Photos:yanga ya manji bungeni jana

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Waziri Mkuu, Mh Pinda kushoto, akiwa na Mama Fatuma Karume kulia. Katikati ni Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' nje ya ukumbi wa Bunge, Dodoma leo.

Na Mahmoud Zubeiry, Dodoma
MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC ya Dar es Salaam asubuhi ya leo wameonyesha Kombe lao ubingwa wa michuano hiyo, maarufu kama Kombe la Kagame katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodoma.
Mheshimiwa Spika, Mama Anna Makinda baada ya kumaliza kikao cha asubuhi alianza kutambulisha wageni mbalimbali waliotembelea Bungeni leo na ukumbi wa Bunge uliripuka kwa shangwe nzito, alipofikia kuwatambulisha mabingwa hao wa Kagame.
Mama Anna Makinda, alianza kwa kuwatambulisha viongozi wa Yanga, Wajumbe wa Baraza la Wadhamini, Mama Fatuma Karume, Francis Kifukwe na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji, Makamu wake, Clement Sanga na Wajumbe wengine kabla ya kukiinua kikosi kizima wafalme wa soka kwa nchi 12 barani Afrika.
Wakati wa zoezi hilo, Wabunge ambao ni wapenzi wa Simba, mahasimu wa jadi, wa Yanga, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wekundu hao wa Msimbazi, Alhaj Ismail Aden Rage, walianza kuwabeza wapinzani wao hao, kwa kuwakumbushia kipigo cha mabao 5-0 walichowapa katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu.
Lakini hiyo haikuzuia sherehe za Yanga kuendelea hadi nje ya ukumbi wa Bunge, ambako Wabunge na Mawaziri wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda walipiga picha na wachezaji, viongozi na Kombe lao hilo.
Wabunge wengine na Mawaziri, ambao ni wapenzi wa Simba wakiwemo Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Mh. Amos Makala, Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azam na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia nao pia walijumuika kupiga picha na Yanga.
Baada ya hapo, wachezaji wa Yanga na viongozi walikwenda kwenye ukumbi mdogo wa Bunge kukutana na Uongozi wa Tawi la klabu hiyo, Bungeni chini ya Mwenyekiti wake, Mohamed Hamisi Misanga uliochaguliwa Julai 31, mwaka huu ambako huko Mama Karume alizindua rasmi tawi hilo.
Yanga, waliotwaa Kombe hilo mara mbili mfululizo sasa, wachezaji wake waliwasili usiku wa jana na baadhi ya viongozi, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Titus Osoro, Mohamed Bhinda na George Manyama pamoja na Katibu Mkuu, Celestine Mwesigwa na Meneja, Hafidh Suleiman, wakati Mwenyekiti, Yussuf Manji na Makamu wake, Clement Sanga na Wajumbe wengine waliwasili mapema leo.
Kwa upande wa timu, wachezaji walifika pia jana na makocha wasaidizi, Freddy Felix Minziro na Mfaume Athumani Samatta, wakati kocha Mkuu, Mbelgiji Tom Saintfiet alikuja leo pamoja na viongozi hao wakuu na Wajumbe wa Baraza la Wadhamini, Francis Mponjoli Kifukwe na Mama Fatuma Karume.
Yanga ilitwaa Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo wiki iliyopita, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kuifunga Azam FC mabao 2-0, ambayo yalitiwa kimiani na Hamisi Kiiza ‘Diego Milito’ na Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Hiyo kwa ujumla ilikuwa mara ya tano mfululizo, Yanga inatwaa Kombe hilo, baada ya awali kuchukua mwaka jana, wakiifunga Simba katika fainali bao 1-0, Uwanja wa Taifa mfungaji Kenneth Asamoah ambaye ametemwa, ingawa siku hiyo Kiiza pia alifunga bao safi, ambalo refa alilikataa.
Yanga ilichukua kwa mara ya kwanza Kombe hilo, mwaka 1975 ikiifunga tena Simba katika fainali, mabao 2-0 wafungaji Sunday Manara ‘Computer’ na Gibson Sembuli (sasa marehemu) Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Ikachukua tena mwaka 1993, Uwanja wa Nakivubo, Kampala, Uganda kwa kuifunga SC Villa mabao 2-1, yaliyotiwa kimiani na Said Nassor Mwamba ‘Kizota’ (sasa marehemu) na Edibily Jonas Lunyamila.
Ilichukua tena mwaka 1999, ikiifunga tena SC Villa, Uwanja wa Nakivubo, kwa penalti 5-3, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, Yanga ikisawazisha bao kupitia kwa Lunyamila, baada ya Hassan Mubiru kutangulia kuifungia Villa, siku hiyo Manyika Peter akicheza penalti mbili za Waganda.

Mh Pinda akiwa kikosi cha Yanga na kocha Mbelgiji, Tom Saintfiet


Wachezaji mjengoni







Cannavaro akionyesha Kombe kwa wabunge


Mh Nkamia akiwa na Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa


Mh Azzan akiinua Kombe, kulia kwake ni Mh Pinda na Martha Mlala




Mh Makalla kulia akisalimiana na Manji. Katikati ni Mh Mtemvu


Mh Makalla akiwa ameshika kwa pamoja Kombe na Manji. Katikati ni Cannavaro


Mh Makalla akisalimiana na Kocha Tom


Mh Pinda na wadau mbalimbali wa Yanga, wakiwemo Wabunge na Mawaziri


Mh Makalla wa pili kutoka kulia akiwa na Mhariri wa Habari Leo, Eric Anthony. Kulia kwake Makalla ni Kevin Yonda na kushoto kwa Eric ni Athumani Iddi 'Chuji' na Mwigulu Lameck Mchemba, Mbunge wa Iramba Magharini


Mh Pinda na wadau wa Yanga


Manji akiteta na William Ngeleja




Wachezaji mjengoni


Kocha Tom, Mohamed Bhinda na Mwenyekiti wa Vijana wa Yanga, Bakili Makele

Mh Mkuchika na Manji

Martha akihesabu michango ya Wabunge wenzake

Mh Zambi kulia akifungua kikao

MAKOCHA; Kutoka kulia ni Tom, Minziro na Samatta

Waheshimiwa Yanga damu

Tegete na Chuji

WALIOTOKEA SIMBA KIVYAO; Kutoka kulia Gumbo, Barthez na Yondan

Mh Mtemvu, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe katika utambulisho wa Tawi la Yanga Bungeni

Meza kuu

Manji na Misanga

 
Siku timu yetu yoyote ikichukua kombe la klabu bingwa Africa nadhan kutakuw na mapumziko mwezi mzima, Tz hatujielewi kabisa.
 
Mbona sijaona sehemu yeyote Mheshimiwa Rage amepiga picha na Kombe,vipi yeye hatamani kupata ukumbusho wa picha na Kombe kubwa kabisa kwa ngazi ya Club katika ukanda huu wa Africa Mashariki na Kati kabla hajang'atuka,au ndo nafsi ilitaka lkn macho ya watu yakamzuia?
 
Nafikiri umefika wakati sasa Mheshimiwa Rage na jopo lake na usajili mzuri huu wa mwaka huu wakahakikisha Simba nayo inafanya vema katika michuano ya kimataifa angalau wakate kiu ya Waheshimiwa wadau wa team yao,nawaona Wakereketwa na Wanachama wa Simba Mheshimiwa Makalla na Mkamia wameona wasimalize vipindi vyao vya ubunge (ukichukulia Chadema wanatishia amani ya 2015) bila angalau kupata kumbukumbu ya kulishika kombe la Kagame.
Very nice Waheshimiwa,bora mmeamua kupata kumbukumbu kabisa ksbb hiyo team yenu haina mdhamana,msingepiga picha hapo mngeweza kutopata kumbukumbu hiyo kabisa.
 
Mbona sijaona sehemu yeyote Mheshimiwa Rage amepiga picha na Kombe,vipi yeye hatamani kupata ukumbusho wa picha na Kombe kubwa kabisa kwa ngazi ya Club katika ukanda huu wa Africa Mashariki na Kati kabla hajang'atuka,au ndo nafsi ilitaka lkn macho ya watu yakamzuia?

mkuu asingeweza,mashabiki wa simba wangemfanya kama ngasa alivyofanywa na azam.!
 
Nasisi tutakuja na kombe letu la urafiki, hilo la kagame hatuna uwezo nalo marefa wa kagame nouma,. hawaelewi somo letu lile la ujanjaujanja
 
Kitendo cha kupiga picha na huyo bwana mwenye mabendera shingoni kimeharibu kabisa ladha ya Ubingwa wa chama langu!
 
SIMBA WALIPOPELEKA NGAO(SIO KOMBE)BUNGENI


s7.jpg

Nahodha Juma Kaseja akiwa kashikilia Kwa majonzi Ngao yao ya Jamii mjengoni








 
SIMBA WALIPOPELEKA NGAO(SIO KOMBE)BUNGENI


s7.jpg

Nahodha Juma Kaseja akiwa kashikilia Kwa majonzi Ngao yao ya Jamii mjengoni



Wa kwanza kushoto: "hiv jamani inaleta sense kweli kuleta hiki kibao Mjengoni,wenzetu walileta kombe la kimataifa sisi tumeleta hiki kibao kilichotengenezwa na Fundi Seremala wa pale Gerezani,nafikiri Mwenyekiti wetu naye sometimes huwa hazi'charge"
Kamwaga: " Aibu, naona hata wale waheshimiwa wapenzi wa team yetu moyoni wanatushangaa,anyway kuja kuosha macho humu ndani ya mjengo mara 1,1 siyo mbaya"
Kaseja: Natamani ningempachika Kamwaga akakibeba hiki kibao,ksbb hii siyi issue wala nini ni ubwege,waheshimiwa hawajahamasika kabisa kama tulivyoona walivyohamasika wakati Yanga walivyoleta kombe la Africa Mashariki na Kati huku,anyway haya yote kayataka Rage,ona sasa tunavyoaibika"
 
Kumbe yanga wana jeshi njano na nyeusi kama PAN African au Toto?nilidhani Njano na Kijana!!
 
wazee wa tano bila wakiwa bungeni..subirini huku ngasa,okwi,kazimoto,chombo,kanu,kaseja,mbuyu,sunzu,boban mtatukoma..
 
wazee wa tano bila wakiwa bungeni..subirini huku ngasa,okwi,kazimoto,chombo,kanu,kaseja,mbuyu,sunzu,boban mtatukoma..

hatari dida, osca,luhende,canavaro,yondani,damayo,niyonzima,chuji,kavumbavu,kiza,bahamagori,. Apo lazma mkate rufaa na hivi mwaka huu mmeishiwa hata hela ya kununa penart mtakoma
 
iko poa sana

Kwa ujinga wenu na kwa kupitia mpira, Manji amewafanya wajinga mpaka mmesahau[ nyie na wabunge wenu] kuwa huyu huyu ndie alituibia fedha zetu benki kuu [ EPA] kwa kupitia kampuni ya KAGODA!! Miafrika ndio mlivyo!!
 
Back
Top Bottom