Tausi Mzalendo
JF-Expert Member
- May 23, 2010
- 1,470
- 722
Kila mtu anakula ofisini kwake. wabunge wanajipitishia posho kubwa, hawa hawana mahali pa kupata posho. Posho yao ni hiyo!!!! ni sahihi kabisa. Songa mbele polisi kula rushwa kwa kwenda mbele!!!!!
Sasa wale nini na maisha magumu kama mawe?
Kwa namna maisha yalivyo ghali watu wenye kipato kinachoweza kuitwa cha chini lazima wafanye mipango mingine ili kutosheleza mahitaji ya familia. Inasikitisha ila hiyo ndio hali halisi. . .
Traffic waliopo barabara kuu eneo la Bwawani Chalince-Morogoro wakipokea rushwa. Raia mwema aliyesafiri na kuwanasa hawa traffic wakipokea rushwa alikaa kwa muda katika eneo hili na kuwapiga picha. Vijana walioandaliwa wakijishughulisha kama wanasafisha gari ili kuwa kizingizio huku wao wakiendelea na zoezi la kukabidhiana rushwa. Askari hao baada ya kubaini mdau huyo amewapiga picha walimfuata ndani ya bus alilokuwemo na kuanza kupambana naye lakini mpiga picha aliwazidi ujanja na kuwashinda. Kairusha picha hii kupitia mdandao wa Michuzi.
Nakubaliana na Paka jimmy kwa asilimia 95.9 sioni kama stori inaendana na pichaKwa picha hiyo hakuna kitendo chochote kinachoonyesha transfer ya cash au kitu chochote cha aina ya rushwa kati ya traffic na hao raia! Mleta mada umejuaje kuwa rushwa ilitolewa hapo?...au unahisi tu kutokana na default value juu ya tabia ya hawa ndugu? Ni rushwa gani inatolewa mbele ya kundi la watu namna hiyo? Halafu kwani traffic police hawana ndugu na jamaa zao wanaoweza kuongea nao kama hivyo pichani? Mi naona ni shughuli za kawaida tu zinaendelea hapo, kuna kijana anaosha gari, wengine wanachati tu na maafisa hao, lakini hakina m'badilishano wowote wa pesa hapo! Mleta mada alitakiwa apige na picha labda inayoonyesha gari fulani imepaki kwa kukamatwa, hapo ndipo ingeleta ushawishi wa kuamini kuwa madereva wake ndiyo wanamsaundisha traffic, lakini kwa mazingira hayo. hakuna dalili hizo!
Gerry Muro kwa mtindo huu alisukiwa zengwe karibu atemeshwe uhuru wake aitwe mfungwa!!!! Vitu vingine kuweni realistic issue iweze kueleweka vizuri!!! Lakini kwa mazoea ya Trafic wa TZ mtu anaweza kutafsiri picha hiyo vyote apendavyo!!!Hii kapiga Gerry Muro nini?
Traffic waliopo barabara kuu eneo la Bwawani Chalince-Morogoro wakipokea rushwa. Raia mwema aliyesafiri na kuwanasa hawa traffic wakipokea rushwa alikaa kwa muda katika eneo hili na kuwapiga picha. Vijana walioandaliwa wakijishughulisha kama wanasafisha gari ili kuwa kizingizio huku wao wakiendelea na zoezi la kukabidhiana rushwa. Askari hao baada ya kubaini mdau huyo amewapiga picha walimfuata ndani ya bus alilokuwemo na kuanza kupambana naye lakini mpiga picha aliwazidi ujanja na kuwashinda. Kairusha picha hii kupitia mdandao wa Michuzi.
Kwa picha hiyo hakuna kitendo chochote kinachoonyesha transfer ya cash au kitu chochote cha aina ya rushwa kati ya traffic na hao raia!
Mleta mada umejuaje kuwa rushwa ilitolewa hapo?...au unahisi tu kutokana na default value juu ya tabia ya hawa ndugu?
Ni rushwa gani inatolewa mbele ya kundi la watu namna hiyo?
Halafu kwani traffic police hawana ndugu na jamaa zao wanaoweza kuongea nao kama hivyo pichani?
Mi naona ni shughuli za kawaida tu zinaendelea hapo, kuna kijana anaosha gari, wengine wanachati tu na maafisa hao, lakini hakina m'badilishano wowote wa pesa hapo!
Mleta mada alitakiwa apige na picha labda inayoonyesha gari fulani imepaki kwa kukamatwa, hapo ndipo ingeleta ushawishi wa kuamini kuwa madereva wake ndiyo wanamsaundisha traffic, lakini kwa mazingira hayo. hakuna dalili hizo!