PICHA: Rais Samia akiweka Shada la maua kwenye kaburi la Hayati Dkt Magufuli

PICHA: Rais Samia akiweka Shada la maua kwenye kaburi la Hayati Dkt Magufuli

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
36,354
Reaction score
23,760
Ndugu zangu Watanzania,

Mama yetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge ameweka shada la Maua kwenye kaburi la Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Awamu ya Tano.

👉DKT. SAMIA AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA HAYATI MAGUFULI

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ambaye pia ni Mwenyekiti wq Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu Jioni Oktoba 13, 2025 amefika Chato Mkoani Geita nyumbani kwa familia na sehemu alipozikwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na kuweka shada la maua pamoja na kumuombea dua ya kuendelea kupumzika kwa amani.

Dkt. Samia amefika kwenye Makaburi hayo ya familia Rubambangwe Chato akiambatana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt. Asha- rose Migiro na baadhi ya wanafamilia mara baada ya kuhitimisha Mkutano wake wa kampeni Katika Wilaya hiyo ya Chato Mkoani Geita.

Hayati Dkt. John Magufuli alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Tano wa Tanzania, akiongoza serikali kwa miaka yote mitano ya awamu ya kwanza na takribani mwaka mmoja katika awamu ya pili akiwa na Makamu wake kipindi hicho Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mpaka pale mauti ilipomfika Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar Es Salaam alipokuwa akitibiwa, akiweka rekodi enzi za uhai wake kama Rais wa kwanza wa Tanzania kumuamini na kumteua Makamu wa Rais mwanamke katika Historia ya Tanzania.
Screenshot_20251013-193531_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Wafu wakizikana haliwahi kuwa ni kosa katika ulimwengu wa kiroho.
 
Unanaa tu

Kwani hiyo inatupa chakula?
Nani akuletee chakula wakati wewe umekaa umebweteka na kupiga Umbeya tu kwenye vibaraza vya majirani. Fanya kazi kwa bidii ,juhudi na kujituma na ndipo utapata chakula cha aina yoyote ile utakacho.
 
Back
Top Bottom