Kweli hili ni janga na wahanga wote poleni. Shida iliyopo ni namna jamii zetu au nchi kwa ujumla ilivyo tayari kukabili zilizara kama hili na mengine. Hakuna utayarifu wowote katika ngazi yoyote.
TMA wanalipa pango ya bilion moja kwa mwaka pale ubungo plaza ili hali hawana vyombo thabiti vya kufanyia utabiri wa papo kwa papo na kutoa taarifa kwa maeneo husika. Mvua ya mawe inaweza kuonekana hata kwenye rada, jambo ambalo walitakiwa walione hata dakika chache kabla ya maafa.
kwa upande wa wananchi, inasikitisha kuwa wahanga ni watu maskini sana. Hawana nyumba imara kuweza kuhimili hata kwa sekunde, tufani hata ya kipimo kidogo.
Tujifunze, tujiandae.
poleni sana wahanga