Picha ya kutisha: Simba wa kushangaza auawa Marekani

Quickly

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,056
649
Simba wa kushangaza aliyeuawa Marekani

12 Januari 2016
160110180321_idaho_lion_624x351_ap.jpg

Simba wa milimani aliyeuawa katika jimbo la Idaho, nchini Marekani ameshangaza wengi kutokana na hali kwamba alikuwa na meno ya ziada kichwani.

Meno hayo kamili yanachomoza kutoka kwenye paji la uso na kuonekana kama pembe.

Simba huyo aliuawa na wawindaji walioidhinishwa tarehe 30 Desemba.

Idara ya Wanyamapori na Samaki ya Idaho imesema meno hayo huenda ni masalio ya pacha ambaye labda alifariki akiwa tumboni, au labda inatokana na saratani.

Wataalamu wa vimbe katika jimbo hilo wanasema hawajawahi kuona ulemavu wa aina hiyo awali.

Simba huyo aliwindwa na kuuawa baada ya kumshambulia mbwa karibu na mji wa Weston. Mbwa huyo alinusurika lakini mwindaji akatumwa kumuwinda simba huyo na kumuua.

Afisa wa uhifadhi wa wanyama alikagua mzoga wa simba huyo kama ilivyo sheria na ndipo akagundua meno hayo.

Mnyama huyo pia alikuwa na masharubu kwenye paji la uso kushoto.

Simba wa kushangaza aliyeuawa Marekani - BBC Swahili
 
Duuuu kweli wa kushangaza,kumbe hadi marekani kuna simba? Nilijua ni Africa tu hapo ndipo nakubaliana na wanasayansi kabla ya big bang kulikuwa hakuna hayo mabara yote yalikuwa yameungana.
 
Duuuu kweli wa kushangaza,kumbe hadi marekani kuna simba? Nilijua ni Africa tu hapo ndipo nakubaliana na wanasayansi kabla ya big bang kulikuwa hakuna hayo mabara yote yalikuwa yameungana.
Wanyama mfano wa simba wapo aina nyingi kama Puma,Panther,Mountain Lion nk wa America sio kama hawa wetu
 
Duuuu kweli wa kushangaza,kumbe hadi marekani kuna simba? Nilijua ni Africa tu hapo ndipo nakubaliana na wanasayansi kabla ya big bang kulikuwa hakuna hayo mabara yote yalikuwa yameungana.
Wapo lakini si sawa na hawa simba wa huku afrika, ni aina nyingine kabisa na wao ni wadogo kimaumbile na kiuwezo ukilinganisha na simba wa huku, wanawaita mountain lions au cougars au panthers.
 
Back
Top Bottom