PICHA: KALENDA ya YANGA YAZINDULIWA

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
TUESDAY, DECEMBER 04, 2012
KALENDA YA YANGA YAZINDULIWA
KLABU ya Yanga imeingia mkataba na kampuni ya Pecha Media Health Promotion kwa ajili ya kutengeneza kalenda za klabu hiyo za mwaka ujao 2013 na inategemea kuvuna shilingi milioni 150,000,000 kupitia kalenda hizo.

Katibu mkuu wa Yanga Laurance Mwalusako alisema kuwa kampuni hiyo tayari imeshatengeneza kalenda 100,000 kwa kuanzia ambapo zitauzwa siku ya mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika kwenye ukumbi wa PTA uliopo Sabasaba jijini Dar es Salaam.

"Tuna bidhaa nyingi ambazo watu wanauza kiujanja ujanja bila ya kuingia mkataba na sisi sasa tumeamua rasmi kuwavalia njuga watu hao na yeyote atakayepatika anauza bidhaa zetu visivyo halali tufamfikisha kwenye jeshi la polisi.

Alisema kalenda hizo zitauzwa kwa shilingi 5,000 kila moja na hiyo itasaidia kuinua kiuchumi klabu hiyo ambayo alidai kuwa imedhamiria kufika mbali kimaendeleo.


Naye mkurugenzi wa Pecha Media Nassib Limira alisema wameamua kuingia mkataba na Yanga akiamini kuwa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo watawaunga mkono kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameisapoti klabu hiyo ambayo itanufaika na shilingi 1500 kwa kila kalenda na iwapo zitauzwa kalenda zote 100,000 basi Yanga itavuna shilingi milioni 150,000,000.


Alisema kampuni yake itavuna shilingi 400 kwa kila kalenda wakati wauzaji watapa shilingi 300 kwa kila kalenda na gharama nyingine zitabaki kuwa za uzalishaji.

TUESDAY, DECEMBER 04, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG

 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225

HONGERA YANGA... KILA KITU YANGA lazima kiwe na TRADE MARK kwahiyo kutakuwa hakuwa WEZI na WATU wa ku-COPY
 

MKALIKENYA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,196
1,170
YANGA! YANGA! YANGA! YANGA! naipenda Yanga nitanunua kalenda 2 moja ofisi nyingine nyumbani ooh nimesahau nitaongeza ya 3 nitaiweka chumbani kwa mwanangu COLLINS ha! ha! ha! dogo lazima awe YANGA.
 

Nyakipambo

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
435
0
Duh kweli wabongo kazi tunayo yaani kutengeneza kalenda nayo ni big newz kwa klabu yenye zaidi ya miaka 80!
 

Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
60,628
2,000
DSC_8633.JPG
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom