Muju4
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 5,322
- 7,161
Mkuu ulibahatika kumsikia Mwigulu wakati akitangaza nia? hii jamani ni kuwa betray watanzania kwasababu wakati watoto wao wakisoma shule ambazo wewe unaziita St. Kayumba wao wanasomesha watoto International school hauoni kuwa hili ni tabaka???.. Hivi unafikiria waziri huyu anaesomesha watoto huko atakuwa na uchungu na watoto wa wanyonge??? hebu jaribu kuufahamu uzalendo kwa maana na vitendo maana huyu ni kiongozi anatakiwa a lead by example
Kwani UZALENDO una maana gani??????
Kutumia bidhaa au huduma za ndani ya nchi/haijalishi zina ubora ama la?
Okey, ampeleke kijana wake St Kayumba, je huko St Kayumba vifaa vyote watumiavyo kwa kutoa elimu vinatengenezwa nchini? Lakini pia hizo fedha atakazozi-save baada ya kutompeleka kijana wake shule za gharama atazitumiaje tumuone ni MZALENDO??? je akizitumia kwa kuongeza mjengo mwingine wa maana wenye thamani kutoka ulaya au kuagiza gari nyingine toka Ulaya, hapo ndio atakuwa MZALENDO?????
UZALENDO ni nini sasa????
Mimi nadhani picture hii ukiitafsiri kwa lugha ya KIZALENDO sidhani kama tutapata majibu zaidi ya kuwa perplexed tu, viongozi wengi tu nchi hii na hata Africa kwa ujumla baadhi ya ngazi za elimu yao wameipatia ULAYA kwenye elimu bora huko Mf Nyerere n.k na bado waliweza kuziletea nchi zao manufaa (Je kutotumia huduma ya elimu ya ndani hawakuwa wazalendo ???, lakini hii huduma nzuri ya elimu waliyoipata nje ya nchi zao ndio imewafanya/wawezesha wafanye mambo makubwa katika nchi zao)
Kwa mfano huyo kijana wake akamaliza hapo na matokeo mazuri (kwa sababu shule ni nzuri) yatakayomuweza kuwa admitted katika prestigious universties ambako atapata elimu bora kisha kuja kuajiriwa na serikali, akaitumia elimu na ujuzi wake vizuri kuwatumikia wananchi wa Taifa la Tanzania, je hatokuwa MZALENDO??
UZALENDO ni nini sasa!!!??