SI KWELI Picha ya Rais Museveni akiwa amezidiwa ni ya kweli?

SI KWELI Picha ya Rais Museveni akiwa amezidiwa ni ya kweli?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Museveni mahututi.jpg
 
Tunachokijua
Yoweri Museveni ni Rais wa Uganda ambaye amekuwa akiongoza taifa hilo kuanzia mwaka 1986. Museveni alichaguliwa tena mwaka 2026 kwa awamu nyingine tena na kuendelea kumfanya kuwa miongoni mwa Marais walitawala kwa muda mrefu zaidi kutokea barani Afrika.

Madai

Kumekuwa na picha inayosambaa kupitai mitandao ya kijamii ikiwemo X na Facboook ikimuonesha Rais wa Uganda Yoweri Musevi akiwa katika hali mbaya ya kiafya akipumulia mashine.

Mtumiaji mmoja wa X alichapisha taarifa hiyo na kuandika ujumbe unaosomeka:

"Bundi yupo mlangoni kwa majirani"

Uhalisia wa picha hiyo ni upi?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha hiyo si halisi. Kumekuwa na taarifa zinazosambaa mwishoni mwa mwezi Machi, 2026 kuhusiana na hali ya Mama Janeti Museveni, mke wa Yoweri Museveni ambayo pia si ya kweli na baada ya taarifa hizo zikaibuka tena taarifa kumuhusu Yoweri Museveni.

Hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha kuhusu hali mbaya ya Rais Museveni. Pia hakuna taarifa kutoka Ikulu ya Uganda ama chanzo chcochote kutoka serikali ya Uganda kueleza kuwa hali ya Rais Museveni ni mbaya.

Picha inayosambaa inamuonesha Rais Museveni akiwa kitandani huku akipumulia mashine akiwa amezungukwa na waatalamu wa Afya pamoja na Mkewe Janeti Museveni pamoja na Mwanwe Jenerali Kainerugaba Muhozi imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde.

Pamoja na mapungufu mengine, ufuatiliaji kwakutumia nyenzo ya kidigitali ya Hive Moderation inabainisha kuwa picha hiyo ina viashiria vya kutengenezwa kwa AI kwa takribani 87%.
1774945633256-png.3564939
Back
Top Bottom