PhD ya Open University inathaminika?

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,536
32,144
Wakuu nataka kusoma PhD Chuo Kikuu huria, je hii Shahada toka chuo pendwa inathaminika huko kitaa? Nisije kupoteza muda na pesa. Asanteni
 
Wakuu nataka kusoma PhD Chuo Kikuu huria, je hii Shahada toka chuo pendwa inathaminika huko kitaa? Nisije kupoteza muda na pesa. Asanteni
We kajipatie gamba lako maisha yasonge. Hata mwendazake alijipatia PhD yake hapo Mlimani kilaini tu.

Mtaalam mbobezi wa kupima viuno vya mikorosho...
 
Ulishawahi kwenda hata kwenye ofisi zao kupata abc hasa pale kinondoni

OUT ni chuo cha serikali kimeanzishwa kwa sheria ya bunge

Kina madocta na maprofesa na kinatumia misingi ile inayopotiwa na vyuo vingine katika utoaji wa shahada zao .

Watembelee waulize wao wahusika ukiona panakufaa go ahead ukiona hapakufai piga chini

Tabia za kitanzania za kupambanisha vyuo ni za kipumbavu wakati vyuo vyote vya serikali viko kisheria

Mara chuo cha kata

Wengine wako jalalani

Ujinga na upumbavu ni ule ule
 
Unasoma LLB open, ukutane kisutu na aliyetokea UDSM? Jiandae kwa PO
 
Soma mkuu PhD ya hapo ni sawa tu na vyuo vingine vyovyote, ni Kama useme shule ya kata na shule ya wilaya kwamba ukisoma ya kata na ukafaulu bas kile Cheri hakitambuliki. Tena nikupe Siri elimu ya hapo ni ngumu kinoma ujiandae kisaikolojia la sivyo PhD ya miaka 3 utaimaliza kwa miaka 6 had 7, mi niliipita hapo ngaz ya masters macho yakanitoka almanusra niahirishe masomo ila mwisho nikamaliza. Kama unataka usome kwa kurelax nenda vyuo vya private Kama tumaini na vinginevyo
 
PhD yake ipo hivi 👇 , ila kama unataka uitwe Dr wala haina shida wewe nenda tu 😁

phd.jpg
 
Sidhani Kama Elimu yako imekusaidia lolote hadi sasa vinginevyo usingeuliza swali la kiboya namna hii, Ubora wa Elimu utatokana na juhudi zako na kujituma kwako, na Kama hadi Leo unangoja PhD ndo ikutoe kimaisha basi hesabu umefeli Maisha, hata hiyo Master Degree uliyonayo achana nayo itoe kichwani mwako na kabatini mwako.
 
Umeuliza swali, tunapaswa kukujibu, ingawa, kwa level yako hupaswi kuuliza swali la namna hii! bado unamidhania ya ulinganishi wa maneno ya mtaani ambao unafanywa na watoto wadogo hasa degree ya kwanza.

OUT inawanafunzi wengi sana wa PhD, na kimsingi unapaswa kujiandaa haswa kisaikolojia! wanahitaji mtu usome na uelewe! Elimu unayoihitaji pale sio lelemama! ni kuandika na ku present ulicho find.

Level ya PhD ni kubwa sana, ndio mana huwezi kita watu wenye level hiyo wanajadili eti chuo kipi ni zaidi.

nakushauri soma pale unapoona panafaa, wote mtaitwa Dr, na ufanisi wa u Dr wako utategemea na uzamivu wa eneo ulilofanyia research
 
Nenda ukasome mkuu.

Msingi mkuu wa PhD ni utafiti na juhudi zako za kuandika tasnifu iliyosimama.

Utakua na supervisors watatu na utaona faida yake.

Go for it kaka hutojuta
 
Mkuu Open achana nacho kabisa kipo juu sana kitaaluma kupitia tafiti na machapisho. Kuna vyuo kama vinne na Open kipo hapa nchini the best kuhusiana na machapisho
 
Back
Top Bottom