Phobia? Selfishness, au Nini?

Hii mpya kwangu.
Ila kama ipo,basi hao wanao fanya hivo nahisi ndo
wale utaskia kamuua mwenzi wake,.....ili arithi mali.

Ingawa sitaki kuamini kama kuna kitu kama hicho.
 
.....hebu vuta taswira mke anakuwa Ambassador, au waziri....au mkurugenzi mkuu kwenye shirika lenu...

Ni sifa kwako mume au ni majanga? mwekundu tafadhali bana, heheh
kama mnapendana(mnaaminiana) hamna tatizo lakini kama mnaishi kwa mtego ni sababu ya janga hiyo
 
Reactions: Mbu
Low self esteem inajitokeza kwa mifumo tofauti tofauti. Ukiwa na mwenza wa aina hiyo, ni kumsaidia kujitambua thamani yake binafsi (bila mali, uzuri, wala sifa yeyote). Akishajua ana thamani basi hawezi ona shida mwenza ukimzidi kitu chochote.
 
Roho hii ni mbaya mkuu kama ya kichawi tu...nipo mkuu Kivumah...habari ya siku


A REAL RELATIONSHIP: has fights, trust, faith, tears, pain, argument, patience, secrets, jealousy & LOVE.
Nakuelewa Vin Diesel, Nipo mkuu hauchi hauchi kunakucha, Al Shabaab nao wanatuwinda
 
Last edited by a moderator:
Mbu bana. . . kwani hujui ule msemo usemao 'maskini akipata ndio utajua tabia zake halisi' ?!Kuna watu makucha yao hung'arishwa kwa mafanikio.

Hali kama hiyo inapotokea kwa wanandoa (sio ndugu/rafiki) kunaweza kusababishwa na WIVU ila nadhani WOGA/WASIWASI na KUTOKUJIAMINI au hata kutokumwamini mwenzi ndio zaidi.

Kuna watu ambao wanaishi maisha waishiyo kwasababu tu mifuko haijatuna, kuna watu wametulia kwenye ndoa zao na pia watu wengine ni(au tuseme wana-act) humble kwasababu hiyo hiyo.
Kwahiyo inapotokea hali kama hiyo uwezekano ni kwamba mume/mke anaweza akawa anafurahia kabisa tena sana tu mafanikio ya mume/mke wake lakini mafikio hayo hayo yanamletea WOGA, WASIWASI na KUTOKUJIAMINI ndani ya ndoa yake.

Woga wa kunyanyapaliwa, woga wa kuanza kudharauliwa na kuonekana hufai tena (mwenzio amepanda daraja), woga wa yeye kuanza kufanya mambo ambayo hakuwa anaweza kuyafanya kutokana na kipato chake mf. kulewa, woga wa kutafutiwa 'replacement' inayoendana na mafanikio ya mwenzi n.k

Muhimu ni kumwaminisha mtu wa aina hiyo kwamba hutobadilishwa na mafanikio hayo bali maisha yenu pamoja ndio yatakayobadilika for the better. Mtoe woga na wasiwasi ajue kwamba yeye ndie wako wa moyoni no matter how succesful you get. Asipoonyesha kuchangamka na kufurahia pamoja na wewe baada ya hapo basi huyo hana jema. Chuki, wivu na gubu ndio zake.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Mbu
Low self esteem inajitokeza kwa mifumo tofauti tofauti. Ukiwa na mwenza wa aina hiyo, ni kumsaidia kujitambua thamani yake binafsi (bila mali, uzuri, wala sifa yeyote). Akishajua ana thamani basi hawezi ona shida mwenza ukimzidi kitu chochote.

- kimsaidia kujitambua-

Ohh yeah, so la mwanzo ni kujikubalisha mwenzio 'hajitambui' la pili kumkubalisha 'ajitambue' kwamba ana mapungufu....

A good starting point Kongosho
 
Last edited by a moderator:
kama mnapendana(mnaaminiana) hamna tatizo lakini kama mnaishi kwa mtego ni sababu ya janga hiyo

- kuishi kwa mtego!-

Hehehe, kumbe kuna wengine wanaviziana kwenye ndoa ee?!
 
Hii mpya kwangu.
Ila kama ipo,basi hao wanao fanya hivo nahisi ndo
wale utaskia kamuua mwenzi wake,.....ili arithi mali.

Ingawa sitaki kuamini kama kuna kitu kama hicho.

....utaamini vipi kama huja experience hiyo kitu banaa....hahaha... Speaker, duniani kuna mambo!
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
A REAL RELATIONSHIP: has fights, trust, faith, tears, pain, argument, patience, secrets, jealousy & LOVE.

......hahaha, truth hurts!
Enhee, ulitaka kusema nini vile
Maana "secrets" imo katikati ya mstari!
 
Hivi unadhani ni ubaya shosti? Ukimuuliza mtu anayefanya hayo hajui hata kama ni tabia mbaya, anajua anajilinda yeye na maslah yake(ndoa included)

Lakini chanzo nachoona ni low self esteem, hili gonjwa ni baya mno. Na mbaya zaidi lina mifumo karibu elfu kidogo ya kujitokeza. Sijui kama uliwahi kupanga afu ukawa na usafiri? Unakuta mtu kamwagia gari yako maganya ya nyanya na vitunguu. Ukichunguza sababu "unaringa na gari lako'. unadhani hii ni roho mbaya? Kwa mtu anayejiamini au mwenye esteem ya kumtosha haiwezekani kufanya jambo la aina hii, it's crazy!

Acha mtu na mwena unaweza hisi anaogopa kulipishiwa, inakuwaje mtu anamfanyia hila mwanane afukuzwe kazi? AU unaona siblings wanachongeana kupoteza kazi ama kitu chochote?

Nimeishi na watu wenye low self esteem, ni kama 'mental case', vitu anavyofanya mtu hazina hata maelezo.

Niliwahi mtuma mtu akapokee mgeni wangu mie niko bize na maandalizi, tena kituo cha treni. Miaka hiyo hakuna simu ila kanitumia barua atapita hiyo sehemu tarehe fulani na mida. Tumejiandaa wee, tukatuma mtu wa kumpokea. Akaondoka kwenda kumpokea, kumbe wala hakwenda akarudia njiani akaja na stori za ameshindwa kuja yuko na watu na blah blah blah blah. Anyway, siku zikapita, nikamwandikia barua kwa nini hakutimiza ahadi ya kuja home na sie tulijiandaa. Akanijibu kuwa hakuna anajua ninapoishi, na sikutuma hata mtu wa kumpokea. Nilibaki what:yuck:?

Niliyemtuma alimwambia cousin mmoja kuwa, kwani mgeni wangu kapewa mapokezi yale na familia? Hadi kesho sijawahi kuelewa, but alikuwa na tatizo la esteem sana.

 

-woga!-

Weye Lizzy weye.....
Sasa kama jamii yenyewe ishajikubalisha "mswahilu mpe cheo, au kipato!" Uyaone makucha yake...
Huoni kuna ugumu wa kumshawishi huyo spouse?
 
Last edited by a moderator:
Hakuna tunu kubwa mtu unapewa duniani kama kujitambua na kujikubali kuwa una thamani wewe binafasi bila kitu chochote. Yaani vile ulivyozaliwa, hiyo tu inakupa thamani na huhitaji kitu kingine ili uonekane wa maana.

Hivi vitu vingine tunavyotafuta be it pesa, cheo, status ni tools za kutusaidia sie kuishi kwa rahisi zaidi. Na kama mwenza akiwa na tools nyingi, kwa namna moja zinawasaidia wote.

Mtu akishatambua hili sioni kama ataona hatari kuzidiwa chochote na yeyote.


Na ili umsaidie kwa urahisi zaidi, ni vizuri kujua historia ya alikotokea, labda alinyanyaswa sana na pesa, cheo kwa ujumla 'mali' ikamfanya subconsiously kuabudu 'mali' na kuipa uthamani wa ubinadamu.

- kimsaidia kujitambua-

Ohh yeah, so la mwanzo ni kujikubalisha mwenzio 'hajitambui' la pili kumkubalisha 'ajitambue' kwamba ana mapungufu....

A good starting point Kongosho
 
Reactions: Mbu
......hahaha, truth hurts!
Enhee, ulitaka kusema nini vile
Maana "secrets" imo katikati ya mstari!
Unachoulizia wewe Mbu kwa mtizamo wangu jibu lake Ni Jealousy, ambayo ni the most dangerously feeling, Jealousy creates insecurity. Insecurity creates hatred, and hatred kills softly.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Mbu
kuna wapenzi ambao wakipata mafanikio ndio jeuri dharau na kiburi kinazidi.... kama mwanaume unakuta harudi hata nyumbani.. amani inatoweka na hakuna upendo. unategemea mafanikio yake mwenza wake atayafurahia? nani atafurahi kuona mpenzi wake ana kazi nzuri analipwa vizuri lakini haioni hata sh kumi yake!!! sio tu roho mbaya... unaambiwa ukitaka kujua tabia ya mtu subiri apate pesa au cheo. lol
 
Reactions: Mbu
Mbu ni kweli, kwa mfano, kuna wanaume ambao hawataki kabisa mwanamke wake atongezwe na wanaume wengine.

Lakini ni kawaida kwa mwanamke kutongozwa awe ana mwanaume or not. In fact, ina-boost confidence ya mwanamke.

Baadhi ya wanaume are not used to this, wengine wana insecurity, wengine are just too possessive, wapo ambao wana psychological problems, being obsessive au ujinga tuu.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Mbu

-insecurities.-

Hahahaha, kuna wengine wanafikia hata kuwauliza wake zao kama wamewahi kutongozwa, wakijibiwa "HAPANA!" Pia wana mind!

What's wrong with these insecurities?
 
Last edited by a moderator:

......mnh, Husninyo wewe pia ni mmoja katika waoga?
Umeandika kwa uchungu sana mydear
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…