Phobia? Selfishness, au Nini?


au wana mengineyo yamejificha nyuma ya pazia? mana kwangu huyo sio mwenza bali adui yangu!
 
Reactions: Mbu
Interestingly,

....majibu mengi yanafanana wajameni, mmejigundua?
Wengi wenu mna fikra kwamba mafanikio huenda yakambadilisha mtu.

Hii ni dhana!
Nini madhara ya dhana 'mbaya' katika mahusiano?

..... Spouses inabidi kujifunza kufurahia furaha ya wakati uliopo badala ya kujipa wahka na dhana mbaya ya kesho itakuwaje!
 
hapa umenena kiutu uzima kabisa
 

Mbu hiyo 'dhana' watu wameeiishi na bado wanaendelea kuiishi kupitia ndugu, jamaa na marafiki zao kwahiyo lazima wawepo wanaitegemea kutokea hata kwa wenza wao.

Wale wanaoishi kwa kuangalia uchanya wa kila jambo ndio pekee wanaoweza kufurahia kwanza na kuhuzunika baadae ikiwa mambo yataenda vibaya.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Mbu

......-positive mental- attitude!
Yeah Lizzy upo kwa mstari kabisa,
Ila,.....

Umemallizia "...kuja kujuta baadae ikiwa mambo yataenda vibaya" hilo ni somo jingine jipya.

Akili hizi nazo zinahitaji 'gym' ya mara kwa mara kuweza beba matukio yasotarajiwa kuliko kila wakati kuivisha 'protective armour'...as if kila breaking news ni "hatari!"
 
Last edited by a moderator:
Wengi ni tabia za kuzaliwa, hata jamaa kumsifia jamaa mwenzake
 
Reactions: Mbu
Tatizo ni kutokujiamini. Mara nyingi wanaume ndio wanakuwa na fikra hafifu za aina hiyo. Ikitokea girl/mke wake akiwa amemzidi either elimu + kipato huwa anaona atadharaulika. Ili aendelee kuabudiwa kama mungu wa familia basi ataakikisha kila opportunity ya girl/mke wake anaiziba.
 
Reactions: Mbu
Jealous is a disease!!! Get well soon people!!
 
Reactions: Mbu
inapofikia hali hiyo inakuwa sio wenza tena upendo dhahiri unapungua unapopanda cheo au mafanikio na kubadili tabia uliyokuwa nayo mwanzo inaleta woga kwa mmoja wapo na kutokushangilia mafanikio yenu na inapotokea akashangilia baada ya muda ni kwamba hakuona vile alivyotarajia yaani mabadiliko asiyoyapenda....hii ipo kwa wote me au ke
 
Reactions: Mbu
Mbu kakangu... Nimekusoma. Na nimeona sana tu hiyo... Na ipo zaidi kwa wanaume kuliko kwa wanawake. Mwanamke mumewe anapozidi kupanuka na kukua ki maendelea huwa happy na supportive sana tofauti na kwa wenzetu.

Mie nadhani inaweza kuwa kwa sababu hizi:-

1. Insecurity

Uwoga wa kujiona si lolote kwa mkewe kisa kamzidi. Tunajua kuwa kichwa cha familia tumechukulia kuwa ni mume tukiacha pembeni dhana ya kusema ni partnership ambayo kimsingi yapaswa kusaidiana. Mwisho wa siku mwanaume ndiye anakuwa mtatuzi mkubwa wa masuala ambayo ni msingi... Na bahati mbaya ama nzuri kile ambacho kifanya kimpe heshima mwanamume kama baba/mme ni kwa kiasi ambacho anaweza idhibiti na kuisimamia familia yake hasa katika basic needs. Na basic needs daima huwa solved tokana na pesa ambayo tegemezi ni kipato. So inapotokea kuwa mke awe na pesa zaidi ya mume kuna majukumu ambayo by default yanaporwa na kumfanya yale ambayo yana define nani kichwa cha familia kuhama toka kwa mume kwenda kwa mama.

2. Fikra Pana

Uelewa tu ule wa kutambua kuwa mke atakapozidi kipato cha mume bahati mbaya ama nzuri wengi hubadilika tabia na kujenga dharau. Hivyo kutikisa msingi mzima wa mahusiano. So anaona ni kheri siku zote bora aendelee kuwa pale pale... Na hata kama atakuwa si to the extent ambayo yeye mume yupo.

Sijasoma michango mingine bado. I do look forward to doing that. Asante kwa kunishtua.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Mbu
Soulmate.......samahani kwa kuchelewa but sidhani kama nimechelewa sana........... Hahahah nianze kwa kucheka kwanza maana umenikumbusha Enzi za Kulivua penzi........ mie nlikuwa naambiwa live kuwa hizo degree zako ni makaratasi tu any Dick and Tom can have them........ yaani hapo mwenyewe nimekuja na smile kubwa meno yote nje kwa furaha, tena hapo nimejizuia nisifurahie barabarani ili nije nifurahie na mwenzi wangu lol.....................But I believe most of the time huwa ni inferiority complex tu.......... Mwingine anajua kaisa kuwa hata kama mwenzi wake awe successful kiasi gani hawi threat kwake but huwaza sana jamii inayomzunguka, marafiki zake watamchekaje au kumwonaje.
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…