Picha za ziara ya mwanamfalme wa Saudi Arabia, bandari ya Dar es salaam!

TPA

Member
Sep 28, 2016
49
71
SAUDIA-IMG-20170221-WA0018.jpg

Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Freddy Liundi (watatu kulia) akifafanua jambo kwa Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Ahmed Ben Bendar Alsedary (wapili kushoto) wakati wa ziara yake bandari hivi karibuni.

SAUDIA-IMG-20170221-WA0017.jpg

Mhandisi, Joseph Mtenga (kulia) akitoa maelezo kwa Mwanamfalme kuhusu shughuli mbalimbali za kitengo cha mafuta cha KOJ kilichopo bandarini hapo.

SAUDIA-IMG-20170221-WA0012.jpg
 
Saudi Arabia ndio wanaotesa dada zetu wanaoenda kufanya kazi za ndani huko Saudi,nasikia huwa wanawanyanganya passport,wanawalaza njaa,wanawabaka,wanawanyima mishahara yao halali na mateso mengine

Hivi Saudi huwa wanaleta bidhaa gani Tanzania ukiachilia mbali mafuta ambayo hutuuzia kiduchu?
 
Fungua uzi kwa shutuma zako, jadili kilichopo hapa
 
Alikuja kufanya nini hapo Bandarini? dhumuni la kuja hapo ni nini hasa?

Toeni Taarifa kamili.

Baada ya kutembelea hapo Alisemaje?
 
TPA muna uhakika kuwa huyo ni mwanamfalme?
maana watoto wa royal family wote ni Alsaud sio Alsedary.
Mkuu umetoa i zuri sana sana....ila Kupitia Ubalozi wao lazima wawe na Taarifa za huu ujio na Lazima balozi wa Saudia hapa TZ Ajue...ujio huu ni wa binafsi Au wa Kiserikali...
 
Saudi Arabia ndio wanaotesa dada zetu wanaoenda kufanya kazi za ndani huko Saudi,nasikia huwa wanawanyanganya passport,wanawalaza njaa,wanawabaka,wanawanyima mishahara yao halali na mateso mengine

Hivi Saudi huwa wanaleta bidhaa gani Tanzania ukiachilia mbali mafuta ambayo hutuuzia kiduchu?
Tanzania ina import 53% ya bidhaa kutoka saudia na 47% kutoka nchi zingine ,na bidhaa kubwa ni petrol..hata kama ni kiduchu fahamu Tanzania ina import 53% kutoka saudia

Top 3 ya imports.

1.Saudia
2.china
3.India

Kuhusu hayo masuala mingine huyo mwana mfalme hayamuhusu yaani recruitments zifanyike na mtu ambaye yupo sinza ,ilala na trafficking zifanywe na mtanzania apelekwe kwa MTU asiyemjua nchi ya mbali afanye kazi za ndani

Ni kama vile akina dada waliopo Guangzhou wanajiuza sasa nani wakulaumiwa serikali ya China?

Au punda wanaopeleka madawa nje wakulaumiwa Nani magu ,majaliwa??

Huyo mwanamfalme haimuhusu trafficking mnafanya wenyewe kwa siri

Yeye yanamhusu $$
 
Leta ushahidi wa hayo ndugu, maana unaandika habari za kufikirika zaidi ya ukweli, mbona hujamuhoji balozi wa marekani kwanini wanazuia raia kutoka nchi za kiislamu kwao?
Wamarekani wanazuia magaidi
 
Back
Top Bottom