Phiri na Uchawi wa Wenger | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Phiri na Uchawi wa Wenger

Discussion in 'Sports' started by njiwa, Sep 22, 2010.

 1. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,075
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  kuna habari zipo katika mtandao flani wa jamii kwamba Kocha wa Simba Patrick Phiri ameanzisha uchezaji mpya ndani ya timu hiyo itakayoifanya icheze soka la hali ya juu na la kuvutia zaidi.

  Ukiangalia mazoezi ya Simba, Phiri ameanza mbinu za Arsene Wenger wa Arsenal licha ya yeye mwenyewe kuwa mshabiki wa Man United.

  Phiri ambaye timu yake inaendelea na mazoezi makali kwenye uwanja wa Tanganyika Peackers kawe jijini Dar kila asubuhi amewaambia wachezaji wake anahitaji kuona mpira wa kasi na wa kuvutia zaidi.

  Kocha huyo amekua akisisitiza jambo hilo kwa ukali katika mazoezi ya wiki hii ambayo alitumia muda mwingi kuwafundisha kulenga shabaa langoni na kukiri kuwa ilikuwa ngumu ila akaridhika na ufanisi wa vijana wake.

  Nataka kuona mabadiliko makubwa kiuchezaji kwa vile nina kikosi imara chenye wachezaji wakila aina na wenye uwezo nataka timu icheze soka kwa nguvu na liwe la kuvutia alisema Mzambia huyo aliyezaliwa mwaka 1956.

  Nimewafanyisha mazoezi ya kisasa na kuwapa mbinu mbalimbali takribani wiki mbili sasa wameonyesha uelewa mkubwa na nadhani muda mfupi ujao.

  Simba itacheza mpira tofauti na wa kuvutia sana na wenye matokeo mazuri tunatakiwa kufanya hivyo kwa vile ligi ni ngumu na kila timu imejiandaa vizuri.

  Nawatakia wana MSIMBAZI safari njema!
   
Loading...