Picha: Ofisi ya CCM Mbinga yachomwa Moto

Picha: Ofisi ya CCM Mbinga yachomwa Moto

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=3][/h]

[h=1]
[/h]

Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambao hawapo pichani.
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi akionyesha sehemu iliyoanzia moto kuwaka na kukamata pazia.
Kama unavyoona katika picha hapo ni ndani ya ofisi baada ya moto kuwaka.
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi anayeonekana katika picha akitoa maelezo kwa nje ambapo walimwaga mafuta aina ya petroli dirishani na kuwasha moto.
Huu ni mlango uliomwagiwa mafuta katika upenyo kisha kuwashamoto ambao haukuleta madhara kama walivyo kusudiwa na wachomaji.


Watu wasiojulikana wamechoma moto jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma tukio lililotokea Juni 21 mwaka huu majira ya usiku pamoja mlinzi wa ofisi hizo kuwepo katika eneo hilo la ofisi mpaka majira ya saa 12 asubhi na hakuweza kutambua kutokea kwa kitendo hicho kilichofanywa na watu wasiojulikana usiku huo.



Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Juni 21 mwaka huu ambapo watu wasiojulikana walichoma moto moja ya jengo la ofisi za chama hicho wilayani humo moto ambao ulielekelezwa katika chumba cha ofisi ya katibu ambapo walivunja vioo na kuchoma moto mapazia lakini kabla hawajachoma vitu vilivyokuwemo ndani walikimbia na kuacha dumu lililokutwa likiwa na mafuta aina ya petroli.


Alisema kuwa mpaka sasa hakuna hisia zozote zinazohusiana na tukio hilo ingawa uongozi wa chama cha mapinduzi wilayani humo umeshatoa taarifa kwenye vyombo ya ulinzi na usalama ambavyo vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.



Katika hatua nyingine hali ya sintofahamu imejitokeza katika uchaguzi wa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga baada ya halmashauri hiyo kugawanywa na kuzaliwa kwa halmashauri mpya ya wilaya Nyasa kwa kuibuka kwa vitendo vya hujuma vinavyodaiwa kufanywa dhidi ya mgombea mmoja wa nafasi ya mwenyekiti jina lake kuenguliwa katika mazingira ya kutatanisha na kuzua maswali mengi miongoni mwa madiwani wa halmashauri pamoja na wananchi na kutaka uchaguzi huo usifanyike mpaka majina yote matatu ya wagombea yawepo.



Mmoja wa wananchi wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Mbinga ambaye pia ni katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi wa kata ya Mbinga mjini Monika John alisema kuwa hizo ni dalili za kuwepo kwa njama za wazi za kupanga safu ya uongozi ambao siyo chaguo la walio wengi bali ni chaguo la baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo kwa masilahi yao.



Akizungumzia hali hiyo katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbinga alisema kuwa uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo hufanywa kwa kuzingatia kanuni za chama na wenye jukumu la mwisho la uteuzi ni uongozi wa chama ngazi ya mkoa na yeye si msemaji wa maamuzi ya ngazi mkoa ingawa amepokea tarifa ya kusitishwa kwa uchaguzi huo mpaka taarifa nyingine itakapotolewa na ofisi ya chama ngazi ya mkoa.




Picha na Habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com
 
Pakishapigwa dili, suluhisho ndo huwa hilo.... ila kabla ya kuchoma huwa wanahakikisha nyaraka zote zinazoweza kubumbulua dili zinachomewa nyumbani. Maana zikianchwa ziungue na makaratasi mengine zinaweza salimika bureee...!!!!
 
...jamaaa wameshachukua mzigo wanataka kupoteza ushahidi...lohhh...
 
Pakishapigwa dili, suluhisho ndo huwa hilo.... ila kabla ya kuchoma huwa wanahakikisha nyaraka zote zinazoweza kubumbulua dili zinachomewa nyumbani. Maana zikianchwa ziungue na makaratasi mengine zinaweza salimika bureee...!!!!

Unadhani kwa nini wachome ofisi wakitie chama hasara? Tatizo letu huwa tunatatua matatizo yetu kwa njia isiyofaa.
 
Huchelewi kusikia Chadema

"To know the enemy is half the victory"
 
kwanini hawakuwachoma moto na hao viongozi wao? tukazika yakaisha?
 
Badala ya kufanya retirement ya pesa mnachoma moto vijengo vyenu,wezi wakubwa'
 
Macho yangu haya, mi hiyo picha namwona Nape katia ushungi na kisketi. Dah!
 
Uovu waliouanza ccm watakula matunda yao baada ya kuiva, ni mbegu waliyokwisha ipanda tayari na hakika hawataacha kuvuna.

Proverbs 11: 27 ''Whoever seeks good finds favor, but evil comes to one who searches for it''
 
Hawa magamba sina huruma nao. Ofisi zao sehemu nyingi zimejengwa ktk viwanja walivyopora.
 
Hebu acheni utani. Ofisi ichomwe moto halafu hata pazia na vitambaa vya mezani visiungue! Au ni vya chuma?
 
Back
Top Bottom