nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
* CCM ZAWADI ZIKO WAPI? NAPE ALIKUWA SINGIDA ALIONDOKA NA ZAWADI ZOTE?
Mgeni rasmi Katibu wa Uchumi na Fedha Taifa wa CCM Mwigullu Nchemba (Mb) akizungumza na wana CCM na wananchi wa kata ya Itigi na Majengo katika hafla ya mapokezi ya kumpongeza Mbunge Lwanji baada ya kushida kesi yake ya kupinga ushindi wake.
Mbunge wa jimbo la Manyoni Magharibi (CCM) mkoani Singida Mh. John Lwanji amewataka vijana kujiunga kwenye vikundi vya SACCOS ili kujijengea mazingira mazuri ya kukopesheka na taasisi za kifedha.
Mh. Lwanji amesema vijana wakipata mikopo hiyo isiyokuwa na masharti magumu, wataboresha kwa kiwango kikubwa hali zao za kiuchumi na kwa njia hiyo hawatakuwa tena madaraja ya baadhi ya watu wasiokuwa na sifa za uongozi ,kuwatumia kufanikisha malengo yao binafsi.
Mbunge huyo amesema hayo wakati akizungumza kwenye mapokezi makubwa yaliyoandaliwa na wana CCM wa kata ya Itigi na Majengo kwa ajili ya kumpongeza, baada ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya kupinga ushindi wake kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Dodoma Mei 20 mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Mh. Lwanji alitumia fursa hiyo kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpigania wakati wote kesi yake ya kupingwa ushindi wake ilipokuwa ikiendelea na hatimaye kuibuka kidedea kwa kesi hiyo kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Dodoma.
"Huyu mtu ni ndugu yangu (binamu),nimemgaragaza kwenye kura za maoni za CCM, akaamua kutimkia CHADEMA, huko nako nikampiga mwaleka wa nguvu, akaona haitoshi, akakimbilia mahakamani, huko nako kashindwa kupata ushindi, Sasa nadhani atakata rufaa mbinguni, lakini huko ni mpaka mtu ufe ndio unaweza kupata nafasi ya kukata rufaa", alisema na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi.
Mh. Lwanji alifunguliwa kesi ya kupinga matokeo namba 2/2010 na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia tiketi ya CHADEMA Donald Madeje Lupaa. Kesi hio imetupiliwa mbali na Jaji Mary Shangali kwa madai kwamba ilifunguliwa kwa makosa, kwani sheria iliyotumika kuifungua ilikuwa ni ya mwaka 1971 ambayo ilishapitwa na wakati kufuatia sheria mpya ya mwaka 2010.
Mbunge Lwanji akipokelewa na wana CCM wa kata ya Itigi na Majengo.