Picha/sura ya bakhresa

Status
Not open for further replies.
Wapo wengi, ila dini yetu hairuhusu waweke sura zao hadharani na hairuhusu wafanye kazi kama kaka zao!

Nilidhani hawa ni waislam! Kama ni waislam nilisoma mahali kuwa mke wa mtume bi. Hadija alikuwa mfanyabiashara. kama mke wa mtume amefanya biashara basi kukataza wanaweke kufanya biashara au kazi sio swala la dini bali ni la tamaduni fulani za jamii husika.
 
kwani huyu bwana ni mhindi?
Lol! Na wewe banaa! Wahindi hawauzi sura wanapiga kazi! Jamaa akienda ulaya hana nafasi ya kupiga picha na maceleb kama rais wako, anaangalia chikilimu za kisasa alete kwao!
 
Ni kweli huyu bwana ni mkimya sana "kwa sasa".

Ni kweli ameanza na biashara ndogo ndogo sana.

He is probably the richest man in TZ.

Huko nyuma kabla hajainukia hakuwa mkimya. Alikuwa ni mdhamini mkubwa sana wa Simba.

Miaka ya themanini wakati Mwinyi akiwa rais, alikamatwa na pembe za ndovu. Kesi yake ikazimwa zimwa, nafikiri kwa sababu ni mzenji. Tokea hapo akawa mkimya mpaka leo. Hata support ya Simba ikaisha.

All said, jamaa ni mfanyabiashara mzuri sana, namkubali. Amenifurahisha kuanzisha utengenezaji wa juice mbalimbali. Hizi juice zimeua soko ya juice za kutoka Kenya na Sfrica Kusini.
 
Jamaa amekamata soko la kusini mwa Jangwa la sahara Billie
 
Last edited by a moderator:
Huyo siyo Bakharesa ila ni Said Bakharesa na Wanawe, tunataka tuone picha ya Bakharesa mwenyewe.

Huyo siyo Bakharesa ila ni Said Bakharesa na Wanawe, tunataka tuone picha ya Bakharesa mwenyewe.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Taifa ya Misaada Ya Kibanadamu Somalia muda mfupi baada ya kuizindua rasmi ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Wajumbe wa kamati hiyo ambayo jina lake rasmi ni Kamati ya Okoa Maisha Somalia walimchagua Bwana Reginald Mengi(Watatu kushoto) kuwa mwenyekiti.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Bwana Haruna Zakharia, Said Bakhresa,Reginald Mengi,Gulam Dewji na Balozi Said Shamo.
 
chairmanImgThumb1.jpg
SAID SALIM AWADH BAKHRESA, Chairman, Bakhresa Group of CompaniesSAID SALIM AWADH BAKHRESA is the founding father and the Chairman of the Bakhresa Group Of Companies. He is a well-known industrialist in the mainland of Tanzania and island of Zanzibar. With a humble beginning as a small restaurateur in seventies, he created the business empire within a span of three decades. He is the mastermind behind the success of all the businesses within the group. His vision and excellent managerial skills contributed to the growth of this group to great heights.Mkuu.@Billie

mzizi mkavu ucpende jaza server yetu bure kwa maelezo mengi kwa kitu kisichotakiwa,mwanzisha uzi ameomba mwenye picha au sura ya bakhresa amwekee ,weye unakuaja na mastory mareeefu,picha yake ingetosha tu ,nyie ndo mnaofail mitihani kwa kujibu msichoulizwa...aaaargh
 
[h=4]Topic Information[/h][h=5]Users Browsing this Topic[/h]There are currently 59 users browsing this thread. (20 members and 39 guests)




Mkuu Billie wala hujakosea kuuliza, swali lako linaonyesha umuhimu wake huyu bwana, kwa idadi ya waliopo kwenye mada yako inaonyesha wazi kuwa ni watu wengi walikuwa hawaitambui sura ya huyu mlipa kodi wetu....
 
Last edited by a moderator:
Toka tupate uhuru Mwalimu Nyerere alikuwa anatuambia kuwa tuna maadui wakubwa watatu; UJINGA,UMASKINI na MARADHI [ Bakhressa alilielewa hilo na ndio maana amewasomesha wanae vizuri]!! Hivyo basi katika utawala wake Mwalimu alihakikisha kuwa sera za nchi zilielekezwa kwenye kuimalisha shule kama njia ya kupigana na ujinga na pia umaskini kwani elimu inasaididia uelewa wa mambo hivyo kuwakwamuwa watu na umaskini kiurahisi. Alitambua pia kuwa kwa kuwaelimisha watu na kuwapatia huduma za afya wananchi wangeweza kuepukana na maradhi!! Hawa maadui watatu bado tunao na kitu cha kushangaza watawala wa leo hawaoni umuhimu wa Elimu wala watu kuwa na afya bora na ndio maana hawawathamini waalimu na madaktari watu ambao ni muhimu kupigana na maadui hao!! Viongozi wetu priority yao ni kushinda chaguzi za kisiasa na ndio maana wamewekeza pesa nyingi ambazo zingetumika kwa elimu na afya kwenye siasa /yaani kuwaridhisha the political class especially wabunge, kuvikandamiza vyama vya upinzani na kuthibiti uhuru wa vyombo vya habari na hasa magazeti!! Such a priority is wrong for the development of the country because it leads to the allocation of resources to non priority areas.
 
Nimependa CV za wanawe...wamekwenda shule...hii ndio kitu inakosekana kwa matajiri wengi..
inanipa picha ya upande mwingine kwamba tuende tuendako lakini bado mfumo wa shule ulio mzuri unapatikana Magharibi (US na UK)
 
Huu nao uvivu, kuwaza bakhresa ana sura gani. Umeenda google ukakosa result? Changamsha kichwa mkuu!

Hawa si ndio walewale.., shangaa JF anaweza kupost thread but kutafuta elimu zaidi through google hawazii! Siku hizi tuna namna nyingi sana za kujielemisha but wabongo tupotupo tu! Kazi kweli kweli.
 
ukienda kwenye website ya kampuni zake unamkuta kajaa tele na wanae na wadogo zake,ninachofurahia ni kwamba wanae wamesoma vizuri sana na kila biashara ia managing director wake,chain yake ya utawala wa biashara zake iko poa.jamaa hawa ni wabunifu mno!

nami nimejifunza hapa,,,,,,sasa ndo tujiulize inakaje watoto wa kiaskin hata wapatapo fursa hawasomi,,,,,????halafu hawa wamesoma kwa MALENGO SANA,,,,,,,
 
inanipa picha ya upande mwingine kwamba tuende tuendako lakini bado mfumo wa shule ulio mzuri unapatikana Magharibi (US na UK)

nakubaliana na wewe case study hawa watu wake bakhresa,ila hata malaysia nako mdau
 
[h=4]Topic Information[/h][h=5]Users Browsing this Topic[/h]There are currently 59 users browsing this thread. (20 members and 39 guests)




Mkuu Billie wala hujakosea kuuliza, swali lako linaonyesha umuhimu wake huyu bwana, kwa idadi ya waliopo kwenye mada yako inaonyesha wazi kuwa ni watu wengi walikuwa hawaitambui sura ya huyu mlipa kodi wetu....

Asante kwa uelewa wako mzuri akili yako malidadi sana
 
Last edited by a moderator:
Hawa si ndio walewale.., shangaa JF anaweza kupost thread but kutafuta elimu zaidi through google hawazii! Siku hizi tuna namna nyingi sana za kujielemisha but wabongo tupotupo tu! Kazi kweli kweli.

Sina ushamba wa kugoogle ndugu ila ngoja nikuache tusije anza kutukanana bure.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom