Photo of the Day - Dar es Salaam 1985

UDA dogo,not sure
3079232848_a46d62066c_b.jpg
Hiyo uda dogo ndiyo lilikuwa linaitwa nusu mkate zilikuwa ISUZU, nakumbuka wakati huo nilikuwa shule ya msingi darasa la nne. Watu wanakumbuka SIMBA LUWALA madaladala ya mwanzo pamoja na vile arusha wanaviita vifodi vilikuwa isuzu muundo wa Toyota Hiace siku hizi?
 
Ukienda mjini jumapili kila mtu wa tatu unayemuona unamjua, mnasoma wote, mmecheza mpira, mmeenda kusali pamoja etc.

Enzi hiyo kabla machinga hajaingia mjini, ukikutwa unazubaa zubaa mjini unapigwa "uzururaji" watu wanakutia kwenye lori wanakupeleka Gezaulole au Kibugumo.

Penye red hapo ni kweli kabisa ndugu yangu. Unanikumbusha mbali we acha tu.
 
@masopakyindi. Nakurudisha tena enzi zetu za ujanani. Hapo IPS chini na lile duka la Tanzania Elimu Supplies. Siku zile kweli Dar kulikuwa na watu wachache!

ips-dar.jpg
 
Kumbe JF wazee mko wengi!
Ha ha ha ha! Nyie vijana akina muwaha msijifikirie ni nyie tu mnaojua maswala ya utandawazi. Tumo humu humu na tunakula na nyie sahani moja mpaka kieweleke:=))
 
Hii imepigwa mwaka 1975!

5847896120_eacdf5130b_b.jpg

Ilo jengo la vigae hapo mbeleni ilikuwa chuo cha utalii (karibu na Kilimanjaro Hotel). Kabla ya vita dhidi ya Iddi Amin Dar ilikuwa tambarare, yaani basi tu! Nakumbuka ofisini kwetu huo mwaka 1975 (Insurance, Motor Underwriting Dept, chini ya bosi Mwabulambo) tulikuwa tunapata chai ya bure kila saa nne na saa nane. Vijana wazawa mpo hapo?
 
Heshima yako mkuu, hiii siyo Dar tuliyokulia sisi wengine ya miaka ya 80s halafu utakuta hapa ilikuwa ni siku ya kazi
 
Hivi Ndinda kuna ka compyuta script uliwahi kukatengeneza ili kuibua picha manaake huwa unaibua vitu visivyoonekana ati
 
Back
Top Bottom