PICHA za CCM: CCM YAIBWAGA CHADEMA BUGARAMA, KAHAMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA za CCM: CCM YAIBWAGA CHADEMA BUGARAMA, KAHAMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 29, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  [​IMG]Kampeni za CCM za Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27, 2012 (picha: Bashir-Nkoromo blog)

  Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kuibwaga CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Udiwani uliofanyika katika Kata ya Bugarama wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

  Habari zilizopatikana zimesema, katika uchaguzi huo ulifanyika leo CCM imepata kura 1145
  CHADEMA: 772 na TADEA: 156 wagombea wakiwa Nixon Igoko (CCM) Erasmus Francis (CHADEMA) na Clement Michael (TADEA) .

  Pia habari zilizopatikana kutoka Kata ya Shinyanga mjini ambako pia uchaguzi mdogo wa Udiwani umefanyika, zimasema CCM imeshinda. Hata hivyo hatukuweza kupata mizania ya ushindi huo kwa kura.

  ---
  Chanzo cha taarifa:
  Bashir-Nkoromo blog

  [​IMG]Kampeni za CCM za Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27, 2012 (picha: Bashir-Nkoromo blog)

  [​IMG]Kampeni za CCM za Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27, 2012 (picha: Bashir-Nkoromo blog)

  [​IMG]
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Sinyanga Hamis Mgeja wakishiriki kucheza ngoma ya Baswezi kwenye mkutano wa kampeni za udiwani kata ya Bugarama mkoani humo.
  [​IMG]
  Madiwani wa Kata za Kahama wakiwa na mgombea Udiwani wa CCM, Kata ya Bugarama katika wilaya hiyo Nixon Ikoko wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za udiwani katika kata hiyo, uliohutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
  [​IMG]
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige wakati akimuombea kura mgombea udiwani wa CCM Kata ya Bugarama, kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika mji mdogo wa Bugarama.
  [​IMG]
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimnadi mgombea wa Udiwani kata ya Bugarama, Nixon Igogo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM.
  [​IMG]
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige wakiwa na watafiti wa madini kutoka kampuni ya Majordrilling, katika kijiji cha Kakola wilayani Kahama mkoani Shinyanga
  [​IMG]
  Wazee wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipohutubia mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga.[​IMG]
  Kina mama wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Kata ya Bugarama
  [​IMG]
  Mzee wa miaka 98, Nickson Toma akifuatilia kwa makini mkutano wa kampeni za udiwani Kata ya Bugarama mkoani Shinyanga uliohutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  Source:
  http://www.wavuti.com/#ixzz2AhP4louo
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ni Uchaguzi wa UDIWANI? Mnakaa chini... Mkipata USHINDI hao Mnapotea kwenda kugawana FURAHA zenu USWISI
   
 3. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,101
  Likes Received: 7,351
  Trophy Points: 280
  Mvutoless
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hao wazee sura zinaonyesha umaskini wa kutupwa ila wagombea wote wana sura za kutakata
  Hapo ni ahadi kwa ahad na utekelezaji ni sifuri
  hao wazee wataambulia kuona sura za hao wagombea na waheshimiwa mwaka 2015 watakapopita kuomba tena kura nyingine na kudanganywa tena
  Maskini Watanzania
   
Loading...