Should long-term partners know each others' phone passwords?
(Je, wapenzi wa muda mrefu wanafaa kujua nywila za simu za kila mmoja?)
---
Chaguo lako ni lipi.
Ni muhimu kushare inaongeza uaminifu.
Wangu anapenda kuficha utakuta tu kabadili pattern na hakwambii huwa naigundua pattern yake kwa njia rahiiiiisi kama maombi ya mwamposa
Kwa mtu uliyezaa naye na mnaishi kwenye ndoa kama mke/mme, ni muhimu kushirikishana nywila, kwa kuwa ni mwili mmoja kutokana na mafunzo ya ndoa, ili chochote kitakachotokea iwe ni umauti au janga lolote aweze kushika hatamu
Hapana kabisa.
Sioni haja ya ku-share password.
Kila mtu abaki na nywila yake, isipokuwa tu kwa sababu maalum.
Mfano: mke/mume/mpenzi yuko katika matibabu au chini ya uangalizi hapo password lazima, ila matibabu yakishaisha basi haina haja