Warangi na Wasi wakija mjini wote wanajiita Warangi. Lakini Kwa hakika warangi hasa ukiwaona hawana tofauti yeyote na wahabeshi kwasababu wote wana asili inayofanana. Wakati Fulani nilipokuwa Ethiopia niliwahi kujisahau na kufikiri kuwa niko Kondoa maana ni warangi kwisha kazi.
Basi hawa jamaa asili yao ni Saudi Arabia na sababu ya ukabila huko walisafiri kwa miaka mingi kuja kusini na wakawa wanaacha baadhi yao njiani waliokuwa wanashindwa kuendelea na safari. Walipofika maeneo ya kanda ya kati wakakuta hawakubaliliki na wenyeji waliokuwa wanaitwa Waharagwa. Hivyo wakapigwa vita sana hadi wakaamua kurudi walikotoka. Lakini walipofika huko Saudia wakakuta kuna dini mpya na wao hawakubaliki na dini yao ya kuabudu miti na mawe na hawakukubali kuingia dini mpya ya uislamu. Mwisho wakaona bora warudi huku kwenye vita na waharagwa. Wakarudi na kupambana na mwisho wakaishi pamoja na wenyeji wao waharagwa.