Mkuu,
Nakushauri ununue photocopy aina ya CANON image runner 2420. Ki ukweli ni photocopy ya kisasa halafu haili umeme, umeme unaotumia ni kama wa printer.
Ukija kwenye maintanance yake ni very minimum na output ya photocopy ni karatasi 9,000 - 11,000. Kingine ni kuwa unaweza ukaiunganisha na computer ikawa hiyohiyo ni printer and at the same time ni photocopy.
Toner yake inacost 80,000 ila zipo nyingine nimeziona dar wanauza kwa 40,000 nimeshanunua ila sijazijaribu.
Mashine kwa kuwa mimi niko Tanga nilinunua mpya kabisa kwa 1,900,000 lakini kwa Dar nilijaribu kuuliza Jamhuri Stationers mtaa wa jamhuri opposite na NBC kichwele branch wanauza 1,800,000.
Ni hayo mkuu...............