GE2025 Picha za Shule maalumu za Sayansi Zilizojengwa na Mama Samia Mikoa yote Tanzania.Hapa ni Siha-Kilimanjaro

GE2025 Picha za Shule maalumu za Sayansi Zilizojengwa na Mama Samia Mikoa yote Tanzania.Hapa ni Siha-Kilimanjaro

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
79,081
Reaction score
84,973
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa jumla ya shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

Kati ya fedha hizo, jumla ya shilingi Bilioni 4.450 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Kilimanjaro, ambayo tayari imeanza kufanya kazi huku ikiendelea na ukamilishaji wa maeneo yaliyosalia.

Kati ya fedha hizo jumla ya shilingi Milioni 352.509 zimetumika kukamilisha ujenzi wa Miundombinu ikiwemo ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa, Ofisi 3 za walimu na matundu 3 ya vyoo vya walimu, Shilingi milioni 65.2 zimetumika kukamilisha ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu ya vyumba vitatu, Shilingi milioni 61.370 zikiwa zimetumika kukamilisha ujenzi wa nyumba ya afya (Sick Bay), Shilingi milioni 194.067 zimetumika kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala sambamba na shilingi Milioni 104.640 zikitumika kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mwalimu ya moja kwa mbili (2 in 1).

Shilingi Milioni 225.069 zimetumika kukamilisha ujenzi wa vyumba 4 vya maabara ya Fizikia, Baiolojia, Kemia na Jiografia. Shilingi milioni 50.871 zimetumika kukamilisha ujenzi wa matundu 16 ya vyoo sambamba na shilingi Bilioni 1.101 zikitumika kukamilisha ujenzi wa mabweni 8, Shilingi Bilioni 1.092 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Bwalo, Shilingi milioni 7.2 zimetumika kukamilisha ujenzi wa vichomea taka viwili pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa mashimo 9 ya maji taka kwa gharama ya shilingi milioni 59.631

Sambamba na fedha hizo pia katika awamu ya pili ya mradi wa SEQUIP serikali imetoa shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa 10, Mabweni 4, nyumba za walimu 3, Chumba cha TEHAMA na Maktaba.

Wakati huo huo serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule mpya ya Amali ya inayojengwa katika kijiji cha Roseline kata ya Ndumeti katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
Screenshot_20250712-105026.jpg
Screenshot_20250712-104958.jpg
Screenshot_20250712-104933.jpg
Screenshot_20250712-105648.jpg

My Take
Watoto wa kike wa Tanzania hii ni fursa yenu.
Mama Samia pekee Ndio ameweka legacy hii.
 

Majengo ni jambo lingine , na kile wanafunzi wanakipata ni jambo lingine, leo hao wanafunzi na wahitimu wa vyuo vikuu wanaambiwa waende Veta, sasa kama taifa hatuna mipango mizuri kwa hawa vijana bila kujali majengo Mzuri inasaidia nini?
 
Usipoteze mda na watu wenye tatizo la Afya ya akili
Kweli kama wewe una tatizo la afya ya akili. Unapoteza energies kumsifia mtu aliyetimiza WAJIBU WAKE?
Mbona taarifa ya mkaguzi mkuu haijasomwa bungeni? Jibu kama ulivyosifia ujenzi wa shule
 
Wewe jamaa sijui huwa unafikiri Rais huwa ana kazi gani zengine ambazo ni tofauti na hizi unazoweka, yani utafikiri hao waliyomtangulia wao shughuli zote za serikali zilisimama wakati wa uongozi wao.
 
Back
Top Bottom