PICHA - Hatari Tunayoichekelea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA - Hatari Tunayoichekelea

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, May 6, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Vijimambo vya fainali ya kiduku Thursday, May 06, 2010 3:02 AM
  Ile fainali ya mchezo wa kiduku ambao wanaume huvaa nguo za kike wakishindana kukatika mauno kama wanawake imefanyika na muaandaji wa mashindano hayo amepongezwa kwa kuwaletea wabongo ubunifu mpya ingawa baadhi ya wadau wanahofia mchezo huo utawaharibu vijana. Ilikuwa ni usiku ambao kusema kweli nilisikitika kumuona mwanaume akiwa amevaa sidiria na gagulo akikatika viuno kama mwanamke.

  Kijana mwingine naye bila haya aliyabenua makalio yake kumuelekezea mwenzake huku akikata mauno ambayo yalinifanya nijiulize wapi tunawapeleka vijana wa taifa la kesho.

  Hiyo ilikuwa ni sehemu ya vionjo vya fainali ya kiduku ambapo vijana wa kitanzania walishindana kukata mauno kuwania dola 250.

  Katika fainali hiyo kundi la Visqua toka kiwalani ndilo lililowashinda wenzao kwa mauno na kutunukiwa dola 250.

  Mamia ya watu walifurika kwenye ukumbi wa Travertine, Magomeni kushuhudia fainali hizo.

  Ingawa baadhi ya wadau wanauona mchezo wa kiduku kama vile unawahatarisha vijana kugeuka kuwa mashoga, muandaaji wa mashindano hayo Maimartha wa Jesse alipongezwa sana na kusifiwa kwa ubunifu wake wa kutuletea watanzania mchezo mpya aliouita kiduku.

  Wiki mbili zilizopita niliwaletea picha za hatua ya awali ya mashindano ya Kiduku na wadau wengi walikasirishwa na wanafunzi wakiwa katika unifomu za shule kushiriki kwenye mashindano hayo.

  Vijana wengine walionekana wakiwa wamevaa vipande viwili vya kanga hali iliyowafanya watu wengi waweke maswali ya kuuliza muandaaji wa kiduku ana malengo gani.

  Hata hivyo Mgeni rasmi wa fainali za kiduku zilizofanyika jumamosi alikuwa mbunge wa Kinondoni, Mh. Iddi Azzan wakati viongozi wa klabu ya Simba walikuwa wageni waalikwa na walikuja na kombe lao la ligi kuu ya bara walilolitwaa wiki chache zilizopita.

  Ukita kuangalia picha zaidi bonyeza hapa http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=793601
   
 2. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni kawaida yetu kutafuta mchawi baada ya kifo (au shuka asubuhi). Mungu atupishie mbali..
   
 3. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mzee mzima anaaibika bure mbele za watu.
   
 4. L

  Likwelile New Member

  #4
  May 8, 2010
  Joined: May 8, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu si ubunifu, ni maangamizi kwa taifa.
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Huu ni mchakato maalum wa kuuingiza ushoga kwa nguvu na kwa spidi katika jamii ya kitz.
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ngoja ninyamaze, naweza kutusi watu hapa ikawa tabu
   
 7. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  So Disgusting..........aaargh
   
Loading...