Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa na jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.
Ametumia siku ya leo katika kuboresha taarifa zake katika daftari la mpiga kura na hatimae kupatiwa Kadi ya mpiga kura. Ambapo ametumia nafasi na fursa hiyo kuwataka watanzania kutumia fursa hiyo kuboresha taarifa zao ili kupata nafasi ya kuchagu viongozi wanaowataka na watakao weza kuwaletea maendeleo na kuwahudumia vizuri.
Ambapo Rais wetu Mpendwa amewataka watanzania wajiandikishe kwa wingi na kuweza kuirejesha madarakani serikali inayowaletea maendeleo.
Kwa upendo na unyenyekevu mkubwa sana kama ilivyo kawaida kwa Rais wetu Mpendwa amewasihi sana watanzania kutopoteza haki yao ya kuchagua viongozi watakao weza kuwaongoza. Ambapo wananchi mbalimbali ambao walifurika eneo hilo wameonyesha kumuunga mkono Rais wetu kipenzi na kuwa tayari kujiandikisha na kushiriki uchaguzi kikamilifu kabisa.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.