Achana na huo mpangilio wa ukaaji.. Achana na makochi mazuri na zulia jekundu.. Itazame kiroho zaidi hata kama nyuso zao hazionekani ama hazionekani vema
Ni picha iliyobeba hisia za majuto.. Wote walioko hapo walitokea majumbani kwao kwenye vitanda vyao, wakapata nafasi ya kujiandaa na kuvaa nguo nzuri na safi na kuendeshwa hadi kazini
Kisha wote wakakusanyika kushuhudia kesi ya mahabusu wa kisiasa mwenye tuhuma za uhaini akiwa katokea mahabusu bila familia yake ndugu jamaa marafiki
Akiwa na ulinzi mkali wa magereza polisi na usalama.. Cha ajabu ana tabasamu pana ana furaha ana nuru. . korti iko kimya ikimsikiliza kwa hamasa na tafakuri kuu
Linganisha maudhui ya kortini na ya hapa kwenye hii picha... Kuna ujumbe mbingu zinajaribu kutuambia.. Tuihifadhi vema hii
Baada ya court session.. Wao wamerudi majumbano kwao lakini wakiwa wamejawa fadhaa.. Huku mtuhumiwa akirudishwa rumande akiwa na tabasamu kuu
By the way! Ni nani aliamua kuvujisha hii picha? Jibu ni moja tuu... Nguvu ya asili...Ila sidhani kama kibarua chake kitasalimika!
Nature is taking its course!
Good morning TanganyikaView attachment 3390796
Unadhani watakubali?Mkuu mbona JamiiCheck walsema sio kweli?
Ukiangalia picha ya chini unamuona tena samia akiwa amekaa kwa pembeni kwenye tv (ndani) halafu ukisoma maelezo yanasema alikuwa anasikiliza bajeti akiwa ikuu ya chamwino.Unadhani watakubali?
Hahahaaaaaa!Mzee unaishi wapi mpaka unakosa taarifa sahihi kiasi hiki?
Imeelezwa sana kwamba hiyo picha ni edited
Ukweli ni kwamba walifuatilia kesi ila kwa picha pengine imehaririwaUkiangalia picha ya chini unamuona tena samia akiwa amekaa kwa pembeni kwenye tv (ndani) halafu ukisoma maelezo yanasema alikuwa anasikiliza bajeti akiwa ikuu ya chamwino.
Swali samia aliwezaje kuonekana kwenye tv na muda huohuo aaangalie mubashara?
Bado sijawaelewa hawa jamiicheck
Picha zote mbil ni edited.Ukiangalia picha ya chini unamuona tena samia akiwa amekaa kwa pembeni kwenye tv (ndani) halafu ukisoma maelezo yanasema alikuwa anasikiliza bajeti akiwa ikuu ya chamwino.
Swali samia aliwezaje kuonekana kwenye tv na muda huohuo aaangalie mubashara?
Bado sijawaelewa hawa jamiicheck
General Forums
Sports &
Entertainment
Education, Tech
& Professional
JF English Only
Forums
East African
Forums
Fichua Uovu
Stories of Change
JamiiCheck
My Account My Threads Subscribed Threads Subscribed Forums
Change Theme
Start Discussion Staff Online
Pre GE2025 POTOSHI Picha ya Rais Samia akifuatilia kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
- Thread startercurie
- Start dateYesterday at 12:00 PM
- Tagskesi tundu lissu kesi ya uhaini picha rais samia
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Jump to newSubscribe
•••
Source #1View Source #1Source #2View Source #2
Picha inaelezea vitu vingi
Tunachokijua
Tarehe 01, Julai 2025 Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu imeendelea kuunguruma huku ikirushwa mbashara kwa njia ya mtandao na vyombo mbalimbali vya habari ili kutoa nafasi kwa umma kufuatilia kinachojiri katika kesi hiyo iliyoarishwa hadi Julai 15, 2025.
Baadhi ya watumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na X walichapisha picha inayomuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na wasaidizi wake, wakionekana kufuatilia kesi inayomkabili Tundu Lissu, kupitia matangazo mbashara yaliyorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.
Je, ni upi uhalisia wa picha hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umebaini kuwa picha hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika ukurasa wa Ikulu kwenye mtandao wa X tarehe 13, Juni 2024.
Rais Samia alikuwa akifuatilia Bunge la Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2024/25 kwa njia ya runinga akiwa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma. Hotuba hiyo ilikuwa ikisomwa bungeni na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Picha hiyo imepotoshwa kwa kubadilishiwa picha ya Televisheni, ambapo imeondolewa iliyokuwa ikonesha Televisheni ya Taifa iliyokuwa ikirusha matangaza ya bajeti kuu ya serikali 2024/25 na kuweka picha ya matangazo ya ITV inayohusu matangazo mbashara ya Kesi inayomkabili Tundu Lissu
Attachments
Acha ushamba zile ni picha mbili tofauti upande mmoja ni Mwigulu alafu upande mwingine wameonyesha Samia akifuatilia bajetiUkiangalia picha ya chini unamuona tena samia akiwa amekaa kwa pembeni kwenye tv (ndani) halafu ukisoma maelezo yanasema alikuwa anasikiliza bajeti akiwa ikuu ya chamwino.
Swali samia aliwezaje kuonekana kwenye tv na muda huohuo aaangalie mubashara?
Bado sijawaelewa hawa jamiicheck
Sawa mjanja.Acha ushamba zile ni picha mbili tofauti upande mmoja ni Mwigulu alafu upande mwingine wameonyesha Samia akifuatilia bajeti
Hilo picha nami nimelliona, nikataka kujuwa maana yake ni nini hasa?Achana na huo mpangilio wa ukaaji.. Achana na makochi mazuri na zulia jekundu.. Itazame kiroho zaidi hata kama nyuso zao hazionekani ama hazionekani vema
Ni picha iliyobeba hisia za majuto.. Wote walioko hapo walitokea majumbani kwao kwenye vitanda vyao, wakapata nafasi ya kujiandaa na kuvaa nguo nzuri na safi na kuendeshwa hadi kazini
Kisha wote wakakusanyika kushuhudia kesi ya mahabusu wa kisiasa mwenye tuhuma za uhaini akiwa katokea mahabusu bila familia yake ndugu jamaa marafiki
Akiwa na ulinzi mkali wa magereza polisi na usalama.. Cha ajabu ana tabasamu pana ana furaha ana nuru. . korti iko kimya ikimsikiliza kwa hamasa na tafakuri kuu
Linganisha maudhui ya kortini na ya hapa kwenye hii picha... Kuna ujumbe mbingu zinajaribu kutuambia.. Tuihifadhi vema hii
Baada ya court session.. Wao wamerudi majumbano kwao lakini wakiwa wamejawa fadhaa.. Huku mtuhumiwa akirudishwa rumande akiwa na tabasamu kuu
By the way! Kwanini hili litokee? Jibu ni moja tuu... Nguvu ya asili...!
Nature is taking its course!
Good morning Tanganyika
Haijalishi!