Petrol stations Morogoro Road ni kero sana

Petrol stations Morogoro Road ni kero sana

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,702
Sisi tunaotoka Kiluvya kuja mjini hakuna vituo vya mafuta njiani, wajenzi wa barabara wameziba njia zote za kuingilia vituoni.

Mfano kituo cha Henry Filling Station kilichopo Chuo cha St. Joseph kuingia hadi upite Luguruni utembee rough road kama 1km to & from ndio uendelee na safari.

Oilcom Mbezi Kwa Yusufu wamefunga njia ya kuingia hadi uzunguke nyuma ya sheli.

Ukija Temboni sasa, kuingia hadi uzungukie kile kibarabara cha vumbi kama unarudi Msuguri ndio uingie sheli.

Yaani kama unaelekea mjini sheli isiyo na kizuizi ni Puma iliyopo Baruti.

Huu ni usumbufu usio na ulazima, wangeweza kuacha nafasi kidogo ili huduma ya upatikanaki wa mafuta kwa watumiaji wa vyombo vya moto uwe rahisi.

Tunajua sheli zipo kwenye hifadhi wa barabara inayomilikiwa na Serikali ila kwa wakati huu wakati mkiweka mambo sawa na wamiliki wa sheli sisi wananchi tusipate huu usumbufu.

Nawasilisha!
 
Kuna siku naenda mkoa kidogo niaibike. Sema mafuta yalinisitiri nikafika mpka kibaha, ila kuanzia Mbezi mwisho sikuona hata sehemu moja ya kuchepuka kuingia sheli.
Mkuu ni kero sana umeosha gari lako lakini ili kuweka mafuta lazima uchafue gari.
 
Tatizo mnamiliki magari bila kujiandaa.


Weka mafuta yakiwa yamebaki ya kuendesha km 50!


Mie kwenye sanlg yangu wese napimia kidole. Kisipogusa mafuta najazia. Tena huu mwaka wa 6 sijaishiwa mafuta.... Hata ile wiki mafuta yaliadika fisi wangu aliendelea kupumua moshi.
 
Kuna ORYX pale Kimara Resort.

Kama unaelekea ueleko wa shamba, hakikisha umejaza mafuta ya kutosha pale Puma au Oryx.

Zaidi ya hapo petrol station ya kueleweka mpaka Njuweni Maili Moja.
 
Tatizo mnamiliki magari bila kujiandaa.


Weka mafuta yakiwa yamebaki ya kuendesha km 50!


Mie kwenye sanlg yangu wese napimia kidole. Kisipogusa mafuta najazia. Tena huu mwaka wa 6 sijaishiwa mafuta.... Hata ile wiki mafuta yaliadika fisi wangu aliendelea kupumua moshi.
Swala sio kwenda mara kwa mara ila ule usumbufu wa kuingia kituo cha mafuta hata kama ntaenda mara moja kwa wiki.
 
Back
Top Bottom