Picha inaeleza mengi sana hii

nditolo

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
3,802
Reaction score
4,459
Huyu dogo alikuwa analia siku mwili wa Magu unaagwa pale taifa. Nilifikiria mengi sana lakini kilichokuwa kinanishangaza ni nguvu kubwa iliyokuwa inatumika kuwaaminisha watu kuwa Magu anapendwa.

Nikaanza kufuatilia matukio yaliyokuwa yanafanyika huko wilaya ya Hai, matukio ya kuharibu mashamba, kuvamia hotel mbalimbali ikiwemo Ile Aishi Machame.

Huyu dogo alisimamia kudhoofisha upinzani kwa nguvu nyingi sana tofauti na nguvu aliyonayo DC kikatiba. Hata mkuu wa mkoa alikuwa hamuheshimu kabisa ( Anna Mgwira)

Akaenda kuharibu mashamba ya Mbowe, akawasingizia wafanyabiashara wa mabasi kung'oa mataaluma ya reli, ikatumika nguvu kubwa kuuaminisha umma kuwa kweli wafanyabiashara wa mabasi wamechukizwa na kufufuliwa kwa reli hivyo wakahujumu miundombinu.

Likaja suala la kumdhuru Mbowe yeye alikuwa wa kwanza kutangaza kuwa Mbowe kaumia sababu ya kulewa konyagi.

Kifupi alifanya fujo sana Kanda ya kaskazini. Watu walinyanyasika sana.

Sasa baada ya jiwe kufa akajua tayari muda wowote atashughulikiwa. Ndicho kilichokuwa kinamliza.

Pili huyo Denis Urio, mbali na ukilaza wake alikuwa na malengo mazuri tu ya kumtafutia Mbowe walinzi. Baada ya kupatikana walinzi ikawa tishio kwa Sabaya na vibaka wenzake.

Hapo niseme tu huyo mtuhumiwa Bwire alikuwa anawatisha sana maana ni mwamba kwenye mapigano. Watu wanafahamiana kutoka kweye mafunzo mpaka kazini.

Niliwahi kumsikia mkurya mmoja huko jeshini akisema "mwana umeliona li Bwire? " Akimaanisha kwamba sasa mtu akitaka kumdhuru Mbowe, Bwire atakuwa kikwazo.

Urio kapigwa sana na kateseka sana na kifupi tangu akamatwe miezi kumi na Tisa iliyopita mishahara imefungwa na familia yake ilikuwa haijui Yuko wapi.

Nimefurahishwa sana na kitendo Cha mawakili wa utetezi kutambua kuwa Urio Yuko mahabusu.

Yote tushukuru COVID-19, yule mwehu angetumaliza.

Mungu tubariki sisi watanzania wazalendo kama Mbowe na uwalaani watanzania waovu kama kingai.

Ahsante sana
 
Hatari sn
Na hao akina Kingai waliingizwa mkenge na huyo dogo. Wakajua watakapokomaa na Mbowe Kisha kumbambikia kesi hiyo ya ugaidi wangepanda cheo.

Kipindi hicho kulikuwa na watu wengi tu walijihusisha na kubambikia askari kesi za kujihusisha na siasa au kumtukana jiwe lengo ni kupata vyeo.

Huko majeshini walikuwepo akina Captain Linje, huyu alipakazia sana wanajeshi wenzake kesi hizo.

Tushukuru mungu
 
Wote hao MUNGU wetu atawatafuna
 
Urio kapigwa sana na kateseka sana na kifupi tangu akamatwe miezi kumi na Tisa iliyopita mishahara imefungwa na familia yake ilikuwa haijui Yuko wapi.

Nimefurahishwa sana na kitendo Cha mawakili wa utetezi kutambua kuwa Urio Yuko mahabusu.
Inamaana huyu jamaa amelazimishwa kutoa ushahidi
 
Unashukuru covid-19 iliyoondoka na ndugu yake Mbowe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…