Picha: Magufuli atinga jikoni kusonga ugali

Campaign manager wa Magufuli ni Lusinde, unategemea nini?
 
inaonekana picha ya zamani,kumbe vitendo kwa mifano hakuanza leo
 
Mh:Lowassa alipokwenda sokoni na kunywa chai na wamachinga mlikuja juu na kuanza kutoa povu kuwa siku sote alikuwa wapi oooh ni ulaghai tu hana lo lote. Sasa na mimi nauliza tu kuwa siku zote Mh: Magufuli alikuwa wapi leo ndo ajue kuwa kuna akina mama ntilie wanahutaji kusaidiwa kusongewa ugali na kuwa karibu nao? Au ndo ule msemo usemao KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHARISHA? SIASA NYINGINE BWANA NI ZAIDI YA MATATIZO.
 
Duh..... mgombea wa magamba kweli amekuwa full comedian, mara kupiga push ups jukwaani, kwa kujiweka fit kama vile kaambiwa kule Ikulu anaenda kuwa bondia!

Sasa ameanza kufanya mazoezi ya kupiga ugali, utadhani kaambiwa kuwa moja ya jukumu lake kubwa atakapotinga Ikulu itakuwa kuwasongea ugali Staff wa Ikulu!

Hilo ndiyo tatizo la kuwa na timu ya kampeni ambayo 3/4 yake imejaa wasanii wa bongo muvi na bongo flava.
 
Kwani hajui!? huko nyumbani kwake janet akimwambia nisaidie kuosha vyombo, atarusha ngumi huyo..!!
 
Magufuli jembe na mbunifu.
Hiyo ni namna alivyo karibu na wananchi.
 
Ebu atoe hilo igizo lake, hii kuongozana na wasanii imemfanya kubuni maigizo tofauti tofauti. anafikiri atamhadaa nani? Mke wake mwenyewe amemsahau hadi akumbuki kumtambulisha unafikiri atawakumbuka wanawake wa TZ?
 
bado kuoga hadharan au bafu ya passport size
 

Hii ni picha ya wakati wa Semina ya viongozi wa serikali za mitaa waliochaguliwa mwaka jana.
 
Lowassa yeye hajui shida za wananchi kwa kuwa amezaliwa New york.

Haya maigizo mwisho 25 oct Lowassa tutakavyompa kura
 
Kama ikitokea akawa rais watz tutarajie aibu, nafikiri hata jk alipo anaanza kuhisi hiyo hali.
 

Kupika Na Urais Kuna Uhusiano Gani?

Alikuwa wapi zamani?kumbuka ikulu sio sehemu ya kusonga ugali.


swissme

Full comedian, na sisi mateja huku ili tumpe kura zetu aje ale unga pamoja nasi.

Ebu atoe hilo igizo lake, hii kuongozana na wasanii imemfanya kubuni maigizo tofauti tofauti. anafikiri atamhadaa nani? Mke wake mwenyewe amemsahau hadi akumbuki kumtambulisha unafikiri atawakumbuka wanawake wa TZ?

Picha ya zamani hii, wakati ambao kulikuwa hakuna kampeni za urais
 
“A vote is like a rifle: its usefulness depends upon the character of the user ,vote for magufuli for better development sustanability and well being of Tanzania people

Kwa kuwa kura ni kama bunduki,sasa imewageukia CCM na JPM yake,ahadi zao hazitekelezeki.
 
Full comedian, na sisi mateja huku ili tumpe kura zetu aje ale unga pamoja nasi.

hii Kali. na mashoga nao wamwalike, wakwezi, aingie madarasani kusiko madex, afanye kazi za vibarua...nk. wanaita kuingia jikoni. Maji ya shingo
 
Lazima mkewe atakua anamnyanyasa sana huyu mzee. Nani anakumbuka story ya Twalipo yule alikua boss wa jeshi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…