PICHA:Machinga siyo watu wa mchezo mchezo

PICHA:Machinga siyo watu wa mchezo mchezo

jsenyinah

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
249
Reaction score
339
Wanabodi, kauli ya Mh Rais juu ya kuwapa machinga uhuru na taratibu mzuri wa kufanya biashara zao,sasa wamekuwa na amani kujinafasi maeneo tengefu,hasa nyakati za jioni.

Hapa ni karibu na sheli ya GAPCO jijini Dsm ambapo machinga wamepanga bidhaa zao na wanaendelea kupiga mzigo.
 
Attachments

  • IMG-20161220-WA0124.jpg
    IMG-20161220-WA0124.jpg
    73.4 KB · Views: 63
ubungo mataa na pale darajan, wameibana sehemu ya kupita watembea kwa miguu, wakat nafas ipo. changamoto kwel!
 
Wanabodi, kauli ya Mh Rais juu ya kuwapa machinga uhuru na taratibu mzuri wa kufanya biashara zao,sasa wamekuwa na amani kujinafasi maeneo tengefu,hasa nyakati za jioni.

Hapa ni karibu na sheli ya GAPCO jijini Dsm ambapo machinga wamepanga bidhaa zao na wanaendelea kupiga mzigo.

Gapco zipo nyingi jijini taja ni Gapco ya eneo gani ili tatizo lifanyiwe kazi
 
Tuliahidiwa taifa la viwanda........tunapata taifa la wachuuzi...
 
Simbachawene leo Kawaonya Ma RC na Wakurugenzi na Ma DC waliosusa na kuwaacha Wamachinga wakivuruga Mpangilio wa Miji!
 
Simbachawene leo Kawaonya Ma RC na Wakurugenzi na Ma DC waliosusa na kuwaacha Wamachinga wakivuruga Mpangilio wa Miji!
Simachawene naye mpumbavu, anashindwa kumwonya mkuu wake anaenda kuwaonya wanaopokea maagizo? Hebu aache usanii! Hapa Rais akubali kwamba alikurupuka, hayo ndo madhara yake ya agizo lake kutumika vibaya! Aje awaonye sasa machinga wake, maana akina Makonda wameufyata mikia chini ya miguu!!
 
Kwa hilo wakubali kuwa wamefeli nashindwa kuamin kama hawa jamaa ndo wapiga kura pekee maana imekuwa hatari ila ndo hivyo kwa hili tabaka la watawaliwa
 
Simachawene naye mpumbavu, anashindwa kumwonya mkuu wake anaenda kuwaonya wanaopokea maagizo? Hebu aache usanii! Hapa Rais akubali kwamba alikurupuka, hayo ndo madhara yake ya agizo lake kutumika vibaya! Aje awaonye sasa machinga wake, maana akina Makonda wameufyata mikia chini ya miguu!!
Anajua na anakumbuka kuwa Mafuru na Dr. Likwilile wanasubiri kupangiwa kazi nyingine kutokana na utendaji wao uliotukuka!
 
Hapa nafikiri ni magomeni usalama karibu na Travetine Hotel
Natamani Machinga wakapange bidhaa mpaka kwenye gate la Ikulu, tena wapange bidhaa moja moja kwa umbali wa nusu mita kutoka bidhaa moja hadi nyengine!!
 
Hii ni fursa hivi nikiagiza bidhaa kutoka China ama India kwa bei ya jumla si ninaweza kutafuta vijana wangu ninaowaamini na kuwakabidhi jukumu la kuuza hizo bidhaa kama machinga ? Tena sihitaji kilipia kodi ya pango la kufanyia biashara ama VAT.
Tutumie hii fursa kabla mambo hayajabadilika maana hawajapewa uhuru kutokana na sheria ama sera ya nchi bali ni kwa tamko la Mh. Rais, inamaana wakati wowote anaweza kubadili maamuzi na kuwaondoa.

When life gives you lemons make lemonade🙂
 
Back
Top Bottom