Picha za maafa ya mvua Kahama

Picha za maafa ya mvua Kahama

Aksante mdau kwa uzi huu na picha za baadhi ya matukio. ..kwa waliobahatika kufika na kujionea tufani hii haina tofauti na matukio ya kutisha yaliyowahi kuandikwa kama simulizi kwenye vitabu vya dini. ..kuna familia imepoteza watoto wote, kuna familia nzima imeangamia (wazazi na watoto wote) mimea na mazao yamekaushwa na kuharibiwa vibaya. Ni pigo kwetu wana Kahama.

Mungu awape nguvu waathirika wote...na serikali ijipange kukabiliana japo kwa kutoa msaada wa mapema sio tu kwa baadhi ya sehemu bali kwa nchi nzima...janga kama hili lingeweza kutokea popote na yeyote angeweza kuwa muhanga
 
Du! Poleni sana ndugu zetu wa kahama,,Mungu awape moyo wa uvumilivu..
 
mwenyezi mungu ni mkali wa kuadhibu.acheni kuua albino mtasamehewa otherwise msubiri maafa makubwa zaidi.

Unataka useme hao watoto nao walikuwa wanaua albino?
 
kazi ya Mungu haina makosa, poleni sana wahanga wa hili janga!
 
hizi ni baadhi za picha wadau

Mkuu hii picha ya pili si ya Kahama hapo umechanganya hii picha ni ya mafuriko yaliyotokea Mto wa mbu takribani miaka mitatu iliyopita tena huyo alikuwa msaidizi wa mitambo inayolima barabara
 
si vizuri kuombea watu mabaya kwa kuwa kuna wengine hawahusiki.

KUWA:HICHO KIJIJI KILICHOPATA MAAFA YA MAFURIKO NI WATU WASHIRIKINA WAKUBWA NA WANGA WAKUBWA.

hizo habari za uhakika kuna mtu ametokea jirani na kijiji hicho ndio alivyotoririka
Kawaida mawe ya barafu yanayeyuka mara tu baada ya mvua au hata kabla, lakini haya yapo huku jua linawaka! Lakini ukubwa wa mawe yaliyoanguka...moja kg 50! Itabidi either geographers watusaidie au wanaoona mambo kwa mtazamo wa kiroho watusaidie kujua nini kimetokea na kwa nini
 
Back
Top Bottom