadi vijijini ndani kabisa.

Ila usisahau kutuambia ahadi yako mshahara wa JK anakunja ngapi kwa mwezi,akisafiri bajeti yake ni ngapi,posho kwa ziara anavuta ngapi na kodi anakatwa ngapi.?
 
Asante mkuu kufika mitaa ya HOME, IGALULA maana yake Geuza ; Badilisha, kwa hiyo nafikiri wanyamwezi wataamua kugeuka kwa kuipa kisogo CCM ambayo imetawala miaka nenda rudi bila maendeleo ya kuonekana kwa macho.

Kuhusu matunda aina ya Mahama, haya huwa tunayatumia kwa kiasi kidogo sana wakati wa njaa, mengi huliwa na wanyama kama tembo nk, ni jamii ya nazi lakini yenyewe huiva, ukiondoa ganda lake la juu basi unakutana na Supu tamu na nzito ya njano iliyogandiana na vinyuzi vidogo vidogo.

Unaweza kukamua ile supu na ukatumia kuchanganyia kwenye uji kama kifungua kinywa, au ukalila kwa style ya kufonzya hivyo hivyo kupoza njaa kali. Wengi tuliotoka mkoa huu hatujadadisi matumizi yake hasa kwenye viwanda vya kisasa. ndiyo najifunza hapa kwamba inaweza kutengeneza mafuta ya kupikia kama yalivyo yale Mawese.

Otherwise - karibu kwetu - vipi mbona hujasifika msosi wa Tabora - Mgeni lazima ale bwana - kabla hujaondoka hakikisha unapata Ugali wa Muhogo mboga ni Nsansa au Nswalu. Kwa kifungua kinywa unaweza pata uji wa muhogo uliochangawa na asali kitafunio pata Mihogo ya aina ya Makopa!! Kama utapata Matoborwa pia si mbaya!!

Pata Mwenyeji atakueleza zaidi - Best wishes kamanda - enjoy Tabora, Mji wa watu wapole na wacheshi.
 
ninazo videos mbili za watsup za huko mpanda ZZK anatisha!
 
Mungu ampe nguvu yakuendeleza elimu ya Uraia.Hawa jamaa wa Kijana wanapenda maeneo yenye watu waisioelewa dunia inaelekea wapi na kadri muda unavyo kwenda maeneo kama hayo yanapungua kwa Kasi kwa Kazi za Makamanda kama hii Safari ya Mhe.Zitto

 
Simply Presenting - points!!!... Ingekuwa CCM hapo aaah Ungeona Mashati Mapya ya Kijani; Khanga Mpya na Tumbo zimejaa...

Hivi ina maana kila mkutano wanapata nguo mpya? Watakuwa wamejaza masanduku na makabati. Hapo bado vitumbua na maandazi na waki na maharage.
 
Hivi ina maana kila mkutano wanapata nguo mpya? Watakuwa wamejaza masanduku na makabati. Hapo bado vitumbua na maandazi na waki na maharage.

Hao wanaohutubiwa ni wapya na Unawaona wana Vitu vya KIJANI - Yeah NDIO PESA zote za MAENDELEO zinakopelekwa
 
Back
Top Bottom